Wudhuu Unatenguka Akipeana Mkono Au kugusana Na Asiye Muislamu?

SWALI: Kupeana mikono kwa kusalimiana na mtu mwanaume mwenzangu lakini si muislamu (mkristo) inatengua UDHU?

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani kwa swali lako kuhusu kutenguka wudhuu kwa kusalimiana na asiyekuwa Muislamu. Kupeana mkono na asiyekuwa Muislamu hakutengui wudhuu kabisa. Hilo si miongoni mwa mambo yenye kutengua wudhuu. Huenda watu wengine wakafikiria hilo kwa kuwa Allaah Aliyetukuka Ameiwaita ni najisi katika Suratut Tawbah lakini najisi walio nayo ni ule ukafiri wao wala sio unajisi kama ule unaojulikana kama wa mkojo, kinyesi na vitu vinginevyo. Na Allaah Anajua zaidi




Vitambulisho: