Yanayo faa, na yanayo chukiza, na yale yanayo vunja Swalah

10580

 

Kwanza: Yanayo faa katika Swalah

1. Kutembea katika Swala kwa tukio muhimu kwa sharti ya kutogeuka upande wa kibla kama kufunguwa mlango

2. Kubeba mtoto katika Swalah

3. Kuuwa nyoka na n’nge katika Swalah

4. Kuzunguka katika Swalah kwa dharura

5. Kulia katika Swalah

6. Kuleta tasbihi kwa wanaume na kupiga makofi kwa wanawake

7. Kumfunguza Imamu

8. Kuashiria kwa kidole kwa ajili ya kurudisha salamu au kwa mkono

9. Kutoa ishara ya kufahamisha kwa anae swali wakati akitokewa na haja

10. Kumshukuru Mwenyezi Mungu anapoona linalo kupelekea kufanya hivyo

11. Kutema mate na kohozi katika Swala upande wakushoto

12. Kumzuia anaepita mbele ya mwenye kuswali

Pili: Yanayo chukiza katika Swalah

1. Mtu kuswali akiwa na mawazo mengi yenye kumshawishi, ama mbele yake kuna jambo la kushugulisha na swala yake, kama kujizua na haja ndogo ama kubwa ama upepo, au akiwa na njaa au kiyu ama kuwa mbele yake chakula anacho kipenda, au kutazama kitu kinacho mshughulisha na swala yake

2. Kufanya jambo lenye kukutowa kwenye unyenyekevu na utulivu katika swala, mfano kufanya harakati nyingi bila ya haja, na kuchezacheza na ndevu na nguo na kilemba na saa na kuvialisha vidole na kuvishikanisha na mfano wa hayo

3. Kuzunguka kwa uso katika Swala bila ya haja kwa sharti mwili uwe umeelekea kibla, lakini mwili ukitoelekea kibla swala itaharibika

4. Nakushika kiuno kwenye swala kama wanavofanya mayahudi

5. kuufunga mdomo na pua katika swala

6. Kukunja nguo kama mikono ya kanzu na mfano wake

7. Kuzifunga nywele kwa anaekuwa na nywele nyingi ili anapo sujudu zi sisujudu pamoja na yeye

8. Kutema mate ama kohozi mbele ya kibla au upande wake wa kulia

9. Kutizima mbingu

10. Kufumba macho bila ya haja

11. Kunyosha mikono wakati wakusujudu.

Tatu: Mambo yanayo Haribu Swala

1. Kufanya jambo linalo pingana na sharti miongoni mwa sharti za swala kama kufanya jambo lenye kutenguwa twahara, au kukusudia kufunguwa uchi, au Kuzunguka upande wakibla, kwa mwili wake, au kuvunja nia

2. kukusudia kuacha nguzo au wajibu wa swala.

3. kujishughulisha na vitendo vingi kwa kitendo nje ya swala bila ya dharura kama kutembea na haraka nyingi

4. Kucheka na kujikohoza

5. Kuzungumza ndani ya Swala kwa kusudi

6. Kula na kunywa kwa kusudi.

7. Kuzidisha Rakaa au Nguzo kusudi

8. Maamuma kutoa salamu kabla ya imamu wake