Namna ya kuswali

126337

 

Amesema Mtume ﷺ (Swalini kama munavoniona mimi nikiswali) [ Imepokewa na Bukhari]

Aisha alipokewa kwamba alisema: (Mtume ﷺ alikuwa akifungua Swalah kwa Takbiri na kisomo cha “Alhamdu lillaahi Rabbil ‘aalamiin”, na alikuwa akirukuu hakiinamishi kichwa chake na wala hakisimamishi sawa, bali alikikiweka baina ya hali hizo mbili. Na alikuwa akiinua kichwa chake kutoka kwenye rukuu, hasujudu mpaka alingane katika kusimama. Na alikuwa akisoma Atahiyatu katika kila rakaa mbili, na alikuwa akikalia mguu wake wa kushoto na akiusimamisha mguu wake wa kulia. Na alikuwa akikataza mkao wa Shetani (kukaa kama shetani) na alikikataza mtu kuiweka chini mikono yake katika kukaa kama vile mnyama wa kuwinda, na alikuwa akihitimisha Swala yake kwa kupiga Salamu) [ Imepokewa na Muslim.].

Kuelekea Kibla na Takbiri ya kufungia Swalah

- Anayetaka kuswali atasimama hali ya kuelekea Kibla na kujihisi kuwa amesimama mbele ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, hali ya kuwa ni mnyenyekevu katika kuswali kwake.

- Kisha anuilia kuswali moyoni mwake.na nia pahali pake ni moyoni, na haifai kuitemka nia kwani kufanya hivyo ni uzushi.Amesema Mtume (Hakika amali zote ni kwa nia na kila mtu hulipwa kwa alilo nuiliya) [Imepokewa na Bukhari.na muslim. ]

- Kisha ainue mikono yake mkabala wa mabega yake au masikio yake na aseme: ALLAHU AKBAR (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa) [ Imepokewa na Muslim.].

- Kisha aweke mkono wake wa kulia juu ya wa kushoto kifuani mwake au aushike mkono wa kushoto kwa wa kulia [ Imepokewa na Ahmad.].

Dua ya kufungulia Swalah na kusoma Fatiha

- Mwenye kuswali ainamishe kichwa chake, atazame mahali pa kusujudia, kisha aseme: SUB’HANAKA ALLAHUMMA WABIHAMDIKA, TABAARAKA IS’MUKA WATA’AALA JADDUKA WALAA ILAAHA GHAY’RUKA (Kutakasika ni kwako na sifa njema ni zako. Lina baraka jina lako na uko juu utukufu wako, na hakuna mola asiyekuwa Wewe) [ Imepokewa na Muslim.].

Kisha aseme baada ya hapo: A’UDHU BILLAHI MINA SHEYTWANI RAJIIM (Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani aliyefukuzwa kutoka kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu) BIS’MILLAHI ARRAH’MAANI ARRAHIIM (Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu) kwa siri [ Imepokewa na Muslim.].

Baada ya hapo asome Fatiha [ Imepokewa na Bukhari.], kisha aseme “Aamiin”, yaani: Ewe Mola! Takabali.

. Kisha, huyo mwenye kuswali, asome Sura au baadhi ya aya za Qur’ani zilizo sahali kwake kuzisoma katika rakaa mbili za mwanzo, na asome kwa sauti katika Swala ya alfajiri na katika rakaa mbili za mwanzo za Magharibi na Isha.

Kurukuu na kuinuka kotoka kwenye rukuu

- Mwenye kuswali atainua mikono yake na alete takbiri hali ya kuinama kwende kwenye rukuu, aiweke mikono yake juu ya magoti yake, huku amekunjua vidole vyake kama kwamba anayashika magoti, asawazishe mgongo wake na kichwa chake katika hali ya kuinama kisha aseme: SUBHANA RABIYAL ADHIIM (Kutakasika ni kwa Mola wangu Aliye Mkubwa)(mara tatu ) [ Imepokewa na Tirmidhi.].

- Kisha ainuke na aseme (awe ni imamu au mwenye kuswali peke yake): SAMI’A LLAHU LIMAN HAMIDAH (Mwenyezi Mungu Anamsikia yule anayemsifu) [ Imepokewa na Tirmidhi.], na hapo wote waseme RABANA WALAKAL HAMDUH (Mola wetu! Sifa njema zote ni zako, kujaa kwa mbingu na kujaa kwa ardhi na kujaa vilivyoko baina hizo na kujaa kwa vinginvyo baada ya hizo ) [ Imepokewa na Tirmidhi.].

Na imependekezwa kuweka mikono juu ya kifua kama alivyofanya katika kusimama kabla ya kurukuu.

Kusujudu na kuinuka kutoka kwenye kusujudu

- Atatoa takbiri kisha apomoke hali ya kusujudu, na kitu cha kwanza cha kugusa ardhi kiwe ni magoti yake kisha mikono yake [ Imepokewa na Abuu Daud.] kisha paja lake la uso na pua yake, Na akunjue vitanga vyake vya mikono juu ya ardhi mkabala wa mashikio yake na mabega yake.

Na avielekeze vidole vyake upande wa kibla na ainue mikono yake [ Saa’id: ni sehemu iliyo baina ya kiwiko na kifundo.] isiguse chini na aiepushe sehemu ya juu ya mikono iwe kando na mbavu zake [‘Adhud: ni sehemu iliyo baina ya kiwiko na bega.], na pia matumbo yake [ Imepokewa na Bukhari] ayaepushe na mapaja yake, na aseme: SUBHANA RABIYAL A’ALAA (Kutakasika ni kwa Mola wangu Aliye juu kabisa) [ Imepokewa na Muslim.] (mara tatu), na akithirishe dua katika kusujudu kwake..

- Kisha atainua kichwa chake huku akileta Takbiri, na hatainua mikono yake na atakaa kwa kukalia mguu wake wa kushoto [ Imepokewa na Muslim.], na kusimamisha mguu wake wa kulia hali ya kuvielekeza vidole vyake upande wa Kibla, aiweke mikono yake juu ya mapaja yake ikiwa imekunjuliwa na vidole vyake vimeelekezwa Kibula na aseme: (Mola wangu! Nisamehe, unirehemu, uniungeunge, uniongoze na uniruzuku) [ Imepokewa na Tirmidhi.].

- Kisha atapiga takbiri na asujudu mara ya pili, kisha ainue kichwa chake hali ya kupiga takbiri na akae kikao kidogo kinachoitwa “kikao cha kujipumzisha” kwa hadithi iliyopokewa na Harith bin al-Huwairith (R.A.) katika kueleza namna ya Swala ya Mtume ﷺ kuwa yeye (alikuwa hainuki mpaka akilingana katika kukaa ) [Imepokewa na Bukhari.].

- Kisha ainuke huku akipiga Takbiri ya rakaa ya pili akijisaidia kwa mikono yake. [ Imepokewa na Bukhari.].

- Kisha ataswali rakaa ya pili kama vile ya kwanza, lakini hatasoma dua ya kufungulia Swala.

Kikao cha Atahiyatu

Amalizapo mwenye kuswali rakaa mbili za kwanza atakaa kikao cha Atahiyatu ya kwanza, akikalia mguu wake wa kushoto hali ya kusimamisha mguu wake wa kulia na kuiweka mikono yake juu ya mapaja yake, na aukunjue mkono wake wa kushoto na akikunje kidole chake kidogo[ Al-Khinswar: ni kidole cha mwisho cha mkono.

Al-Binswar: ni kidole kinachofuatia kidole cha kwanza. - Al-wustwaa: kidole kinachofuatia kidole kidoge.- Al-Sabbaabah: Ni kidole chaShahada nacho ni kile kinachofuatia kidole cha kati. - Al-ibhaam: kidole kinachofuatia kidole cha shahada.] na kile kinachokifuatia vya mkono wa kulia, na akikunje kile cha kati pamoja na gumba, na akiinue kidole cha shahada na aashirie kwa kidole chake cha shahada wakati wa kikao cha Atahiyatu, na akitazame kwa macho yake na aseme: (Kila jinsi ya maamkuzi mema ni ya Mwenyezi Mungu, na rehema na mazuri yote. Amani ikushukie wewe, ewe Nabii, na rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka Zake. Amani itushukie sisi na iwashukie waja wema wa Mwenyezi Munjgu. Ninaakiri kwamba hapana mola anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa mwenyezi Mungu, na ninakiri kwamba Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake) [Imepokewa na Bukhari.].

- Kisha atainuka huku akipiga Takbiri, iwapo Swala ni zaidi ya rakaa mbili, na ainue mikono yake apigapo Takbiri, na hatosoma katika rakaa zisaliezo isipokuwa Fatiha.

