Wanaostahiki kupewa Zaaka na kutowa Zaaka

24785

 

Wanaostahiki kupewa Zaka

Ni wale ambao kwamba wanastahiki kupewa Zaka, nao watu aina nane ambao kwamba Mwenyezi Mungu U Amewahisabu katika kauli yake: {Sadaka hupewa (watu hawa): - Mafakiri na Masikini na Wanaozitumikia na Wanaotiwa nguvu nyoyo zao (juu ya Uislamu) na katika kuwapa Uungwana watumwa na katika kuwasaidia wenye deni na katika (kutengeneza) mambo aliyoamrisha Mwenyezi Mungu na katika (kupewa) Wasafiri (walioharibikiwa). Ni faradhi inayotoka kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi (na) Mwenye hikima} (At-Twba – 60).

1. Mafakiri

Mafakiri

Ni wingi wa fakiri, naye ni yule ambaye hawezi kujitosheleza mahitaji yake ya dharura na mahitaji ya aliyechini yake, katika chakula na kunywa na mavazi na makazi.

Na yuwapewa katika Zaka kitakachomtosha yeye na familia yake kipindi cha mwaka mzima.

2. Masikini

Masikini

Ni wingi wa masikini, naye ni yule ambaye kwamba anapata nusu ya mahitaji yake, au zaidi ya nusu, kama yule ambaye ana mia moja, na anahitaji mia mbili. Na anapewa mtu kama huyu kiasi kitakachomtosha sawa na mahitaji yake na familia yake kwa mda wa mwaka mzima kutoka katika Zaka.

3. Wanaotumikia Zaka

Wanaotumikia Zaka

Wale ambao kwamba wanakusanya Zaka kwa idhini ya viongozi, na wanachukua jukumu la kugawa Zaka hiyo kwa wanaostahiki kupewa.

Na watapewa katika mali ya zaka kiyasi ya ujira wao na kazi yao hata kama wako nauwezo, kwa sababu ameacha kazi yake kwa ajili ya kazi hii, isipokuwa kama walipwa na serekali basi hawatopewa zaka, na huhisabiwa ni wenye kukusanya zaka kila anae shughulika, anaye kusanya na anaye andika na anelinda na anaegawanya wote hawa wanasahiki kupewa zaka

Kupewa Zaka wanaoitumikia Zaka
Anapewa zaka mwenye kukusanya zaka na mwenye madeni hata kama ni matajiri, na mwenye uwezo wakufanya kazi ikiwa amejishughulisha nakutafuta ilimu ya kisheria na ikawa hana mali, kwa sababu kutafuta ilimu ni jihadi katika njia ya mwenyezi mungu, na vile vile mwenye kupigana jihadi na wanaotiwa nguvu nyoyo zao kwa ajili ya kusilimu.ama mwenye kukaa nakufanya ibada na akacha kufanya kazi hali yakuwa anaweza kufanya kazi huyu hatapewa zaka kwa sababu ibada faida yake ya mrudia yeye mwenyewe tafauti na mwenye kutafuta ilimu.{ Enyi mlio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa. Shet’ani anakutieni khofu ya ufakiri na anakuamrisheni mambo machafu. Na Mwenyezi Mungu anakuahidini msamaha na fadhila zitokazo kwake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua.} [Al-Baqara: 267-268]

4. Waliosilimu wanaotiwa nguvu nyoyo zao juu ya Uislamu.

wanaotiwa nguvu nyoyo zao juu ya Uislamu.

Viongozi wanaoheshimika katika jamii yao, kwa wanaotarajiwa kwamba kupewa kwao kunaweza kuwa sababu ya kusilimu, au kuzuia shari zao, au kutia nguvu imani zao, au kuwakinga waislamu dhidi ya maadui zao miongoni mwa maadui zao.

Na wanapewa Zaka kwa kiwango ambacho kitafikisha kwao kutiwa nguvu nyoyo zao.

5. Watumwa ili waachwe huru

Watumwa ili wa achwe huru

Mtumwa, na Mukaatib: ni Yule Mtumwa alie andikiyana na bwanake amlipe pesa ili ajikomboe nafsi yake na utumwa, huyu atapewa zaka kulipia deni lake walilo andikiyana

Ili awe huru kila mmoja miongoni mwao kuweza kufanya harakati za kimaisha, na awe ni kiungo chenye manufaa kwa jamii, na atulizane vizuri katika kumuabudu Mwenyezi Mungu kiukamilifu, na hapa pia inaingia kuwakomboa mateka wa kivita waliotekwa nyara miongoni mwa waislamu.

6. Wenye kudaiwa madeni.

Wenye kudaiwa madeni.

Wingi wa mwenye kudaiwa madeni, naye ni yule anayefaa kulipa deni.

Na wenye kudaiwa madeni wako sampuli mbili:

Ya kwanza: Ni yule mwenye deni linalomuhusu yeye mwenyewe, basi anapewa katika Zaka kitakacho kamilisha kulipwa kwa deni lake ikiwa ni fakiri.

Ya pili: Ni aliye na deni kwasababu ya kuleta suluhisho kati ya makundi mawili ya waislamu, basi anapewa katika Zaka kitakacho kamilisha deni hilo, hata kama ni tajiri.

7. Kwa njia ya Mwenyezi Mungu

Kwa njia ya Mwenyezi Mungu

Wale wanaopigana jihadi kwa njia ya Mwenyezi Mungu.

Watu hawa hupewa kinachowatosha katika jihadi kwa njia ya Mwenyezi Mungu.

Na inaingia ndani yake mambo mengi katika mambo ya kulingania dini ambayo yanahisabiwa kuwa ni jihadi kwa njia ya Mwenyezi Mungu na wala hayakupata katika sadaka kitakachosimamia harakati zake.

8. Msafiri (Alioharibikiwa).

Msafiri (Alioharibikiwa)

Msafiri ambaye kwamba amekatikiwa na safari yake wala hakubakia na chochote katika mali.

Anapewa katika Zaka kitakachomfikisha kwao, hata kama huko kwao ni tajiri.

Mambo yanayofaa kuzingatiwa

1. Zaka haitolewi kwa watu ambao hawako katika makundi haya yaliyotajwa, hata kama ni kwa lengo la kufanya wema na hisani, kama vile kujenga msikiti, na madrasa, na mahspitali/zahanati, na mengineo katika mambo ya kheri na ambayo kwamba waweza kuyafanya katika sadaka.

2. Sio lazima kufanya uchambuzi wa kina kwa haya makundi manane yaliyotajwa wakati wa kutoa Zaka, bali yaruhusiwa kutoa kwa kundi lolote kati ya haya makundi manane.

Wale ambao hawafai kupewa Zakah.

1. Matajiri, na watu wenye nguvu nauwezo wa kukidhi mahitaji yao.

Kwa kauli ya Mtume (saw): (Wala hakuna fungu la kupewa tajiri, wala mtu mwenye nguvu anayechuma) [Imepokewa na Abuu Daud.].

2. Walio asili yako baba na mama, na walio vizazi vyako mototo, na mke, ambao ni jukumu lako kuwalisha.

Haifai kumpa Zaka muislamu ambaye ni jukumu lako wewe kumlisha, kama vile baba, mama, babu, nyanya, watoto, na wajukuu; kwasababu kuwapa Zaka watu hawa kutawatosheleza wao kula kwao ambako ni jukumu lako juu yao, hivyo basi kuondosha jukumu la kuwalisha, na hatimaye yarudi kutoa faida ya Zaka kwako mwenyewe, kama kwamba umejipa Zaka mwenyewe.

3. Makafiri wasiotiwa nguvu

Haifai kuwapa Zaka makafiri ikiwa simakusudio kuwatia nguvu, katika uislamu kwa kauli ya Mtume (saw): (Huchukuliwa kutoka kwa matajiri wao, na kupewa mafakiri wao) [Imepokewa na Bukhari.].

Yaani: Matajiri wa kiislamu na mafakiri wao pasina kuwapa wasiokuwa wao, na kwasababu miongoni mwa makusudio ya Zaka ni kuwatosheleza mafakiri wa kiislamu, na kuzidisha mapenzi na udugu kati ya w jamii ya kiislamu, na hivi haifai kwa makafiri.

Kupewa Zaka wanaoitumikia Zaka
Anapewa zaka mwenye kukusanya zaka na mwenye madeni hata kama ni matajiri, na mwenye uwezo wakufanya kazi ikiwa amejishughulisha nakutafuta ilimu ya kisheri na ikawa hana mali, kwa sababu kutafuta ilimu ni jihadi katika njia ya mwenyezi mungu, na vile vile mwenye kupigana jihadi na wanaotiwa nguvu nyoyo zao kwa ajili ya kusilimu.ama mwenye kukaa nakufanya ibada na akacha kufanya kazi hali yakuwa anaweza kufanya kazi huyu hatapewa zaka kwa sababu ibada faida yake ya mrudia yeye mwenyewe tafauti na mwenye kutafuta ilimu.{ Enyi mlio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa. Shet’ani anakutieni khofu ya ufakiri na anakuamrisheni mambo machafu. Na Mwenyezi Mungu anakuahidini msamaha na fadhila zitokazo kwake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua.} [Al-Baqara: 267-268]

4. Aali zake Mtume (saw) (Aalu Nnabiy: jamaa za mtume ni baniy Haashim)

Haifai kuwapa Zaka Aali zake Mtume ﷺ kwasababu ya utukufu wao, kwa kauli ya Mtume (saw): (Hakika hii Zaka ni uchafu wa watu (unaosafishwa), kwa hivyo haifai kupewa Muhammad, wala Aali ya Muhammad) [Imepokewa na Muslim.].

5-Vijakazi vya Jamaa zake Mtume (saw)

Nao ni watumwa ambao kwamba wamewachwa huru na Jamaa zake Mtume (saw); kwa Hadit: (Hakika ya Zaka sio halali kwetu, na hakika watumwa wa watu ni miongoni mwao) [Imepokewa na Tirmidhi.].

Yaani: Hukumu ya watumwa hao ni kama hukumu ya wenye kuwamiliki, hivyo basi ni haramu kupewa Zaka watumwa wa Bani Hashim.- Vijakazi vya Aali zake Mtume (saw)

6. Mtumwa anayemilikiwa

Haifai kupewa mtumwa Zaka, kwasababu mali ya mtumwa ni katika milki ya bwana wake, hivyo basi akipewa Zaka itakwenda kwa bwana wake, na kwasababu jukumu na kulishwa kwake ni la bwana wake. Na imevuliwa kutoka hukumu hio Almukataba (mtumwa alioandikana mkataba na bwana wake), kwani wao hupewa Zaka kiwango kitakacholipa deni la mkataba wao, na mfanyikazi wa kukusanya Zaka – pia- akiwa ni mtumwa anayetumikia Zaka atapewa Zaka, kwasababu ni kama malipo, na mtumwa anafaa kuajiriwa kwa ruhusa ya bwana wake.

Kutoa Zaka

Wakati wake

Ni lazima kutowa zaka kwa haraka inapo fika wakati wakuwajibika kwake pamoja nauwezo wakufanya hivyo, na haifai kuichelewesha kutoa iwajibikapo kutolewa ila kwa dharura, kama vile mali kuwa mbali na mji wake au mfano amefungwa na mfano wa hayo.

na dalili ya kuwajibika kuitoa kwa haraka ni kwa neno lake Mwenyezi Mungu {Na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake} [Al-an’aam 141]

Na kwa neno lake U { Na simamisheni Swala na toeni Zaka, na mti’iin Mtume ili mpate kurehemewa.} [Al-nnuur 56]

Na amri yatakikana kutekeleza kwa haraka bila ya kuchelewesha

Hukumu ya kutoa zaka Mapema

Inafaa kutanguliza kutoa zaka kwa miaka miwili au chini ya hapo, ikiwa imefikia Nisabu yakutolewa zaka Wakati wakuitanguliza kwake.

Sehemu ya kutoa Zaka

Ubora ni kuitoa zaka katika mji ambao ndipo mali yalipo, lakini inafaa kusafirisha zaka zake kupeleka mji wakaribu au wambali kwa haja, mfano ukawa mji wambali watu wake ni mafukara zaidi, au mtu awe ana jamaa zaka mafukara katika mji ule kama mafakiri wa mji wake, kwa sababu kuwapatia mafukara ambao ni jamaa zake kuna maslahi, na kwake itakuwa ni sadaka na kuunga kizazi na kauli hii ya kufaa kusafirisha zaka ndio kauli sahihi kwa kuenea neno lake mwenyezi mungu {Wa kupewa sadaka ni mafakiri na masikini na wanao zitumikia, na wakutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika njia ya Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima.} [Tawba 60] Yaani mafakiri na masikini wakila sehemu.

Mali yanayofaa kutolewa zaka na yasiyofaa kutolewa

Mali yanayo tolewa zaka ni mali ya kati na kati sio mali ya hali ya juu wala mali mbaya, haimlazimu kumtoa mnyama aliemnono au mwenye mimba au dume katika wanyama, wala tende nzuri, isipokua akiridhia kwa jambo hilo na akaridhia nafsi yake.

Kama vilevile hafai kutoa kitu kibovu na kuacha kizuri, isipokua mali yake yote yawe ni mbaya, na wanyama wake wote wawe ni wagonjwa, hapo inafaa kutoa mmoja wao.

Amesema Mwenyezi Mungu { Enyi mlio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa.} [ Al-Baqara: 267]

na katika hadhithi ( Hatolewi zaka mnayama mkongwe [ harim: mnyama aliomzee.]. wala tongo[ mwenye aibu: mwenye amabaye hakubaliwi katika mauzo.]. wala dume [ mbuzi dume ambae hajafikia umri wa kibeberu wala hana manufaa yoyote wala hana kizazi.]. ila anapotaka mwenye kutoa zaka) [Imepokewa na Bukhari.].

Na Amesema Mtume (saw) Kumwabia Muadh: (Tahadharini na mali yao matukufu) [Imepokewa na Bukhari.].

Maelekezo

1. Inampasa kwa mwenye kutoa zaka kuwatafuta wanaostahiki kupewa zaka, wala asiwape wasio stahiki kwa neno lake mtume s.a.w (hapana bahati kwa tajiri wala mwenye nguvu za kutafuta) [Imepokewa na Abuu Daud.].

2. Na mwenye kutoa zaka afanye bidii kumtafuta anaestahiki kupewa zakaa na mwenye haja, na kila zinapozidi sifa nyengi kwa mtu kwa anaestahiki kupewa zakaa basi anastahiki zaidi kupewa zakaa kama kua ni fakiri katika jamii yako, au fakiri anaetafuta ilimu na mfano wa hao

Anaestahiki zaidi kupewa Zaka
Inaetaka kutoa zaka afanye bidii kutafuta anaestahiki kupewa zaka na anaekuwa na haja zaidi na kila alie kusanya sifa za kupewa zaka huyo ndie anaestahiki kupewa zaka. Kama jamaa alie fakiri, au mwanafunzi fakiri, na kadhalika.

Mambo muhimu katika Zaka

Kima cha kutolewa Zaka

Asili ya Zaka ni kutoa kitu asili (chakula) katika kilichowajibika kutolewa, lakini yaruhusiwa ikiwa kuna haja au maslahi yanayokubalika kutoa kima chake.

Mahusiano ya Serekali na Zaka

Asili ya Zaka ya mali ni kazi ya mtawala, wala hawaachiwi wanaotoa Zaka na watu binafsi kujifanyia vipimo, basi utawala ukizembea katika jukumu hili itakuwa jukumu ni kwa mtu mwenyewe binafsi (kuangalia utekelezaji wake wa Zaka).

Kuzalisha mali ya Zaka kwa maslahi ya wanaostahiki kupewa Zaka.

Yaruhusiwa kuzalisha mali ya Zaka kwa miradi yenye manufaa yanayorudi kwa wanaostahiki Zaka hiyo, ikiwa hakuna umuhimu wa haraka wa kutumia mali hayo unaopelekea matumizi ya mara moja.

Je katika mali kuna haki isiyokuwa Zaka kwa mfano kama ushuru?

Zaka ni haki ya mzunguko iliokadiriwa katika mali, na ambayo ni lazima wa kutolewa ulazima wa asili ya mali kwa wanaoweza.

- Na katika mali kuna haki nyengine isiyokuwa Zaka, ambayo imejitenga kwa kuwa ni yenye kutokea ghafla, wala haikupimwa kwa kiwango maalumu, wala si yenye kudumu hali yake kama kudumu kwa Zaka, nayo haiwajibiki kwasababu ya mali, bali inawajibika kwasababu nyenginezo, na mali ni sharti ya kuwajibika kwake, na mfano wake ni kulisha wazazi wawili, na jamaa wa familia, na mke, na kuondosha madhara wakati wa matatizo, ikiwa haitoshi kufanya haya mali yalioko katika hazina ya serikali ya kislamu.

- Ushuru hautoshi hata kama itakuwa kiwango sawa na Zaka, kwa maana Zaka ni ibada miongoni mwa ibada, na ushuru ni jukumu la kikanuni, wala mojawapo haitoshelezi nyengine.