Nusuk na Talbiya

7776

 

Ibada ya Hijja (nusuk)

Maana ya Ibada ya Hija (nusuk)

Nusuk Kilugha

Ibada

Nusuk kisheria

Ni maneno yanayosemwa na vitendo vinavofanywa na Mwenye kuhiji au kufanya Umra.

Nia ya ibada ya Hijja (nusuk)

Anapomaliza kuoga na kujinadhifisha yule anayetaka kuhirimia, akavaa nguo za ihramu, na mwanamume akatoa nguo za mzunguko, atanuilia kuingia kwenye ibada ya Hijja au Umra.

Na inapendekezwa aitamke aina ya ibada anayoikusudia. Aseme akikusudia Umra kisha kujistarehesha mpaka Hijja: «LABBAYKA ALLAHUMMA UMRATAN MUTAMATIAN ILAA-L HAJJI Nakuitikia, ewe Mola, kwa kufanya Umra hali ya kujipumzisha nayo mpaka nifanye ibada ya Hijja» au aseme: LABBAYKA ALLAHUMMA UMRATAN «Nakuitikia kwa kufanya Umra» kisha wakati wa Hijja aseme: LABBAYKA ALLAHUMMA HAJJA «Nakuitikia kwa kuhiji». Na mwenye kuzishikanisha pamoja Hijja na Umra»Nakuitikia kwa Hijja na Umra».

Kwa hadithi ya Anas t kuwa alisema: (Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema: ”Nakuitikia Kwa kuhiji na kufanya Umra”) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Na asipotamka chochote nia ya moyoni inamtosheleza.

Aina za ibada ya Hija

1. Tamattu›:

Nayo ni ahirimie Umra katika miezi ya Hijja mpaka amalize na ajitoe kwenye ihramu yake, kisha katika mwaka huohuo ahirimie Hija.

Na mwenye kufanya tamattu’ anapo fika makka atafanya amali ya Umra nayo: Nikutufu, na kufanya sai kati ya Swafaa na marwa, na kunyoa au kupunguza, kisha atajitoa kwenye ihramu yake na avae nguo zake, ikifika tarehe nane mwezi wa mfungotatu, atahirimia hija kisha atafanya amali za hijja na atawajibika kuchinja kwa kupumzika kwake

2. Qiraan:

Nayo ni ahirimie Hijja na Umra kwa pamoja., au ahirimie Umra kisha anuilie kufanya hija kabla ya kuanza kufanya tawafu, na mwenye kufanya Qiraan atabaki kwenye ihramu yake mpaka amalize kufanya hija, na atalazimika kuchinja kwa kule kuhirimia pamoja kwa amali ya hija na umra.

3. Ifraad:

Nayo ahirimie Hijja peke yake.na mwenye kufanya ifraadi atabaki na ihramu zake mpaka amalize kuhuji na hatolazimika kuchinja.

Na nusuk bora katika hizo tatu ni tamattu’ kwa sababu Mtume (saw) Aliwaamrisha maswahaba zake wafanye tamattu’ [ Kwa hadithi iliyopokewa na ‹Aisha t iliyoko kwenye Sahihi ya Muslim.] Kisha ni Qiraan kisha ni Ifraad

Tafauti kati ya aina tatu za ibada ya Hijja

  Kujitoa Qiraan Ifraad
Wasifu ‘Umra kisha Hijja Umra na hijja Hijja pekeyake
Ihramu Anahirimia mara mbili, ya kwanza kwa ajili ya ‘Umra kisha atahalalika baada ya hapo, kisha anahirimia kwa ajili ya Hijja Atahirim hijja na umra kwa pamoja Atahirimia hija mara moja pekeyake
Talbiya Katika kuhirimia mwanzo anasema: “Nimekuitikia ewe Mola wangu ‘Umra” anapohirimia kwa ajili ya Hijja anasema: “Nimekuitikia ewe Mola wangu Hijja” au anasema: “Nimekuitikia ewe Mola wangu ‘Umra na nitapumzika kwayo hadi Hijja” Atasema wakati wa kuhirimia (Naitikikia umra na hijja) Atasema wakati wa kuhirimia (Naitikia hijja)
Kichinjo Inapasa kuchinja Inawajibika kuchinja Hawajibiki kuchinja
Kutufu Kuna twawafu mbili, ya kwanza kwa ajili ya ‘Umra na ya pili kwa ajili ya Hijja Inalazimu twawafu moja nayo ni twawafu ya hajji Inalazimu twawafu moja nayo ni twawafu ya hajji
Sai’ Kuna sai’ mbili, ya kwanza kwa ajili ya ‘umra na ya pili kwa ajili ya Hijja Ina sai moja peke nayo ni sai ya hijja Ina sai moja peke nayo ni sai ya hijja

Kuleta Talbiya (Labeka)

Maana ya kuleta Talbiya

Kuleta Labeka

Ni Kusema Mwenye kuhirimia: LABBAYKA ALLAHUMMA LABBAYKA, LABBAYKA LAA SHARIKA LAKA LABBAYKA, INNAL-HAMDA, WANNI’MATA LAKA WALMULKA, LAA SHARIIKA LAKA (Nimekuitika ewe Mola nimekuitika! Nimekuitika Huna mshirika Nimekuitika! Sifa njema zote na neema ni zako. Huna mshirika)

Kwa Hadithi iliyopokewa na Ibnu Umar t kwamba Uletaji Labeka wa Mtume wa Menyezi Mungu(saw) ulikuwa hivyo [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Na maana ya “Labbaika Allahumma Labbaika” ni “tumekuitikia baada ya kukuitikia”.

Uletaji Labeka umekusanya kumsifu Mwenyezi Mungu na kumshukuru, kutii amri Yake, kudhihirisha kumpwekesha Yeye na kujiepusha na ushirikina.

Hukumu ya uletaji Talbiya (Labeka)

Uletaji Labeka ni sunna.

Mwanamume atainua sauti yake kwa hiyo Labeka na mwanamke ataifanya chini sauti yake, kwa kuchelea fitina

Wakati wa uletaji Talbiya na sehemu zake

Mwenye kuhirimia ataanza kuleta Labeka kwa wingi akiwa njiani baada ya kuhirimia.

Na inatiliwa mkazo katika mahali pengi miongoni mwako ni:

Akipanda sehemu zilizoinuka juu, au akateremka kwenye bonde, au akaswali Swala ya faradhi, au ukaingia usiku au mchana.

Na ataikata kuleta Labeka akiwa kwenye ibada ya Umra anapoiona Alkaba na akalipa mkono Jiwe Leusi. Na akiwa katika ibada ya Hija ataikata Labeka akianza kukirushia vijiwe kiguzo cha mwisho siku ya Idd.