- Na atakaa kikao. cha tawarruk [ Imepokewa na Abu Daud.] katika Atahiyatu ya mwisho. Na tawarruk ni kuutoa mguu wa kushoto upande wa kulia na kuutaza na akalie matako yake, na mguu wa kulia usimamishwe. Na aseme matamko yaliyokuja kwenye Atahiyatu ya kwanza na azidishe juu yake: (Ewe Mola! Mrehemu Muhammad na jamaa za Muhammad, kama ulivyomrehemu Ibrahim na jamaa za Ibrahim, wewe ni Mwingi wa kuhimidiwa, ni Mwingi wa kusifiwa na kutukuzwa. Ewe Mola Mbarikie Muhammad na jamaa za Muhammad kama ulivyombarikia Ibrahim na jamaa za ibrahim, hakika wewe ni Mwingi wa kuhimidiwa, ni Mwingi wa kusifiwa na kutukuzwa) [ Imepokewa na Bukhari.].

- Kisha aseme: (Ewe Mola! Mimi najilinda kwako na adhabu ya Jahanamu na adhabu ya kaburi na maonjo ya uhai na umaiti na shari ya fitna za Al-Masih Al-Dajjal) [ Imepokewa na Bukhari.].

Kutoa Salamu

Mwisho wa Swala atatoa Salamu upande wake wa kulia na aseme: (Amani iwe juu yenu na rehema ya Mwenyezi Mungu) [ Imepokewa na Muslim.], na upande wa kushoto kadhalika.

Takbiri ya kufungia Swala
Kusoma suratul Fatiha
Kurukuu na kutoka kwenye Rukuu
Kusujudu na kutoka kwenye Sijida
Kukaa kitako baina ya sijida mbili
Kukaa kitako cha Atahiyatu ya Mwisho
Kutoa Salamu

Miongoni mwa dua baada ya Swala

- ASTAGHFIRU LLAH (Namuomba Mwenyezi Mungu msamaha) (mara tatu), ALLAHUMMA ANTASSALAAM WAMINKA SSALAAM TABAARAKTA YAA DHAL’JALAALI WAL’IKRAAM (Ewe Mola! Wewe ni Amani, na amani inatoka kwako, Umetukuka, ewe Mwenye utisho na utukufu) [ Imepokewa na Muslim.].

(Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu Peke Yake Asiye na mshirika. Ni Wake Yeye ufalme na Zake yeye sifa njema. Na Yeye kwa kila kitu ni muweza. Ewe Mola! Hakuna mwenye kukizuia ulichokitoa, na hakuna mwenye kukitoa ulichokizuia, na haimnufaishi bahati ya mwenye bahati kukimbia) [ Imepokewa na Bukhari.].

(Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Asiye na mshirika. Ufalme ni Wake na sifa njema ni Zake, na Yeye kwa kila jambo ni muweza. Hapana hila wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Mwenyezi Mungu. Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu. Hatumuabudu isipokuwa yeye. Neema ni Zak na wema ni Wake, na ni Zake Yeye sifa njema, hapana Mola isipokuwa Mwenyezi mungu, hali ya kuwa sisi tunamtakasia Dini, ingawa makafiri wanachukia).

(Kutakasika ni kwa Mwenyezi Mungu, na sifa njema zote ni Zake, na Mwenyezi Mungu ni Mkubwa) (mara 33) (Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Asiye na mshirika. Ufalme ni Wake na sifa njema ni Zake, na Yeye kwa kila jambo ni muweza) [ Imepokewa na Muslim.]

Ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:
NAMNA YA SWALAH YA IJUMAA

- (Ewe Mola! Nisaidie nikutaje, nikushukuru na nikuabudu vizuri) [ Imepokewa na Abu Daud.]

- Kusoma Ayatul Kursi, na sura ya Ikhlaas, na AL-Falaq na Al-Naas [ Imepokewa na Nasai.].

- Aseme: (Ewe Mola! Mimi nakuomba elimu yenye manufaa, riziki nzuri na matendo mema yenye kutakabaliwa) [ Imepokewa na Ibnu Majah.], baada ya kupiga Salamu ya Swala ya Alfajiri.    

Maelezo:
Mwanamke ni kama mwanamume, sawa sawa, katika namna ya kuswali.