Nguzo za Swala na Wajibu wake na Sunna zake

41832

 

Nguzo za Swalah

Ni sehemu zake za kimsingi ambazo Swala inatokana nazo, kwa namna isiyofaa kuziacha kwa hali yoyote ile. Hazipomoki kwa kukusudia wala kwa kusahau isipokuwa katika hali ya kutoweza.

1. Kutia nia

2. Kusimama katika swala ya faradhi pamoja na kuweza

3. Takbiri ya kufungia Swala

4. Kusoma Fatiha

5. Kurukuu

6. Kuitadili kwa kulingana sawa baada ya kurukuu

7. Kusujudu kwa viungo saba

8. Kukaa baina ya sijida mbili

9. Kukaa kwa Atahiyatu ya mwisho.

10. Kusoma Atahiyatu

11. Kumswalia Mtume ﷺ katika Atahiyatu ya mwisho.

12. Kutoa salamu

13. Kujituliza katika nguzo zote

14. Kutungamanisha baina ya nguzo

Atafanya nini mwenye kuacha nguzo moja miongoni mwa nguzo za Swalah?

1. Mwenye kuacha nguzo kwa kusudi Swala yake inabatilika na inamlazimu kuirudia.

2. Mwenye kuacha kwa kusahau, basi ni moja wa hali mbili:

a. Asikumbuke kuwa yeye ameiacha nguzo hii mpaka baada ya kuifika pale mahali pake katika rakaa iliyofuatia. Basi hapa ile rakaa iliyopita ambayo aliiacha nguzo hiyo haitahesabiwa, na ataifanya rakaa hii ndiyo badala ya rakaa aliyoisahau, kisha atasujudu sijida ya kusahau118.

- Mfano wake: Mtu alikumbuka katika rakaa ya pili katika kusoma Fatiha kuwa yeye alisahau kusoma Fatiha katika rakaa ya kwanza. Hapa ataifanya rakaa yake hii kuwa ndio rakaa yake ya kwanza na ile iliyotangulia ataipuuzwa.

b. akumbuke kuwa alisahau nguzo kwenye rakaa, kabla hajafika kwenye mahali pa nguzo hiyo katika rakaa inayofuata. Hapa itamlazimu kurudia nguzo hiyo kwa haraka pale anapokumbuka.

- Mfano wake: Mtu alisahau kurukuu kisha akasujudu alipomaliza kisomo chake, kisha akakumbuka alipokuwa hali ya kusujudu kuwa bado hajarukuu. Basi huyu itamlazimu asimame arukuu kisha akamilishe Swala yake.

Pili: Mambo ya wajibu katika swalah

Mambo ya wajibu katika swala

Ni yale yanayoungwaungwa kwa sijida ya sahau na yanapomoka kwa kuyasahau

1. Takbiri za kuhamia kutoka kwenye kitendo kwenda kwenye kingine.

2. Kusema SUBHANA RABIYAL ADHIIM “Kutakasika ni kwa Mola wangu Mkubwa”.

3. Kusema SAMI’A LLAHU LIMAN HAMIDA “Mwenyezi Mungu Amemsikia mwenye kumsifu” kwa imamu na kwa mswali pweke, ama maamuma hakuwekewa na Sheria kusema neno hilo.

4. Kusema RABBANAA LAKAL HAMDU “Mola wetu! Na sifa njema zote ni zako” katika kuitadili kutoka kwenye rukuu.

5. Kusema SUBHANA RABBIYAL A’LAA “Kutakasika ni kwa Mola wangu Aliye juu” katika sijida.

6. Kusema RABBIGH FIRLIY “Mola wangu ! nighufirie” baina ya sijida mbili.

7. Kukaa kikao cha Atahiyatu ya kwanza.

8. Kuleta Atahiyatu ya kwanza

Atafanya nini mwenye kuacha jambo la wajibu miongoni mwa wajibu wa swalah ?

1. Mwenye kuiacha kwa kukusudia Swala yake inabatilika na itamlazimu kuirudia.

2. Mwenye kuiacha kwa kusahau, basi Swala yake ni sahihi, na atasujudu sijida mbili za sahau kabla hajapiga salamu.

Tatu: Sunna za Swalah

Na kila kisichokuwa ni miongoni mwa masharti ya Swala, nguzo zake na mambo yake ya wajibu katika vile vilivyotajwa juu ya Namna ya Kuswali, basi hicho ni sunna ambao kuiacha hakuathiri katika usahihi wa Swala wala hailazimu kwa kuacha kusujudu sijida sahau.

Na sunna za Swala ni aina mbili:

Kwanza: Sunnah za maneno

1. Dua ya ufunguzi wa Swala: Nayo ni dua inayosomwa kabla ya kusoma Fatiha.

2. Kuleta Audhu: nako ni kusema A’UDHU BILLAHI MINA SHETWANI RAJIIM (Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani aliyefukuzwa kwenye rehema ya mwenyezi Mungu).

3. Kuleta bismillahi nako ni kusema BISMILLAHI RRAHMANI RRAHIM (Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu).

4. Tasbihi iliyo zaidi ya moja katika kurukuu na kusujudu.

5. Maneno ya ziada baada ya kusema RABBIGH FIRLIY (Mola wangu nighufirie) baina ya sijida mbili.

6. Kisomo cha ziada baada ya RABBANAA LAKAL HAMDU (Mola wetu! Na sifa njema zote ni zako) baada ya kuinuka kutoka kwenye rukuu.

7. Kisomo cha ziada baada ya Suratul Faatiha

Pili: Sunnah za vitendo

Nazo ni nyingi miongoni mwazo ni:

1. kuinua mikono pamoja na takbiri ya kufungia Swala, wakati wa kurukuu, kuinuka kutoka kwenye rukuu wakati wa kuinuka kwenda kwenye rakaa ya tatu.

2. Kuweka mkono wa kulia juu ya wa kushoto wakati wa kusimama kabla ya kurukuu na baada yake.

3. Kuangalia mahali pa kusujudu.

4. Kuiepusha mikono iwe kando na tumbo na mbavu wakati wa kusujudu.

5. Kukaa kikao cha iftiraash: nacho ni kukaa hali ya kuinua nyayo za mguu wa kulia na kuvielekeza vidole vyake kibla, hali ya kuweka mguu wa kushoto chini na kuukalia. Kikao hiki kimesunniwa katika vikao vyote vya Swala isipokuwa kikao cha Atahiyatu ya mwisho ya Swala ambayo rakaa zake zinapita mbili.

6. kikao cha tawarruk: nacho ni kukaa hali ya kusimamisha nyayo za mguu wa kulia na kuzielekeza vidole vyake kibla, na kuziweka nyayo za mguu wa kushoto chini ya muundi wa mguu wa kulia na kuzitoa nyayo upande wa kulia na kukalia kitako kwa kujitegemeza kalio la upande wa kushoto. Kikao hiki ni sunna kwa Attahiyatu ya mwisho ya Swala inayozidi rakaa mbili.
Ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:
Swalaah Za Sunnah Zinaswaliwa Rakaa Ngapi Ngapi?

Kiako cha iftiraash
Kikao cha tawarruk