(Usiku wa cheo)Lailatu Al-qadr

17660

 

 

Kwanini ukaitwa usiku wa cheo (usiku waheshima)?

1. Kumesemwa: Ni kwasababu ya kuutukuza, kama ilivyo kaulu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na (Mayahudi ) hawakumhishimu Mwenyezi Mungu kama inavyotakiwa kumhishimu} (Al-An-a’m – Aya 91).

Na maana yake: Ni kwamba huu usiku ni wenye hishima; kwa kuteremshwa Qur’ani ndani yake na kupatika na kushuka malaika, na ni usiku wa baraka na rehema na msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

2. Inasemekana: Al-qadr kwa maana ya kubanika kwa kuwa ndogo sana, kama kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: { na yule ambaye amepungukiwa riziki yake (riziki yake imebanika kwa kuwa ndogo sana), atoe katika kile alichopewa na Mwenyezi Mungu} ( At-twalaq – Aya 7).

Na maana ya kubanika kwa kuwa ndogo sana: Ni kule kufichika katika elimu za watu kutambua hasa usiku huo ni usiku wa tarehe ngapi.

3. Na inasemekana: Al-qadr kumaanisha makadirio, kwa maana: katika usiku huu ndiyo kunakadiriwa hukumu za mwaka ulioko; kwa kauli ya Mwenyezi Mungu U: { Katika (usiku) huu hubainishwa kila jambo la hikima} (Ad-Dukhan – Aya 4).

Fadhla za Lailatul.Qadr na Hadhi yake

1. Katika usiku huu ndio Qur’ani iliteremshwa.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika Tumeiteremsha (Qur’ani) katika Laylatu-Qadr (usiku wenye hishima kubwa)} (Al-qadr –Aya 1).

2. Usiku huu ni bora kuliko miezi elfu moja.

Mwenyezi Mungu U Amesema kuhusu usiku huu: {Huo usiku wa hishima ni bora kuliko miezi elfu }. (Al-qadr –Aya 3).

Yaani matendo ndani ya usiku huu ni bora kuliko matendo ya miezi elfu ambayo hayako katika usiku huu wa hishima.

3. Huteremka Malaika na Jibril katika Usiku huo.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Huteremka Malaika na roho katika usiku huo } [Al-qadr –Aya 4]. Na makusudio ya roho: Ni Jibril.

Kutoka kwa Abu Hureira t Anasema: Amesema Mtume (saw): (Lailatu Al-qadr ni tarehe ishirini na saba au ishirini na tisa, hakika Malaika usiku huo ni wengi sana katika ardhi kuliko idadi ya changarawe za mawe) [Fat-hul-Baary (4/255).].

4. Ni usiku wa amani.

Anasema Mwenyezi Mungu U: { Ni amani (usiku) huo mpaka mapambazuko ya alfajiri } (Al-qadr – Aya 5).

Yaani usiku wote huo ni kheri tupu, hakuna shari kutoka mwanzo wake hadi kupambazuka kwa alfajiri.

5. Ni usiku wenye baraka.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kwa yakini tumeteremsha (Qur’ani) katika usiku uliobarikiwa – bila shaka Sisi ni waonyaji} (Ad-Dukhan – Aya 3).

Ibn Abbas t Asema: ”Yaani: Usiku wa Lailatu Al-qadr”.

6- Ndani ya usiku huu ndiyo yanakadiriwa makadirio ya mwaka mzima.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Katika (usiku) huu hubainishwa kila jambo la hikima} (Ad-Dukhan – Aya 4).

7. Atakayesimama kufanya ibada katika usiku huu hali ya kuamini na kutarajia malipo atasamehewa madhambi

Amesema Mtume (saw): (Atakayesimama (kufanya ibada) usiku wa Lailatu Al-qadr kwa imani na kutarajia malipo, basi atasamehewa yote yaliyotangulia katika madhambi yake) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Ni Usiku upi wa Laylatul Qadr ?

Mwenyezi Mungu U hakuuweka wazi usiku huu ili watu wapate kujitahidi katika kumi la mwisho wa mwezi wa Ramadhani na haswaa katika siku zisizogawanyika kwa mbili (katika kumi hili) nazo ni usiku wa tarehe 21, 23, 25, 27, na 29; kwa kauli ya Mtume (saw): “Kuweni na hamu (kujitahidi ili kuipata)) usiku wa Lailatu Al-qadr katika siku zisizogawanyika kwa mbili ndani ya kumi la mwisho wa mwezi wa Ramadhani” [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Mambo yanayo pendekezwa kufanywa ndani ya Laylatul.Qadr

1. Kufanya itikafu

Nayo ni katika kumi lote wala sio usiku wa Lailatu Al-qadr peke yake, kutoka wa A’isha t anasema: “Alikuwa Mtume (saw) akifanya itikafu katika kumi la mwisho wa mwezi wa Ramadhani” [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

2. Kusimama usiku wake hali yakuamini na kutaraji malipo

Amesema Mtume (saw): (Atakayesimama usiku wa Lailatu Al-qadr hali ya kuwa na imani na kuridhia, husamehewa yote yaliyotangulia katika madhambi yake) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

3- Kuomba Dua:

Kutoka kwa A’isha Allah awe naye radhi Anasema: (Nilisema: Ewe Mtume wa Allah, ikiniafikia Lailatu Al-qadr niombe kitu gani? Akasema: Sema: Ewe Mola! Hakika yako wewe ni mwenye kusamehe (madhambi) tena Mkarimu wapenda sana kusamehe, basi nisamehe (makosa yangu)” [Imepokewa na Tirmidhi.].

4. Kuwaamsha watu wa nymbani kwa ajiliya ibaada

Amepokeya bibi A’isha t Amesema: (Alikuwa Mtume (saw) likiingia kumi la mwisho akijifunga kibwebwe na akikesha usiku wake na akiamsha wake zake) [Imepokewa na Bukhari.]

Alama za Laylatul.Qadr

1. Ni usiku ambao hauna joto wala baridi kali.

Kutoka kwa Jaabir ibn Abdillahi t Anasema: Amesema Mtume (saw): (Nilikuwa nimeoneshwa Lailatu Al-qadr, kisha nikasahaulishwa, nayo iko katika nyakati za usiku wa kumi la mwisho, nao ni usiku wenye bashasha [ Twalqat: ikiwa hakuna joto wala baridi ya kuudhi] unang’ara [ Baljah: yenyekung’ara] usio na joto wala baridi) [ Imepokewa na Ibnu Khuzeymah].

2. Jua linatokeza Asubuhi yake jeupe halina Miale.

Anasema Ubeyi ibn Ka’ab t alipoulizwa kuhusu dalili za Lailatu Al-qadr: “Kwa dalili aliyotueleza Mtume (saw) ni kwamba jua linachomoza siku hiyo halina miale”. [Imepokewa na Tirmidhi]

Na katika upokezi wa Muslim: “ Jeupe halina miale”.

Maelezo

1. Ni juu ya kila muislamu kuzidisha kufanaya ibada katika siku kumi za mwisho za mwezi wa ramadhani kwa sampuli ya ibada mbali mbali kwa sababu ni masiku bora ya mwaka.

2. Ni juu ya Muislamu asipoteze wakati wake katika masiku matukufu na msimu wa kheri kwa kufanya upuzi na mchezo na kuzurura masokoni, na kutembea sehemu zisizo kuwa nahaja.



Vitambulisho: