Zaka ya Mali ya biashara

14031

 

 

Maana ya Mali ya biashara

mali ya biashara

Kila kilichoandaliwa kwa lengo la kuuzwa na kununuliwa ili mtu apate faida.

Ziliitwa hivi, kwasababu hazidumu, bali hutokeza na kupotea, kwani mfanyi biashara huwa hataki hizi bidhaa ki-uhakika, bali anataka faida ya pesa.

Na bidhaa za biashara zimekusanya vitu vyote vya sampuli zote za mali ambayo sio pesa zinazotumika kununulia vitu, kama vile magari, nguo, vitambaa, vyuma, mbao, na vyenginevyo vilivyoandaliwa kwa biashara.

Vyuma
Gari
Mbao
Nguo

Hukumu ya zaka ya Mali ya biashara.

Ni lazima; kwa kauli ya Mwenyezi Mungu U: {Enyi mlioamini! Toeni katika vile vizuri mlivyovichuma, na katika vile tulivyokutoleeni katika ardhi} (Al-Baqarah: 267).

Jumla ya wanavyuoni wametaja kwamba makusudio ya aya hii ni: Zaka ya mali ya biashara, na kwa kauli ya Mwenyezi Mungu U: {Chukua kutoka kwa mali zao sadaka} (At-tawbah: 103) , na mali ya biashara ni katika mali zilizo dhahiri, basi Kwa ajili hii ikawajibika kutolewa zaka.

Masharti ya kulazimika mtu kutoa zaka ya Mali ya biashara.

1. Kiwango chake kifikie nisabu, na nisabu inakadiriwa kwa kipimo cha dhahabu na fedha.

2. Ikamilishe mzunguko wa mwaka mzima.

3. Iwe imekusudiwa kwa lengo la biashara; na hii ni kwamba iwe imekusudiwa kama kuchuma; kwa kauli ya Mtume (saw): “Hakika ya matendo ni kwa niya ya mtu” [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Mtu atakapobadilisha niya yake kutoka kwa biashara na kutumia bidhaa hizo basi hukatika hisabu ya mzunguko (mwaka), na akirudia niya ya biashara ataanza tena upya kuhisabu mzunguko mpya, ila akiwa amekusudia kufanya udanganyifu kwa lengo la kuondosha jukumu la kutoa zaka, basi hapa mzunguko haukatiki.

- Mfano: mtu anunue ardhi mwezi wa mfungo nne kwa nia ya kufanya biashara kisha alipofika shabani akageuza nia na akakusudia kujenga nyumba ya kukaa, hapa mwaka utakatika, kisha mfungo mosi akamua kuifanyia biashara mwaka wake utahisabiwa mfungo mosi ila kama alifanya hivyo kwa njia ya hila na kukimbia asitoe zaka basi mwaka hautakatika.

Jinsi ya kutoa zaka ya Mali ya biashara

Mali yanapo pitiwa na mwaka zinakaguliwa bidhaa alizouza na kupewa bei ile ambayo kwamba iko sasa sokoni, kisha inatolewa zaka ya hayo mali kwa kutolewa bidhaa zenyewe au kima chake kwa njia ya pesa, kulingana na mahitaji ya mafakiri.

Vipi mfanyi biashara atafanya hisabu ya zaka ya mali ya biashara?

1. Atahisabu vitu vyote alivyonavyo katika bidhaa za biashara kwa kima cha wakati wa sasa.

2. Ataongeza pesa zote alizonazo, sawasawa iwe pesa zile alizitumia katika biashara ama hakuzitumia.

3. Aongeze vyote anavyodai watu katika madeni.

4. Aondowe chochote anachodaiwa.

5. Atoe Zaka kwa yatakayobakia (baada ya kufanya hivi vyote), nayo ni robi ushuri (2.5%)

Zaka inayowajibika kutolewa = (kima cha bidhaa za biashara + pesa + madeni anayodai watu – madeni anayodaiwa) x (kiwango cha kutolewa Zaka 2.5%).

- kuhisabu zaka za biashara hutizamwa mali ya zaka yaliko atazifafanua na azitie kima siku ile yakupasa zaka akijisaidia na orodha ya hisabu ya mali bila yakuzingatia faida au hasara katika hisabu ya faida na hasara

- Vitu viliyo tayarishwa kwa ajili ya kubebea mali kama mifuko au mikebe havitiwi kima pekeyake ikiwa havikununuliwa kwa ajili ya kuviuza pekeyake, ikiwa zitatumiwa kwa kuviuza kibiashara basi vitatiwa kima vikiwa hupita kima cha mali yale. ikiwa havizidi kwa kima kama karatasi za kukunjia hivingii katika kutuwa kima.

