Swalah ya Janeza

44468

 

Kumtayarisha Maiti

Inapendekezwa kuhudhuria pale penye mtu ambaye alama za kifo zimedhihiri kwake, na kumkumbusha kusema «Laa ilaaha illa-llah» kwa kauli yake Mtume ﷺ (Walakinini maiti zenu “Laa ilaaha illa- llaah”) [Imepokewa na Muslim.].

Akifa atafumbwa macho yake na afinikwe nguo na kufanywe haraka kumtayarisha kwa mazishi na kumswalia na kumzika.

Hukumu ya kumuosha maiti na kumtayarisha na kumzika

Kumuosha maiti, kumkafini, kumbeba, kumswalia, na kumzika ni katika faradhi inayotosheleza. Wakifanya baadhi ya waislamu inapomoka madhambi kwa waliobakia.

Hukumu ya kumuosha maiti

1. Yatakikana achaguliwe mtu mwaminifu wa kuosha maiti, pai awe mjuzi wa hukumu za kuosha.

2. Hutangulizwa kuosha yule mtu ambaye maiti mwenyewe alikuwa ameusia aoshwe na yeye. Kisha yule aliye karibu zaidi na maiti, iwapo ana ujuzi wa hukumu za kuosha. Akitokuwa hivyo, basi atatangulizwa mwenye ujuzi wa hilo.

3. Mwanamume huoshwa na wanaume, na mwanamke huoshwa na wanawake. Na kila mmoja miongoni mume na mke anafaa kumuosha mwenzake, kwa kauli ya Mtume ﷺ kumwambia›Aishah t: (Hakuna cha kukudhuru, lau wafa kabla yangu nikakuosha, nikakukafini na nikakuswalia kisha nikakuzika) [Imepokewa na Ibn Maajah.].

Pia inafaa kwa wanaume na wanawake kuwaosha watoto walio chini miaka saba. Na haifai kwa Muislamu - awe mwanamume au mwanamke- kumuosha kafiri, walakubeba jeneza yake wala kumkafini wala kumswalia, hata kama ni jama yake wa karibu kama vile baba.

4. Shahidi aliyekufa vitani haoshwi wala hakafiniwi wala haswaliwi, bali huzikwa na nguo zake.

5. Afikapo tisha- naye ni mwana aliyetoka kwenye tumbo la mamake kabla ya kutimia umbo lake, awe ni mwanamume au ni mwanamke- miezi minne, ataoshwa, akafiniwe na aswaliwe. Kwani yeye baada ya miezi minne huwa ashakuwa na umbo la binadamu kamili.

6. Maji ya kuoshea maiti ni sharti yawe ni maji yanayofaa kujitwahirishia na yawe ni ya halali, na aoshwe mahali pa sitara, na haifai kuhudhuria asiyekuwa na mafungamano yoyote na kumuosha maiti.

Namna ya kumuosha maiti

1. Maiti awekwe juu ya kitanda cha kuoshewa, kisha afinikwe uchi wake, kisha avuliwe nguo zake, afichwe na macho ya watu ndani ya chumba au mfano wake.

2. Inapendekezwa kwa muoshaji atatie kitambaa mkononi mwake wakati wa kuosha.

3. Muoshaji atakiinuwa kichwa cha maiti akaribie kumkalisha, kisha apitishe mkono wake kwenye tumbo lake na alikamue, kisha aisafishe tupu yake ya mbele na ya nyuma kwa kuosha najisi yoyote iliyopo.

4. Muoshaji atanuilia kuosha na atapiga bismillahi.

5. Muoshaji atamtawadhisha maiti kama udhu wa Swala, isipokuwa katika kusukutua na kupaliza puani, huwa inatosha kumpukusa kinywa na pua.

6. Atakiosha kichwa cha maiti na ndevu zake kwa maji ya mkunazi au sabuni au kinginecho.

7. Ataosha sehemu ya kulia kisha sehemu ya kushoto, kisha atakamilisha sehemu ya mwili iliyosalia.

8. Inapendekezwa atie kafuri katika osho la mwisho.

9. Atampangusa maiti.

10. Amuondolee maiti vitu vinavyotakikana kuviondoa kama kucha, nywele za kinena (nywele za sehemu ya siri) na makapwa.

11. Atazisuka mkili nywele za mwanamke aziweke nyuma yake

Atamuinuwa muoshaji ichwa cha maiti
Atatie muoshaji kitambaa mkononi mwake
Atawekwa maiti juu yakitanda cha kuoshewa
Muoshaji atabonyeza kwa mkono wake tumbo la maiti na kumkamua kwa upole
Muoshaji atamtawadhisha maiti kama udhu waswala
Atamuosha kichwa cha Maiti na ndevu zake kwa maji na mkunazi
Atamuosha upande wakulia kisha upande wakushoto
Atampanguswa maiti

Faida

- Lawajibu ni osho moja iwapo litatosha kumsafisha, na linalopendekezwa ni kumuosho mara matatu, hata kama ashasafishika.

- Ikitowezekana kumuosha maiti kwa kukosekana maji au ukiwa mwili umekatikakatika kwa moto au mfano wake, atatayamamishwa kwa mchanga.

- Inapendekezwa kwa mwenye kumuosha maiti aoge baada ya kumaliza kuosha.

Kumkafini maiti

1. Sunnah ni kumkafini mwanamume katika lifafa tatu nyeupe za pamba, zisizoonyesha ngozi ya mwili, yenye kusitiri mwili wake wote, wala zisiwe ni za ghali.

Na mwanamke anakafiniwa ndani ya nguo tano za pamba: nguo ya chini, msuani, kanzu na lifafa mbili.

Na mtoto wa kiume anakafiniwa kwenye nguo moja, na inafaa pia kukafiniwa kwa nguo tatu, na mtoto wa kike anakafiniwa kwenye kanzu lifafa mbili za nguo.

2. Lifafa tatu zinaletwa na zinafukizwa kwa udi, kwa kauli yake Mtume ﷺ: (Mkifukiza [ Jammara: yaani kufukiza kwa udi] maiti basi fanyeni witiri (mara tatu)) [ Imepokewa na Ibnu Hibbaan].

3. Lifafa hizi zitatengwa kila lifafa juu ya nyingine, na baina ya kila lifafa kutatiwa mafuta mazuri kama vile ambari, kafuri, miski na mfano wake. Isipokuwa akiwa maiti yuko kwenye ihramu, hapo nguo yake haitafukizwa kwa udi wala haitatiwa manukato kwa kauli ya Mtume ﷺ: (Wala msimgusishe mafuta mazuri) [Imepokewa na Bukhari.].

4. Atawekwa maiti akiwa amelala kwa mgongo juu ya hizi lifafa, kisha itavutwa ile ncha ya lifafa ya juu ya upande wa kushoto kwenye upande wake wa kulia, kisha itapelekwa ncha yake ya kulia kwenye upande wa kushoto, kisha ile ya pili, kisha ya tatu, kisha ile sehemu iliyozidi huwekwa usoni mwake, kisha hufungwa fundo kwa ufita wa kufungia ili isifunguke, na wakati wa kuzikwa hufunguliwa.

5. La wajibu ni kusitiri mwili wote. Iwapo hakuna ila nguo moja tu haitoshi kuenea mwili mzima, basi atafinikiwa kichwa chake, na katika miguu yake yatawekwa majani ya idhkhir[ Idhkhir: mmea wenye harufu nzuri.], kwa kauli ya Mtume ﷺ kumwambia Khabbaab katika kisa cha kukafiniwa Mus’ab bin ‘Umair: (Akatuamrisha Nabii ﷺ tukifinike kichwa chake na tuweke kwenye miguu yake majani ya idhkhir) [Imepokewa na Bukhari.].

6. Aliyekufa katika hali ya ihramu atakafiniwa kwenye nguo zake mbili alizohirimia, wala hafunikwi kichwa mwanamume aliyekufa katika hali ya ihramu, kwa neno lake Mtume ﷺ: (Muosheni kwa maji na mkunazi. Na mkafinini kwenye nguo mbili, na msimpake manukato [ Hanuutw: Manukato yaliyochanganywa ya kutiwa kwenye kafani za maiti.], wala msimfunike kichwa chake [ Laa tukhammiuu ra’sahu: msimfunike kichwa chake.], kwani atafufuliwa siku ya Kiyama akiwa analeta talbiah (Labbaika llaahumma labbaika..)[ Mulabbiya: analeta talbiah: (Labbaika llaahumma labbaika).]) [ Imepokewa na Bukhari.].

Kuweka manukato katika lifafa (sanda)
Atawekwa maiti kwa kulala kwatani
Kusitiri mwili mzima

Swalah ya Maiti

Nguzo za Swala ya maiti

1. Kusimama kwa anayeweza.

2. Takbiri nne..

3. Kusoma Fatiha.

4. Kumswalia Mtume ﷺ.

5. Kumuombea Maiti Dua

6. Kutugamanisha (kutaratibisha).

7. Kutoa Salamu.

Sunnah za Swalah ya Maiti

1. Kuleta A›udhu..kabla ya kusoma.

2. Kujiombea dua mwenye kuswali na kuwaombea Waislamu.

3. Kusoma kwa siri.

4. Kuzifanya safu ziwe nyingi, ziwe tatu au zaidi.

Namna ya kuswalia maiti(jeneza)

Atasimama imamu kwenye kichwa cha maiti iwapo ni mwanamume, na katikati ya maiti iwapo ni mwanamke. Na maamuma watasimama nyuma yake kama ilivyo kwenye Swala nyingine, kisha atapiga takbiri nne kama ifuatavyo:

1. Atapiga takbiri ya kwanza, nayo ni takbiri ya kufungia Swala, na ataleta Audhu.. na apige bismillahi.. na asisome dua ya kufungulia Swala, kisha asome Fatiha.

2. Atapiga takbiri ya pili, na atamswalia Mtume ﷺ kama ilivyo namna ya kumswalia Mtume katika kikao cha Atahiyatu ya mwisho.

3. Atapiga takbiri ya tatu, na atamuombea maiti. Na miongoni mwa dua ni kusema: (Ewe Mola! Mghufirie na umrehemu, umpe afya na umsamehe, ukirimu mashukizi yake na umpanulie njia yake kuingilia (Peponi), Umsafishe kwa maji, theluji na barafu, umtakase kutokana na dhambi kama inavyo takaswa nguo nyeupe na uchafu, Umbadilishie nyumba umpe nyumba ya kheri kuliko nyumba yake alokuwa nayo, na watu wa kheri zaidi kuliko watu alokuwa nao, na mke wa kheri kuliko yule alokuwa naye, Umtie peponi na umlinde na adhabu ya kaburi, au adhabu ya Moto)[ Imepokewa na Muslim.].

Na iwapo maiti ni mwanamke kutatumika dhamiri za kike (dua isomwapo kwa Kiarabu)

Na maiti akiwa ni mtoto mdogo au ni tisha [ Siqtw: mwana wa matumboni anayezaliwa kabla ya kukamilika.] atasema: (Ewe Mola! Mjaalie ni akiba ya wazazi wake na kitangulizi chema [ Faratw: aliyetanguliwa na kuwa wa mwanzo.] na ni thawabu kwao na kiombezi mwenye kukubaliwa dua) [ Imepokewa na Bukhari.].

4. Atapiga takbiri ya nne, na atanyamaza kidogo, kisha atatowa Salamu moja upande wake wa kulia au salamu mbili.

Kumbeba maiti na kumshindikiza na kumzika

Kunapomalizika kumswalia maiti, sunna ni kufanya haraka kumbeba kumpeleka kwenye kaburi lake. Na imesunniwa kwa anayefuata jeneza kushiriki kulibeba. Na imesunniwa kwa anayemuingiza maiti kaburini aseme: BISMILLAH WA’ALAA MILLATI RASULILLAH (Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na kwa mila ya Mtume wa Mwenyezi Mungu) [Imepokewa na Tirmadhi.],

na amuweke ufukoni [ Lahd: ni kufukuliwa kwenye ardhi ngumu shimo lenye urefu na kuengeza kufukuwa upande wake wa Kibla.] kwa ubavu wake wa kulia na uso wake uelekee Kibla, kisha alifunguwe fundo la kafani, kisha uzibwe mwanya wa ufuko kwa udongo.

Na ni sunna kwa aliyehudhuria mazishi ajaze mchanga vitanga vyake vya mikono na aurushe kaburini mara tatu.Kisha kaburi ifinikwe kwa mchanga, na iinuliwe juu ya ardhi kadiri ya shubiri moja, na viwekwe juu yake vijiwe na mawe, na inyunyizwe maji. Na si makosa kuweka jiwe kubwa kwenye ncha moja ya kaburi au ncha zote mbili liwe ni alama yake.

Kushiriki katika kubeba jeneza
Ufuko
Atajaza mchanga kwenye vitanga vyake vya mikono na aurushe kaburini
Alama juu ya kaburi

Kutaazii

Inapendekezwa kuwataazii waliofiliwa, kwa kuwa hilo linakunjua nafsi zao na linapunguzia msiba wao, na kuwahimiza wasubiri.

Na taazia inafaa kwa neno lolote lenye kutimiza lengo la kutaazii, kama vile kusema: (Ni cha Mwenyezi Mungu alichokichukua, na ni chake alichotoa, na kila kitu, kwa Mwenyezi Mungu, kina muda wake uliyoandikwa) [ Imepokewa na Bukhari.].

Na mfano wa maneno haya.

Wanawake kutoka kufauata jeneza
wanawake Kutoka kufuata jeneza ni jambo lisiloambatana na Sheria, kwa hadithi iliyothubutu kutoka kwa Ummu ‹Atwiyyah t kuwa alisema: (Tulikatazwa kubeba jeneza na hatukuwekewa mkazo) [Imepokewa na Ibnu Maajah].

Kuzuru makaburi

Ni sunna kuzuru makaburi kwa wanaume kwa lengo la kuwaidhika na kuwaombea wafu, kwa kuwa Mtume ﷺ alisema: (Niliwakataza kuzuru makaburi, basi sasa yazuruni, kwani hayo yanawakumbusha Akhera) [Imepokewa na Muslim.].

Miongoni mwa dua zilizokuja za kuombwa wakati wa kuyazuru makaburi ni: (Amani iwafikie nyinyi, enyi mlio kwenye nyumba ya watu Waumini! Na sisi pale atakapo Mwenyezi Mungu ni wenye kukutana nanyi) [Imepokewa na Muslim.].

Au (Amani iwashukie watu wa nyumba hizi kati ya walioamini na kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu Awarehemu waliotangulia na waliokuja nyuma. Na sisi atakapo Mwenyezi Mungu ni wenye kukukutana nanyi) [Imepokewa na Muslim.].

(Namuomba Mwenyezi Mungu Atuafu sisi na nyinyi) [Imepokewa na Muslim.].

Na lau atawaombea rehema na msamaha na mfano wake, basi hilo linafaa.

Makatazo yanayo ambatana na jeneza

1. Kuomboleza na kulia kwa makelele [ Nadb: Kutaja mema ya maiti pamoja na kulia - Niyaahah: Kumlilia maiti kwa kelele.], kuonyesha papatiko na hasira juu ya uamuzi wa Mwenyezi Mungu na kadara Yake.

Anasema Mtume ﷺ: (Mwanamke anayelia kwa makelele kwa kufiwa, iwapo hatatubia kabla hajafa, atasimamishwa siku ya Kiyama akiwa amevaa nguo ya shaba [ Qatwiraan: Kanzu ya shaba iliyoyayushwa.]) [Imepokewa na Muslim.].

2. Kupasua nguo, kujipiga makofi, kupiga kelele, kusumua nywele au kunyoa.

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu: ﷺ: (Si miongoni mwetu mwenye kujipiga makofi au akapasua nguo au akaita mwito wa kijahilia (wa kuomboleza)) [Imepokewa na Muslim.]

