Swala ya Idd mbili

22866

 

Tamasha za idd

Idi za Waislamu ni mbili: Idi ya Fitri baada ya mwezi wa Ramadhani na Idi ya Adh›ha baada ya siku ya Arafa. Na Mwenyezi Mungu Ametupa Idi hizo ziwe ni badala ya Idi za kijahilia na kila idi yenye kuzuliwa. Anas bin Malik t amepokewa akisema: «Watu wa Jahilia (kabla ya Uislamu) walikuwa na siku mbili kila mwaka, wakisherehekea idi hizo. Mtume ﷺ alipokuja Madina alisema: (Mlikuwa na siku mbili mkizisherehekea, na Mwenyezi Mungu Amewabadilishia idi bora kuliko hizo: Idi ya Fitri na Idi ya Adh’ha) [Imepokewa na Nisaa.].

Na haifai kusherehekea wala kushiriki kwenye idi za makafiri. Kwani hizo idi ni alama zenye nguvu zaidi za kila dini na alama zilizojitokeza zaidi za sheria na njia zake. Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Anasema: {Na usifuate mapenzi yao ukaacha haki iliyokujia. Kwani kila mmoja miongoni mwenu tumemuwekea sheria na njia} [5: 48]

Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Ameweka Swala katika Idi mbili hizi inayoitwa Swala ya Idi, nayo ni tukio miongoni mwa matukio yake muhimu zaidi.

Hukumu ya Swalah ya Idi mbili

Ni faradhi ya kutosheleza ambayo wakisimama kuifanya watu wanaotosheleza, wengine wasaliao hupomokewa na dhambi ya kutoifanya- na ingawa amri ya kuifanya imetiliwa mkazo sana- Kwani Mtume ﷺ ameamrisha kuitekeleza. Bali aliamrisha kuwatoa wasichana na kina mama, hata wale walioko hedhini (aada ya mwezi) miongoni mwao ingawa hawatoswali. Hii inaonesha ubora wa Swala ya Idi na kuitilia mkazo. Na dalili ya ulazima wake ni yafuatayo:

1. Neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Mswalie Mola wako na uchinje} [108: 2].

2. Mtume ﷺ Ameamrisha iswaliwe, mpaka amewaamrisha wanawake waiswali, kwa hadithi iliyopokewa na Ummu ‘Atwiyyah t kuwa alisema: (Ametuamrisha Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ tuwatoe wanawake kwa Swala ya Idi: wadogo wanaoanza kubaleghe [’Awaatiq: ni wingi wa ‘aatiq naye ni msichana mwanzo wa kubaleghe.], waliomo hedhini [ Huyyadh (walio na hedhi): ni wingi wa haaidh (aliye na hedhi).] na wanawali walio paziani [ Dhawaat al- khduur: wanawali (Msichana bikira).]. Ama wenye hedhi watajiepusha na kuswali na watahudhuria kwenye kheri na dua ya Waislamu) [ Imepokewa na Bukhari.].

Wakati wa Swalah za idd mbili

Unaanza wakati wa Swala ya idd pale jua linapochomoza na kuangatika kadiri ya uti wa mkuki. Kuangatika huku kunakuwa ni kiasi cha robo saa kuanzia kuchomoza kwa jua mpaka kupinduka.

Na sunna ni kuichanguliza Swala ya Iddul Adh’ha ili waislamu wapate wakati wa kuchinja, na kuichelewesha swala ya iddul Fitr ili waapate nafasi ya kutoa Zaka za Fitri.

Namna ya kuswali Swala ya Idd mbili

Swalah ya Idi mbili ni rakaa mbili bila ya kuadhini wala kukimu. Na kisomo kinasomwa kwa sauti, na namna yake ni kama inayofuata:

1. Atapiga takbiri saba katika rakaa ya kwanza baada ya takbiri ya kufungia Swala na dua ya Ufunguzi na kabla ya kuleta Audhu na kusoma.

2. Ataleta Audhu na apige bismillahi na aanze kusoma Fatiha na sura baada yake. Ni sunna asome katika rakaa mbili hizo sura ya Al-A’laa katika rakaa ya kwanza na sura ya Al-Ghaashiah katika rakaa ya pili, au sura ya Qaaf katika rakaa ya kwanza na sura ya Al-Qamar katika rakaa ya pili.

3. Atapiga takbiri tano katika rakaa ya pili baada ya takbiri ya kuhama (kutoka kwenye sijida ya pili ya rakaa ya kwanza) na atainua mikono yake katika kila takbiri.

4. Atamhimidi Mwenyezi Mungu na kumsifu, na amsalie Mtume ﷺ baina ya hizo takbiri.

5. Akitoa Salamu kutoka kwenye Swala atapanda mimbari na atahutubu hutuba mbili, atakaa baina ya hutuba mbili hizo kikao kichache. Ataanza hutuba ya kwanza kwa kupiga takbiri tisa, na hutuba ya pili kwa kupiga takbiri saba.

6. Inapendekezwa katika Idd ya Fitri awakumbushe watu hukumu za Zaka za Fitri, na katika idi ya Adh, haa awakumbushe hukumu za kudhahi (kuchinja).

Mahali pa kuswali Swala ya idd

Sunna ni kusimamisha Swala ya Idd mbili katika muswallaa (uwanjani), na ikiswaliwa msikitini si makosa –iwapo kuna dharura ya kufanya hivyo.

Yanayo pendeza katika Swala ya idd

1. Mwanamume ajipambe kwa kuvaa nguo zake nzuri zaidi. Ama wanawake, watatoka kwenda kwenye kuswali bila ya kujipamba wala kujitia manukato.

2. Maamuma ahudhurie mapema na atangulie kwenye safu za mwanzo.

3. Aende kuswali kwa miguu kupitia njia na arudi kupitia njia nyingine. Jabir t amepokewa akisema: (Alikuwa Mtume ﷺ, ikiwa siku ya Idi, akibadilisha njia ) [Imepokewa na Bukhari.].

4. Ale tende idadi ya witiri (tatu au tano) kabla hajatoka kwenda kuswali Swala Idd ya Fitri, na asile chochote katika Idd ya Adh’ha mpaka arudi.

5. Inapendekezwa kuchelewesha Swala ya Idd ya Fitri ili Muislamu apate nafasi ya kutoa Zaka za Fitri na kuzifikisha kwa wanaostahiki. Ama Swala ya Idd ya Adh’ha inapenkezwa iswaliwe mapema.

Miongoni mwa hukumu za Swala ya Idd mbili

1. Ni karaha kuswali sunna kabla ya Swala ya Idd na baada yake mahali palepale, isipokuwa iwapo imetekelezwa msikitini, basi itaswaliwa swala ya kuuamkia msikiti wakati wa kuingia.

2. Ni sunna kwa aliyeikosa Swala ya Idd au sehemu ya hiyo Swala: ailipe kwa namna ile ile inavyoswaliwa, nayo ni kuiswali rakaa mbili kwa takbiri zake. Na ile sehemu ya Swala hiyo iliyompita ataitimiza kwa namna yake.

3. Mwenyezi Mungu Amewaamrisha waja wake mwisho wa Ramadhani wamtukuze. Anasema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Na ili mkamilishe idadi na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kile alichowaongoza} [2: 185].

(Tukabbiru llaha): Yaani mumtukuze kwa nyoyo zenu na ndimi zenu. Nako ni kusema” Allahu Akbar, Allah Akbar, Laa ilaaha illa-llah wa Allahu Akbar wa Lillaahil-hamd”

4. Ni sunna kuinua sauti kwa takbiri kwa wanaume. Ama wanawake watapiga takbiri kwa siri, kwa kuwa mwanamke ameamrishwa aifanye chini sauti yake.

5. Takbiri ya Idi ya Fitri inaanza tangu wakati wa kuzama jua usiku wa Idi - ikijulikana kuwa mwezi umeingia kabla ya jua kuzama-. Ama ikijulikana kuingia mwezi kabla ya jua kuzama, kama iwapo watu walikamilisha kufunga siku thelethini, au kuanzia kuthibiti kuonekana mwezi wa Mfungo mosi. Na inakoma hiyo takbiri pale watu waanzapo kuswali Idi. Ama Idi ya Adh’ha, takbiri inaanza baada ya Swala ya Alfajiri ya siku ya Arafa mpaka Swala ya Alasiri ya siku ya tatu katika siku za Tashriq.

Maelekezo

1. Ni sunna kwa waislamu kupongezana kwa Idd.

2. Ni sunna kuifurahia Idd na kuonyesha hiyo furaha, na Muislamu awapongeze jamaa zake na vipenzi vyake na ndugu zake Waislamu.

3. Idi ni fursa ambayo yapasa kuichukua katika kuunga vizazi vilivyo katika na kuwapatanisha watu walioteta.

4. Kuzuru makaburi siku ya Idi hakukuwekwa na Sheria, bali hilo ni jambo linaloenda kinyume na kile kinachotakiwa katika Idi cha kuonyesha furaha na teremo.

5. Sheria imeweka kuwakunjulia watoto katika mavazi na chakula kuwafurahisha siku ya Idi mbili kwa vitu vilivyohalalishwa na Mwenyezi Mungu. Idi mbili ni siku za furaha na buraha na teremo. Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Anasema: {Sema: Kwa nyongeza za menyezi Mungu na rehema Zake, basi kwa hilo na wafurahike. Hilo ni bora kuliko vile wanavyovikusanya}[10: 58]

6. Haifai kusherehekea kwa Masia, nay ale yanayo mkasirisha Mwenyezi mungu kwa kusikiliza miziki na kwa kuchanganyikana baina ya wanaume na wanawake, na kuacha Swala, na kupoteza wakati kwa mambo ya upuzi na yaharamu na kadhalika.