Nyumba Ya Kodi Inatolewa Zakaah?

SWALI: ASALAM ALAYKUM? JE IKIWA NINA NYUMBA AMBAYO NAPANGISHA NA NAPATA KODI NILAZIMA NIITOLEE ZAKA

JIBU: Shukran kwa swali lako hili kuhusu Zakah ambayo ni nguzo muhimu sana katika Uislamu. Ikiwa nyumba hiyo ni ya kukaa mtu mwenyewe basi hiyo haina Zakah. Lakini ikiwa ni nyumba ya kukodisha basi itabidi itolewe Zakah kwa mujibu wa maelezo haya chini. Kitu muhimu ni kuwa ile nyumba inapopitiwa na mwaka mmoja utabidi uitie thamani ya wakati ule lau utataka kuiuza. Ikiwa thamani ya ile nyumba ni zaidi ya gramu 82.5 za dhahabu basi utaitolea Zakah lau thamani yake itakuwa ni duni ya kima hicho kutakuwa hakuna Zakah lakini itategemea yale mapato yako ya kodi na akiba unayoweka kwayo. Ikiwa kodi ya nyumba itatosha matumizi yake au pengine haitoshi hata matumizi yake basi hatolazimika kutoa Zakah kwani Allah anasema: “Allah haikalifishi nafsi juu ya uwezo wake (kwa asichokiweza)” (2: 286). Ikiwa akiba anayoweka ni ndogo kila mwezi baada ya kutoa matumizi yake basi atahesabiwa kuwa ataanza kutoa Zakah pale hela inapofika kiwango cha chini cha yeye kutoa Zakah. Inapofika nisaab (hicho kiwango cha chini cha gramu 82.5 ya dhahabu) ataanza kuhesabu kuanzia siku hiyo mpaka inapofika mwaka na hela haijashuka chini ya nisaab itabidi atoe 2.5%. Na Allah Anajua zaidi




Vitambulisho: