JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), Mola wa viumbe vyote. Swala na salamu kwa kipenzi chetu, Nabii Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ahli zake na Masahaba zake na watu wema mpaka Siku ya Qiyaamah. Kuoga janaba katika mwezi wa Ramadhaan unaweza kufanya wakati wowote wa usiku au Alfajiri kabla ya jua la asubuhi kuchomoza ili uweze kuwahi kuswali Swalah ya Alfajiri. Ikiwa pia umelala mchana na ukaota na kupatikana na janaba ukiamka itabidi uoge ili uweze kuswali. Lakini ikiwa umepata janaba ukiwa macho ima kwa sababu ya matamanio au kupiga punyeto (tendo ni makosa hata ikiwa hukufunga) na ukatokwa na manii saumu yako inakuwa ni batili na hufai kula. Wa Allaahu A'alam
Ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:
Ghuslu - Vipi Kukoga Janabah, Nifaas Na Hedhi