Vyombo vya kuhifadhia maji na vinginevyo
Vyombo vya kuhifadhia maji na vinginevyo
Ni haramu kuvitumia kwa kauli yake Mtume ﷺ: (Msinywe kwenye vyombo vya dhahabu na fedha, na msile kwenye sahani zake. Kwani hivyo ni vyao wao ulimwenguni na ni vyetu kesho Akhera) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
Na kwa kauli yake Mtume ﷺ: (Yule anayekunywa kwenye chombo cha fedha, kwa hakika anaingiza tumboni mwake moto wa Jahanamu) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
Inafaa kuvitumia kwa matumizi mengine yasiyokuwa kula na kunywa, kama kutawadhia na mengineo kwa hadithi ilio tangulia kuwa imekaza kuvitumia kwa ajili ya kula na kunywa, na imethubu kwa hadithi ya Ummu Salamah t alikuwa na chombo (juljul) la fedha ambayo ndani yake kulikuwa na baadhi ya nywele za mtume ﷺ.
Inafaa kutumia vyombo vilivyolihimiwa kwa fedha kidogo kuwapo na haja, kwa kuwa imethubutu kwamba kopo la Mtume ﷺ lilivunjika akapafunga pale palipopasuka kwa silsila ya fedha. [Imepokewa na Bukhari].