- kutia kima huwa kwa Mfanya biashara yeyote awe ni wakuuza jumla au rejareja kwa thamani ambayo aweza kununuliya mwisho wa mwaka kima cha mabadaliko Nacho hutofautiana na bei ya kuuza na kima cha kuuza sokoni au cha tarehe au nukuu.

- bei zikitofautiana wakati wa kupasa zaka na wakati wakuzitoa inazingatiwa yatapewa siku ya kupasa ni sawa zizidi ama zipunguwe.

Na kuhusiana na suala la kutoa zaka kwa bidhaa zinazo safirishwa kabla ya kuzipokea, zaka za bidhaa hizi zitamuhusu yule anayezimiliki. Na umiliki wake unapatikana kwa kuzipokea bidhaa iliyonunuliwa kwa maelezo ya kuwa ipo njiani. Ikiwa imenunuliwa kwa mfano makabidhiano ya msingi yawe katika bandari (gati) la muuzaji. Umiliki halisi utapatikana kwa kupokea shehena hiyo. Na ikiwa imenunuliwa na makabidhiano ya msingi yawe katika bandari (gati) la mnunuzi basi umiliki wa mali hii unapatikana na kwa kitendo cha kufika tu shehena ya mali hiyo katika bandari (gati)..

- mali ya biashara yakiwa ni ya pesa mbali mbali, au ni dhahabu au fedha basi hutiwa kima kwa kujuwa kiwango kinacho pasa kutowa kwa sarafu ambayo aitumia mfanya biashara na hilo ni kwa bei ilioko siku ya kupasa zaka.

- na mizigo ya biashara ambayo mwenye kununua alitangulizia kuilipia lakini hajapokea ile mizigo basi zaka zake hazimpasi mwenye kununua bali humpasa mwenye kuuza.

Zaka za malighafi yakutumika kwa sanaa na vyenye kusaidia

1. Ama malighafi ya kimsingi yaliyo tayarishwa kwa ajili ya sanaa kama chuma kwa ajili ya kutengeneza magari, na mafuta ya kutengeneza sabuni, inapasa kutolewa zaka kulingana na thamani ambayo zilo nunuliwa mwisho wa mwaka, haya vilevile ni kwa wanyama na nafaka na mimea na kama hivyo.

2. Vitu vya kusaidia ambavyo haviingi kwenye orodha za kufanyia vitu vya sanaa kama vitu vya kuchomea havina zaka ni kama mali thabiti.

3. Zaka za bidhaa zisokuwa za sanaa na ambavyo havijesha kutengezwa:

4. Hutolewa Zaka zisizokuwa za sanaa

Na ambazo hazijesha kutengenezwa, zaka za mali ya biashara kulingana na thamani yake kwenye yalivo hivi sasa mwisho wa mwaka

- Kukusanyika sababu nyengine ya zaka pamoja na mali ya biashara

Yakikusanyika pamoja na mali ya biashara mali mengine yakutolewa zaka kama mali yamakulima hutolewa zaka za mali ya biashara

Sampuli ya Mali Yasiyopaswa Zaka

- Mali yanayo toka baharini kama lulu, na marijani, na Samaki, ila yakiwa ni Mali ya kufanyia biashara hutolewa zaka za Mali ya Biashara.

- Mali yaliyo tayarishwa kuajirishwa kama majumba na magari hayana zaka, zaka zake ziko kwenye ijara lake likifikia kiwango cha zaka na kupitiwa na mwaka.

- Vyombo vya dharura zake kama gari na nyumba hayana zaka.

Kumiliki Nisabu

Je inashurutishwa kumiliki nisabu katika kipindi chote cha mwaka, mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka? Ama yatosha kukamilika kwa nisabu mwanzo wa mwaka na mwisho wake? Ama mazingatio ni kukamilika kwa nisabu mwisho wa mwaka?

Mazingatio ni kukamilika kwa nisabu mwanzo wa mwaka na mwisho wake; kwa ugumu wa kuweka vipimo vya kipindi chote cha mwaka mzima, basi inazingatiwa mwanzo wa mwaka kwa kupatikana sababu ya kulazimika kutolewa kwa zaka, na mwisho wa mwaka kukamilika mzunguko wake, na wepesi kwa muislamu ni kujiwekea mda maalumu kama vile mwezi wa Ramadhani au mwezi wowote ule kuhisabu mali yake na kuitolea zaka.

Zaka ya Raslimali
Kinachotolewa zaka katika mali za biashara ni raslimali ambayo kwamba imekusudiwa kwa lengo la kununua na kuuza ili mtu apate faida, ama raslimali ambayo kwamba ni ya mali za kukaa hazizunguki katika biashara yaani si za kununuliwa ili ziuzwe, basi raslimali kama hii haihisabiwi wakati wa kuhisabu bidhaa za biashara wala haitolewi zaka, mfano wake ni kama makabati, na jokofu/firiji ambazo zinahifadhi bidhaa za kuuzwa, na magari yanayobeba bidhaa, na vyombo vya kubebea bidhaa, na mfano wake.

Zaka za Hisa

Maana ya Hisa

Hisa.

Sehemu anayolipwa mtu baada ya kupatikana faida katika sehemu zilizo sawa kutokana na raslimali ya mtu aliyotowa kwenye shirika la umoja wa kuchanga

Mfano wake: Shirika la umoja wakuchanga lina raslimali Dolari milioni tatu, iligawanywa raslimali yake wakati wa kufunguliwa kwake vigawanyo elfu kumi, kila kigawanyo Dolari (300), kigawanyo hichi ndio hisa, na mwenye hisa ni mshiriki katika shirika kwa kiwango cha alichonacho katika hisa.

Hukumu ya kuzunguka kwa zaka ya Hisa.

Ni Mubah, Inaruhusiwa iwapo kazi ya shirika hilo si haramu, au haina mambo yaliyoingiliana na riba.

Namna ya kutoa zaka za Hisa

Idara ya kampuni itabeba jukumu lakuwatolea zaka kwa niyaba yao ikiwa imeelezwa hilo kwenye mpango wake wa kimsingi, au awe ametegemezea hilo Yule mwenye hisa

- Idara ya kampuni ikibeba jukumu la kutoa zaka kongamano la fiqhi la umoja wa mua’tamr wa kislamu kwamba zaka zimefungamanishwa na kapuni kwa kuizingatia kuwa ni mtu wakimazangatiwa likichukuliwa kutoka kwenye kaida ya kuchanganya iliyoko kwenye sunna takatifu kuhusu zaka za wanayama, na wamezieneza baadhi ya wanavioni wa fiqihi kwa mali yote kwa kuwa huzingatiwa mali ya wote wenye kuchangia ni kama mali ya mtu mmoja na hufardhiwa zaka kwa mazingatiwa haya kuhusu kiwango na kiyasi cha zaka na mfano wa hayo

- Msimamo wa jumhuri ya wenye ilimu nikutoishika kaida ya kuchangaya katika zaka za makampuni bali huangaliwa fungu la kila mwenye kushiriki peke peke.

Na ni muhimu kutaja kwamba mkutano wapili la kongamano la kiutafiti wakiilimu umefuata maoni ya jamhuri kwenye kadhia haukushika kaida ya kuchangaya bali iliyatizama kila mali peke yake kwa hivyo ukapitisha yafuatato:

- Kwenye makampuni haya ambayo wanashiriki watu kadha hautizamwi mkusanyiko wa faida za kampuni bali huangaliwa kila yenye kumkhusu mwenye kushiriki pekeyake

- na niwajibu juu ya idara ya kampuni kuweka mbali hisa zisizopaswa na zaka kama hisa za waqfu ya mambo ya kheri, na hisa za makundi ya mambo ya kheri, na asili ya mali thabiti, ambavyo hayapaswi na zaka kama majengo, na maofisi na vyombo, na magari mahsusi na kampuni ikitowatolea zaka hapo itawalazimu wenye hisa kujitolea wenyewe kwa namna ifuatayo:

1. Hisa za makampuni za makulima hutolewa zaka zake kama zaka za nafaka na matunda.

2. Hisa za makampuni ya biashara hutolewa zaka zake, mali ya asili na faida zote, na hukisiwa hisa kwa kima cha sokoni wakati wakuwajibika zaka.

3. Hisa za makampuni ya sanaa hutolewa zaka zake faida safi wala sio vyombo vya kukodisha na majengo na mfano wake.

4. Akiuza mwenye hisa hisa zake wakati wa kupitiwa na mwaka yatakuswanya thamani ya mali yake, na atayatolea zaka, ama mwenye kunuwa atatolea hisa alizo nunuwa kwa namna ilivo tangulia.



Vitambulisho: