Ngamia, Ng’ombe, Kondoo na Mbuzi.
Ngamia, Ng’ombe, Kondoo na Mbuzi.
Ni lazima; kwa kauli ya Mtume (saw): (Hakuna mwenye ngamia, wala ng’ombe, wala kondoo na mbuzi, ambaye hatoi Zaka ya vitu hivi isipokuwa atakuja (mnyama huyu asiyetolewa Zaka) siku ya Kiama hali ya kuwa amenona sana, (Mnyama huyo) atampiga mtu wake kwa pembe zake, na atamkanyaga kwa kwato zake [ Kwato: sehemu ya chini katika mguu wa mnyama anyotumia kukanyagia na kutembelea.], kila anapoisha wa mwisho anarudi tena wa kwanza, mpaka watakapohukumiwa watu wote) [Imepokewa na Muslim].
1. Wanyama wawe wamekamilisha mwaka mzima wakiwa kwa mwenye kuwamiliki; kwa kauli ya Mtume(saw) : (Hakuna Zaka kwa mali yoyote mpaka ipitiwe na mzunguko mwaka) [Imepokewa na Ibn Maajah].
2. Awe ni mnyama wa kwenda malishoni; kwa kauli ya Mtume (saw): “Kwa kila ngamia wa kwenda malishoni, kwa kila ngamia arubaini (toa zaka) ibn labun mmoja” [Imepokewa na Nasaai.].
Na ngamia anayekwenda malishoni: Ni yule ambaye chakula chake ni mimea ya ardhini, na nyasi zilizoruhusiwa – Nazo ni zile zilizomea kwa kujaaliwa na Mwenyezi Mungu bila kupandwa na mtu; ama ikiwa chakula cha mnyama huyo ni kile ambacho mfugaji anakipanda mwenyewe, basi mnyama huyo haihisabiwi kuwa ni mnyama wa kwenda malishoni hivyo basi hatolewi Zaka mnyama huyo.
3. Awe ni mnyama aliyekusudiwa kufaidisha watu kwa Maziwa yake na kuongeza idadi kuzaa au kuzalisha, asiwe mwenye kubebeshwa Mizigo, na ngamia mwenye kubeba mizigo: Ni yule anayetumika kulima shamba au kunywesha Maji Ardhi au kubeba vyombo au kubeba mizigo mizito.Na ngamia mwenye kubeba mizigo hawajibiki kutolewa Zaka, kwasababu kwa hali hii anaingia katika mahitaji ya mtu ya ki-asili kama vile nguo. Ama akikusudiwa kwa lengo la kukodishwa basi Zaka yake itakuwa ni katika yale yanayopatikana kwenye malipo ya kukodishwa, pindi utakapokamilika mwaka.
4. Wawe wanyama wamefika nisabu ya kisheria ya zaka.
Kutoka kwa Anas Ibn Malik radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie, kwamba Abubakar Swidiq radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie alimuandikia: (Hii ni faradhi ya Zaka ambayo kwamba ameifaradhisha Mtume (saw) na wakaitekeleza waislamu, na ambayo kwamba Mwenyezi Mungu amemuamrisha Mtume wake (saw), kwa kila ngamia ishirini na nne na chochote kilichoko chini ya hapo katika mbuzi. Katika kila ngamia watano (atoe Zaka) mbuzi mmoja. Na wakifika ngamia ishiri na tano hadi thelathini na tano atoe binti makhaadhw mmoja [ Binti makhaadhw: Ni ngamia wakike aliyekamilisha mwaka moja.] wa kike. Wakifika thelathini na sita hadi arubaini na tano atoe binti labun mmoja [ Binti labun: Ni ngamia wakike aliyekamilisha miaka miwili.] wa kike. Wakifika arubaini na sita hadi sitini atoe hiqqah mmoja [ Hiqqah: Ni ngamia wakike aliyekamilisha miaka mitatu.]. Wakifika ngamia sitini na moja hadi sabini na tano atoe jadh.a’ mmoja [ Jadh-a’: Ni (ngamia wakike) aliyekamilisha miaka mine.]. Na ambaye hana isipokuwa ngamia wanne basi hana Zaka ya kutoa isipokuwa mfugaji mwenyewe akitaka kutoa, na wanapofika ngamia watano atatoa mbuzi mmoja [ Wala hairuhusiwi katika kondoo au mbuzi anayetolewa isipokuwa kondoo aliyefikisha miezi sita, na mbuzi aliyefikisha mwaka mmoja..] “ [ Imepokewa na Bukhari.].
Idadi ya ngamia | kiwango kinachowajibika kutolewa Zaka |
5 : 9 | Mbuzi mmoja |
10 : 14 | Mbuzi wawili |
15 : 19 | Mbuzi watatu |
20 : 24 | Mbuzi wane |
25 - 35 | Binti makhaadhw (aliyefikisha mwaka) |
36 - 45 | Binti labun (ali efikisha miaka miwili) |
46 - 60 | Hiqqah (aliyefikisha miaka mitatu) |
61 - 75 | judh’a |
76 - 90 | Binti labun wawili |
91 - 120 | Hiqqah wawili |
120:.... | Nakwakila ngamia 40 Binti labuni Na kwakila ngamia 50 Hiqqah |
Kutoka kwa Muadh Ibn Jabal radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie asema: (Mtume (saw) alinituma kwenda Yemen, akaniamrisha nichukue (yaani Zaka kutoka kwa watu wa Yemen) kwa kila ng’ombe thelathini tabia’ mmoja [ Tabii’ na Tabiia’: Ni ng’ombe aliyekamilisha mwaka mmoja.], na kwa kila ng’ombe arubaini musinna mmoja) [ Musinna: Ni aliyekamilisha miaka miwili.]” [Imepokewa na Abu Daud.].
Idadi ya ng›ombe | Kiwango kinachowajibika kutolewa Zaka |
30 – 39 | Tabii’ (ng’ombe aliyefikisha mwaka mmoja) |
40 – 59 | Musinnah (ng’ombe aliyefikisha miaka miwili) |
60 – 69 | Tabii’ wawili |
70 – 79 | Tabii’ mmoja na Musinnah mmoja |
Imepokewa kutoka kwa Anas radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie, kwenye Hadith iliyotangulia: (Na Zaka ya kondoo na mbuzi wanaokwenda malishoni ikiwa wamefikia arubaini hadi mia na ishirini ni mbuzi mmoja, wakizidi mia na ishirini hadi mia mbili watolewe mbuzi wawili, wakizidi mia mbili mpaka mia tatu watolewe mbuzi watatu, na wakizidi mia tatu basi kwa kila mia atoe mbuzi mmoja, na ikiwa mtu ana kondoo au mbuzi wanaokwenda malishoni lakini ni chini ya arubaini basi mtu huyu hana Zaka yakutoa, isipokuwa mfugaji akipenda mwenyewe kutoa) [Imepokewa na Bukhari.].
Idadi ya kondoo au mbuzi | Kiwango kinachowajibika kutolewa Zaka |
40 - 120 | Mbuzi mmoja |
121 - 200 | Mbuzi wawili |
201 - 300 | Mbuzi watatu (na kila wakizidi mia anazidi mbuzi mmoja) |
Wajibu katika kutoa zaka ni zitokamane na mali ya katikati siyo yale yaliyo bora mno wala yalio maovu, ni wajibu wa msimamizi wa zaka atunze miaka yenye kupasa kwa kuwa hazitoshelezi duni ya hizo, kwa sababu ni kuwadhuru mafukara, wala hatukiwi ya mali juu yake kwa sababu ni kuwadhulumu matajiri, na vile vile hachukui mgonjwa na mwenyeila na mkubwa mkongwe, kwa sababu hamnufaishi fukara, kwa upande mwingine hamchukuwi wakuliwa aliyenona aliye tayarishwa kuliwa, wala aliye mlezi mwenye mtoto wala mwenye mimba wala wenye kupendeza macho ambayo ni yale mali matukufu ambayo kuyachukuwa ni kumdhuru tajiri kwa kuwa mtume alisema (Tahadharini na mali yao matukufu) [Imepokewa na Bukhari]
Nao ni sambuli mbili
Nako nikuwa yale mali yameshirikiana, baina ya wawili katika kumiliki kwa kueneya kati mwao kiyasi chakuwa fungu la mmoja halijipambanui na la mwingine, na kuchangaya huku huwa kwa kurithi au kwa kununua
Nako nikuwa fungu la kila mmoja nilenye kulibaini kwa kujulikana na hukusanywa pamoja kwa ujirani tu.
Nako kwa sampuli zake zote mbili huyafanya mali hayo kuwa kama mali ya namna moja, mkusanyiko wake ukifikia kiwango,
Na awe washirika wa wiwli ni miongoni mwa wenye kupaswa kutoa zaka, ikiwa mmoja wao ni kafiri kutangamana hakusihi, wala hakuwi na athari, na hushirikiyana mali mawili kwenye kulala pamoja na kuishi na yashirikiyane kwenye kwenda malishoni wanakwenda pamoja na kurudi pamoja na kukamuliwa maziwa, na malisho na fahali wa kupiga awe ni mmoja, yakipatika masharti haya mali mawili huwa nikama mali ya namna moja, kwa neno lake Mtume (saw) (Havikusanywi vilio tafauti wala haviwekwi mbali vilo pamoja kwa kuogopa kutoa zaka na yenye kuwa yawashirika wawili wataregeleyana kati mwao kwa usawa) [Imepokewa na Ibnu Khuzeymah]
kuchanganyisha kuna athari kuhusu kupasa zaka nakuto pasa, na hilo la husiana na wanyama tu.
Na mfano wa kukusanya kati ya walio mbali mbali
Ni watu wa tatu kila moja amiliki wanyama 40 wote ni mia na ishirini lau tungemzingatia kila mmoja peke yake wangepasa kutoa mbuzi watatu, lakini tukiwakusanya mbuzi wote hapasi ila mbuzi moja, hapa huwa wamekusanaya walio mbalimbali ili wasipaswe na mbuzi wa tatu bali mbuzi moja.
Na mfano wakuweka mbalimbali yaliyo pamoja
Ni mtu akawa na mbuzi arubaini akija mwenye kukusanya zaka akawaweka mbali mbali ishirini ishrini, ili wasichukuliwe zaka kwa kutofikia kiwango