3. Kuwasha taa makaburini:

Ibnu ‘Abbas t amepokewa akisema: (Mtume wa mwenyezi Mungu amewalaani wanawake wenye kuzuru makaburi na watu wenye kufanya misikiti juu yake na kuwasha taa [ Suruj: taa.]) [Imepokewa na Muslim.].

Haifai kuyangarisha makaburi kwa taa wala kuyakandika

4. Kukaa juu ya makaburi au kuyakandika au kuyajengea.

Jabir t amepokewa akisema: (Alikataza Mtume wa Mwenyezi Mungu kaburi isikandikwe [ Yujasswaswu: kukandikwa.], isikaliwe na isijengewe) [Imepokewa na Muslim.].

5. Kutabaruku kwa makaburi na kuyazunguka na kuwaomba wafu.

Haya ni miongoni mwa ushirikina iwapo mtu ataitakidi kuwa hivyo vinamnufaisha au kumdhuru, kwani hakuna mwenye kunufaisha au kudhuru isipokuwa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Anasema U: {Sema: Siimilikii nafsi yangu manufaa wala madhara, ila apendavyo Mwenzi Mungu.} [7: 188]

Haifai kuyazunguka makaburi

6. Kuzika ndani ya misikiti, au kujenga misikiti juu ya makaburi au kuswali kuelekea kaburi.

Mtume wa mwenyezi Mungu ﷺ alisema: (Mwenyezi Mungu Amewalaani Mayahudi na Manaswara, waliyafanya makaburi ya manabii wao kuwa ni misikiti) [Imepokewa na Bukhari.].

Miongoni mwa hukumu za Swalah ya jeneza

1. Mwenye kukosa Swala ya maiti atamswalia kaburini kabla ya kuzikwa au baada yake, kwa hadithi iliyothubutu kwa Mtume ﷺ katika kisa cha mwanamke aliyekuwa akisafisha msikiti alipo kufa na kuzikwa Mtume ﷺ alikwenda akamswalia kaburini [ Imepokewa na Bukhari.].

2. Inapendekezwa kutayarishiwa watu waliofiliwa chakula, kwa kuwa wao wameshughulishwa na msiba na kutotayarisha chakula.

Kwa ilivyopokewa kuwa jamii ya Jaafar walipofiliwa, Mtume ﷺ akasema: (Wafanyieni jamii ya Jaafar chakula, kwa kuwa wamejiwa na jambo la kuwashughulisha) [Imepokewa na Abuu Daud.].

Kuwafanyia chakula waliofiliwa

3. Kumlilia maiti, bila kujitia hasira wala kuinua sauti wala kuomboleza, kunafaa. Mtume ﷺ Amesema alipokufa mwanawe, Ibrahim: (Kwa hakika jicho linatokwa na machozi na moyo unasikitika, na hatusemi isipokuwa linalomridhisha Mola wetu. Na sisi, ewe Ibrahim!, tuna huzuni) [Imepokewa na Bukhari.].

4. Shahidi wa vitani atazikwa na nguo zake alizouawa nazo, na haoshwi wala haswaliwi, kwa haditi iliyothubutu kwamba Mtume ﷺ aliamrisha wazikwe mashahidi wa vita vya Uhud wazikwe wakiwa na damu zao na wasioshwe [Imepokewa na Bukhari.].

Shahidi huzikwa akiwa na nguo zake

5. Akifa aliye kwenye hali ya Ihramu ya Hija au ya Umra, ataoshwa na hatatiwa manukato, wala hatafinikwa kichwa chake na ataswaliwa.

Hii ni kwa iliyothubutu kwamba Mtume ﷺ alisema kuhusu mtu aliyekufa naye yuko kwenye Ihramu ya Hija: (Muosheni kwa maji na mkunazi, na mkafinini ndani ya nguo mbili, wala msimfinike kichwa chake, kwani yeye atafufuliwa Siku ya Kiyama katika hali ya kuleta Labeka) [Imepokewa na Bukhari.].
Ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:
Swala ya Sunna