JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Swawm ya Nabii Daawuud (‘Alayhis Salaam) na Swalah yake. Mwanzo inatakiwa tuelewe kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amewakataza Waislamu kufunga kila siku. Swawm ya Nabii Daawuud (‘Alayhis Salaam) ilikuwa ni ya kufunga siku moja na kuacha siku moja, yaani siku baada ya siku. Na hii ndiyo aliyosema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa ndio Sunnah bora zaidi ya funga (al-Bukhaariy na Muslim). Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kuwa ‘amali iliyo bora zaidi ni ile inayodumu japokuwa ni ndogo au kidogo. Kwa hiyo badala ya kufunga Swawm ya Nabii Daawuud (‘Alayhis Salaam) funga Jumatatu na Alkhamiys au funga kila mwezi wa Kiislamu siku tatu. Na Muislamu anapofunga siku tatu kila mwezi katika tarehe 13, 14, na 15 za mwezi wa Kiislam, zijulikanazo kama ‘masiku meupe’ thawabu yake ni kama kufunga mwezi mzima. Ama kufunga siku ambazo si Jumatatu au Alkhamiys hasa Ijumaa, Jumamosi au Jumapili hazifai kuzifunga pekee, kwani Ijumaa ni siku kuu yetu, na Jumamosi na Jumamosi ni siku kuu za wasiokuwa sisi. Unaweza kufunga siku nyingine ikiwa tu imesibu kuwa ni siku ambazo zimesuniwa kufungwa kama siku ya Arafah, ‘Aashuraa, siku nyeupe, siku sita za Shawwal, na kadhalika. Unaweza kufunga Ijumaa ikiwa unaendelea na Swawm yako iliyoanzia Alkhamiys au kabla ya hapo, lakini si kuitenga Ijumaa kuifunga peke yake. Na Allaah Anajua zaidi JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Swawm ya Nabii Daawuud (‘Alayhis Salaam) na Swalah yake. Mwanzo inatakiwa tuelewe kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amewakataza Waislamu kufunga kila siku. Swawm ya Nabii Daawuud (‘Alayhis Salaam) ilikuwa ni ya kufunga siku moja na kuacha siku moja, yaani siku baada ya siku. Na hii ndiyo aliyosema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa ndio Sunnah bora zaidi ya funga (al-Bukhaariy na Muslim). Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kuwa ‘amali iliyo bora zaidi ni ile inayodumu japokuwa ni ndogo au kidogo. Kwa hiyo badala ya kufunga Swawm ya Nabii Daawuud (‘Alayhis Salaam) funga Jumatatu na Alkhamiys au funga kila mwezi wa Kiislamu siku tatu. Na Muislamu anapofunga siku tatu kila mwezi katika tarehe 13, 14, na 15 za mwezi wa Kiislam, zijulikanazo kama ‘masiku meupe’ thawabu yake ni kama kufunga mwezi mzima. Ama kufunga siku ambazo si Jumatatu au Alkhamiys hasa Ijumaa, Jumamosi au Jumapili hazifai kuzifunga pekee, kwani Ijumaa ni siku kuu yetu, na Jumamosi na Jumamosi ni siku kuu za wasiokuwa sisi. Unaweza kufunga siku nyingine ikiwa tu imesibu kuwa ni siku ambazo zimesuniwa kufungwa kama siku ya Arafah, ‘Aashuraa, siku nyeupe, siku sita za Shawwal, na kadhalika. Unaweza kufunga Ijumaa ikiwa unaendelea na Swawm yako iliyoanzia Alkhamiys au kabla ya hapo, lakini si kuitenga Ijumaa kuifunga peke yake. Na Allaah Anajua zaidi