Zaka za Dhahabu na Fedha

17232

 

 

Maana ya Dhahabu na Fedha

Dhahabu na Fedha

Dhahabu na fedha, na chochote kinachosimamia nafasi ya vitu hivi viwili miongoni mwa pesa za karatasi zinazotumiwa siku hizi.

Hukumu ya Zaka ya Dhahabu na Fedha.

Ni lazima; kwa kauli ya Mwenyezi Mungu U: {Na wale wanaokusanya dhahabu na fedha wala hawazitoi katika njia ya Mwenyezi Mungu, wape habari za adhabu inayoumiza } (At-Tawbah 34)

na kwa kauli ya Mtume ﷺ: ( Mtu yeyote aliye na hazina ya dhahabu na fedha na wala haitolei Zaka basi atachomwa nayo katika moto wa Jahannam na itajaaliwa kama vinoo ambavyo atapigwa navyo kwenye migongo na vipaji kila akipata ubaridi (yakipoa makali ya moto) anaregelewa tena (kupigwa navyo), mpaka Allaah Amalize kuhukumu waja wake siku ambayo ni sawa na miaka elfu khamsini. Kisha ndio ataoneshwa njia yake ikiwa kama ni ya peponi au motoni” [Imepokewa na Muslim.].

Masharti ya kuwajibika kutolewa kwa zaka ya Dhahabu na Fedha

1. Kupitiwa na mwaka.

2. Kuzimiliki kiukamilifu.

3. kufika nisabu ya zaka.

Nisabu ya zaka ya Dhahabu na Fedha

1. Nisabu ya dhahabu ni Dinari ishirini (85gms)

2. Na Dinari moja ya dhahabu = (ina dhahabu) gramu nne na robo, hivyo basi inakuwa nisabu ya dhahabu kwa gramu 4.25 x 20 = 85gms za dhahabu safi (ambayo haikuchanganywa na kitu).

3. Nisabu ya fedha ni Dirham mia mbili (595 gms)

Na Dirham moja ya fedha = (ina fedha) 2.975gms, hivyo basi inakuwa nisabu ya fedha kwa gramu = 2.975 x 200 = 595gms za fedha safi.

Mfano: Ikiwa gramu moja ya dhahabu = inauzwa Dolari 30, basi inamlazimu mtu kutoa zaka ikiwa amefikisha 85 x 30 = Dolari 2550 dolari.

Dhahabu
Fedha
Pesa za karatasi

Kiwango kinachofaa kutolewa zaka ya Dhahabu na Fedha

Kiwango kinachomlazimu mtu kutoa zaka katika dhahabu na fedha na stakabadhi za kiashirio cha pesa ni robo ushuri = 2.5%.

Basi kwa kila Dinari ishirini ya dhahabu atatoa zaka nusu Dinari, na itakayozidi (zaidi ya Dinari ishirini) itapigiwa hisabu, iwe imezidi kidogo au sana.

Na kwa kila Dirhamu mia mbili za fedha atatoa zaka Dirhamu tano, na kitakachozidi atakipigia hisabu; kwa kauli ya Mtume ﷺ: (Ikiwa unamiliki Dirhamu mia mbili, na zimekamilisha mwaka, basi yatakiwa utoe Dirhamu tano, na si juu yako kutoa chochote – yaani – katika dhahabu mpaka umiliki Dinari ishirini, basi ukiwa na Dinari ishirini, na umemaliza nazo mwaka, basi itakulazimu utoe nusu ya Dinari, na zitakazozidi utafanya kwa hisabu hii) [Imepokewa na Abu Daud.].

- Mfano wa kufahamisha:-

Mtu anamiliki Dolari 9000, na imepita mwaka mzima hali ya kuwa anazimiliki hizo pesa, je analazimika kutoa zaka?

Kwanza: Tutahisabu nisabu ya zaka kwa mtizamo wa dhahabu au fedha kama ifuatavyo:

Nisabu = Gramu thamanini na tano katika dhahabu safi = 85 x bei ya gramu moja ya dhahabu safi (inavyouzwa) siku ile ya kulazimika kwake kutoa Zaka, na tukisie kwamba gramu moja yauzwa = Dolari 30.

