Pesa Zenye Malengo Ya Biashara Na Zilotimia Mwaka Zinapasa Kutolewa Zakaah?

Maswali: Zakaah SWALI: Asaalam Alaykum nashukuru sana kwa msaada wenu wa kutuelimisha na suali langu ni kuhusu zakaah nina hela zemetimia mwaka lakini hela hiyo sinayo mimi nimempa mtoto wa dadangu ili azifanyie bishara tuwe pamoja lakini bado hakuanza biashara na hela zimetimia mwaka je sheria inasemaje kuhusu hela hizi.

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho . Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu pesa za kibiashara ambazo zimefikia kiwango cha kutolewa Zaakaah. Ikiwa pesa zimefikiwa kiwango cha kutolewa Zakaah na imepitiwa na mwaka mzima wa Kiislamu ni lazima uitolee Zakaah mali hiyo. Na Allaah Anajua zaidi




Vitambulisho: