JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Kauli za Maulaama wengi zilizowafikiana ni kwamba Swalah za Sunnah zote ikiwa na mchana au usiku zinapaswa kuswaliwa mbili mbili. Na wengineo kama Imaam Ahmad wameona kwamba ni waajib kufanya hivyo. Na hayo ni kutokana na dalili: عن ابن عمر رضي الله عنهما عن النبي صلى الله عليه وسلم قال (( صلاة الليل والنهار مثنى مثنى)) . رواه الترمذي وأبو داود والنسائي وابن ماجه . والحديث صححه الشيخ الألباني في " تمام المنَّة Kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhuma) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: “Swalaah za usiku na mchana ni mbili mbili” [At-Tirmidhiy, Abu Daawuud, An-Nasaaiy, Ibn Maajah na Shaykh Al-Albaaniy amesema Hadiyth hii ni Swahiyh katika Tamaam Al-Minnah] Ina maana kila baada ya Raka'ah mbili unatoa Salaam. Na Allaah Anajua zaidi
Ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:
Swalaah Ya Witr Inaswaliwa Vipi Na Vipi Kutia Niyyah?