= 85 x 30 = Dolari 2550.

Kwa hivyo Nisabu yake = Dolari 2550, hivyo basi itakuwa mali ya mtu huyu imefika nisabu, na imekamilisha mwaka mzima, kwa hivyo inamlazimu kutoa zaka.

Pili: Tutahisabu kiwango anachofaa kutoa zaka kama ifuatavyo: -

Kiwango cha kutolewa zaka = 2.5%.

= 9000 x 2.5/100 = Dolari 225.

Kwa hivyo huyu mtu yafaa atoe kutoka kwa mali yake Dolari 225 kama zaka.

- Kukusanya Dhahabu na Fedha pamoja

Mtu anapo miliki dhahabu na fedha lakini zikawa hazifikii kiwango cha kutolewa zaka, kauli yenye nguvu ni kuwa hatowajibika kutoa zaka, wala hata zikikusanywa pamoja ili zifikiye kiwango, kwani uwajibu ni kutoa dhahabu pekeyake na fedha pekeyake kwa sababu ni vitu viwili tofauti, na hakuna dalili ya kuzikusanya pamoja ili ifikie kiwango, na kwa neno lake Mtume (Hakuna chini ya wakiya tano zaka) [Imepokewa na Bukharin a Muslim]

na atakae zikusanya dhahabu na fedha itakuwa amewajibisha zaka chini ya wakia tano

Zaka ya mapambo ya wanawake

Mapambo ya wanawake yako sampuli mbili: Mapambo ya dhahabu na fedha, na mapambo yasiyokuwa ya dhahabu wala fedha.

1. Mapambo ya dhahabu na fedha.

Kitengo cha kwanza: Mapambo yaliyokusudiwa kwa lengo la kuhifadhiwa au kuwekwa kama akiba ya baadaye kunapotokea jambo, au imenunuliwa kwa nia ya kufanya biashara, basi zaka hapa ni lazima kutoa.

Kitengo cha pili: Mapambo yaliyokusudiwa kwa lengo la kutumiwa, basi uzuri zaidi ni kuitolea zaka ili kijiepusha na lawama, kwa hakika mwanamke mmoja alimjilia Mtume ﷺ pamoja na binti yake, na mkononi mwa binti yake kuna bangili mbili [ Imepokewa na Abu Daud.] nzito za dhahabu, (Mtume ﷺ) akamwambia: “ Je watolea zaka hizi bangili) Akasema: Hapana. Akasema (Mtume ﷺ): (Je utafurahia Mwenyezi Mungu akuvalishe bangili kwa hizi bangili mbili za moto?) Akasema: Yule binti akazivua, akampatia Mtume ﷺ, kisha akasema: “Hizo ni za Mwenyezi Mungu na Mtume wake” [Imepokewa na Abu Daud.]

Na kuna wanavyuoni ambao hawawajibishi mapambo ya wanawake kutolewa zaka; kwasababu hayo mapambo sio mali inayotarajiwa kukua, lakini ni pambo la mtu binafsi yuwatumia na kunufaika nayo kama vile nguo na fanicha na vyombo, na ni katika mahitajio ya mwanamke na virembesho vyake, na asili ya mali ni kukua au kuweza kukuzwa ndio ilazimike kutolewa zaka.

Na ubora wa hali ni mtu kutoa zaka kwa mapambo yaliyokusudiwa kwa matumizi ambayo si kinyume na sheria na kwa lengo la kujirembesha; kwasababu kauli hii iko katika hali nzuri zaidi na kujiondoa kwa lawama; kwa kauli ya Mtume ﷺ: (Wachana na linalokutia shaka na ufanye lile lisilokutia shaka) [Imepokewa na Bukhari].

Mapambo ya dhahabu.
Mapambo ya fedha.

2. Mapambo Yasiyo kuwa ya Dhahabu wala Dedha.

Kama vile almasi, yakut, lulu, na mfano wa hizi, basi vitu hivi havitolewi zaka hata vikawa vingi kiasi gani, isipokuwa vikikusudiwa kwa lengo la biashara vitatolewa zaka vitakuwa vimeingia katika mali ya biashara.

Lulu
Yakut
Almasi


Vitambulisho: