Namna ya kuhiji na kufanya Umra

24266

 

Namna ya kuhiji

Mwenye kuenda hija, ima huwa ametia nia ya kufanya (Tamattu’ ) Kufanya umra kisha kupumzika mpaka wakati wa haji au ametia nia ya ( Qiraan ) nayo nikutia nia ya umra na hija pamoja, na ima awe ametia nia ya(Ifraad) hija pekeyake mwenye kutia nia yatamatt’ huwa ametoka kwenye amali ya hija na akatoka kwenye ihram, ama mwenye kufanya qiraan na ifraad watabaki kwenye ihram zao, na shughuli za Hijja zinaanza terehe nane Mfungotatu. Mpaka siku ya kumi na tatu, Na maelezo yake ni kama yafuatayo kwa masiku:

Siku ya nane ya Mfungotatu (siku ya Tarwiyah)

1. Siku ya nane ni sunna kwa mja kuhirimia hijja kabla ya adhuhuri atahirimia pale alipo, ataoga, atajitia manukato, na atavaa nguo za ihramu na atasema: LABBAYKA ALLAHUMMA LABBAYKA, LABBAYKA LAA SHARIKA LAKA LABBAYKA, INNAL-HAMDA, WANNI’MATA LAKA WALMULKA, LAA SHARIIKA LAKA (Nimekuitikia, ewe Mola, kwa Hija! Nimekuitika ewe Mola nimekuitika! usiokuwa na mshirika nimekuitika! Sifa njema zote na neema ni zako, na ufalme, Usiokuwa na mshirika) [Imepokewa na Bukhari.].

2. Ataelekea Mina, ataswali huko Adhuhuri, Alasiri, na Magharibi, Isha na Alfajiri ya siku ifuatayo. Ataswali kila Swala kwa katika wakati wake. Atazipunguza Swala za rakaa nne-nne azifanye mbilimbili. Na atasalia hapo Mina mpaka kutokea jua la siku ya tisa.

kuoga
kuhirimia
Mina
Kujipaka manukato

Siku ya tisa ya Mfungotatu (siku ya Arafa)

1. Jua linapo chomoza siku hii ya tisa mahujaji wataelekea Arafa na huku wakileta talbiya (labbayka allamuhmma labbayka), na ni Sunna kukaa (Namirah) mpaka jua lipinduke na kuingia wakati wa Adhuhuri, na wakati unapo ingia ni sunna kwa kiongozi wa kiislamu au naibu wake awahutubie mahujaji hutuba yenye kunasibiana na hali yao, awakumbushe kumpwekesha mwenyezi mungu na awafunze hukumu za hijja na mambo muhimu kuhusu dini yao.

2. Kisha atawaswalisha adhuhuri na alasiri kwa kuzikusanya, kutanguliza na kuzipunguza, na huruhusiwa mahujaji kwa siku hii aelekee kibla, na azidishe kumuomba mungu na ajitahidi sana katika kuomba, na adhihirishe unyonge wake na udhaifu wake na kumuhitajia kwake mwnezi mungu U na akariri maombi Amesema Mtume (saw) (Dua bora ni dua ya siku ya Arafa, na maneno bora niyale niliyo yasema mimi na manabii kabla yangu hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi mungu pekeyake hana mshirika ufalme ni wake, na kusifiwa ni kwake yeye, na yeye ni muweza wakila kitu) [Imepokewa na Tirmidhi]

na afanye pupa kuomba dua zilizopokelewa kwa Mtume (saw) na ajiepushe na dua ya kujikalifisha, na asome Qur’ani kadiri anavo weza, na akithirishe kumswalia Mtume (saw).

3. Kisha wataondoka mahujaji kutoka arafa wakielekeya Muzdalifa baada jua kuzama na haifai kuondoka kabla ya kuzama kwa jua, na akiondoka kabla kuzama kwa jua itamlazimu arudi hata kama ni usiku na asiporudi itamlazimu yeye damu kuchinja nayo ni kuchinja mbuzi au fungu la saba la ngamia ama fungu lasaba la ngombe

Muzdalifa
Namirah
Arafa
Maelekezo

1. Inahisabika kuwa mtu amesimama arafa kwa kuweko mwenye kuhiji uwanja wa arafa siku ya tisa, sawa akiwa amesimama ama amekaa ama amelala ama amepanda, na silazima kuwa amesimama.

2. Kusimama arafa ni nguzo miongoni mwa nguzo za hijja na haisihi hija ya mtu ikiwa hakusimama Arafa, na mwenye kukosa kusiamam arafa huwa ameikosa hija kwa neno lake Mtume (saw) (Hija ni Arafa) [Imepokewa na Ahmad]

3. Unaanza wakati wa kisimamo cha Arafa kuanzia kutoka kwa alfajiri siku ya tisa mpaka alfajiri ya siku ya kumi, mwenye kusiama Arafa katika wakati huu japo kidogo hali yakuwa ni mtu afaaye kusimama hija yake itasihi, na mwenye kukosa kusimama wakati huu hija yake haikusihi Amepokea Ibnu Abbas kutoka kwa Mtume (saw) Amesema (Mwenye kuipata arafa kabla ya Alfajiri basi ameipata hija) [Amesahihsha Al’albaniy katika swahihil-jaami’ No(5995)]

4. Arafa yote ni uwanja wa kisimamo, na Mtume (saw) alisimama kwenye jabali karibu na swakharaat hali yakueleka kibla na wala hakupanda juu ya jabali Amesema (Nimesimama hapa na Arafa yote ni sehemu ya kisimamo) [Imepokewa na Muslim], ikiwa ataweza kusimama alipo simama Mtume ni uzuri na asipo weza atasimama sehemu yoyote, wala haifai kusimama kwenye jangwa wala kupanda jabali,

5. Ni juu ya mwenye kuenda hijja akumbuke kuwa siku ya arafa ni siku kubwa na ina fadhla kubwa, na mwenyezi mungu anawakirimu waja wake, na ajifakhiri mbele ya malaika wake, na nisiku ambao watu huacha huru na moto.Amesema Mtume (saw) ( Hakuna siku ambao Mwenyezi Mungu huacha waja wake huru na moto kuliko siku ya Arafa, na siku hiyo Mwenyezi Mungu anakurubia kisha anajifakhirisha na waja wake, na anasema: wataka nini wajawangu?) [Imepokewa na Muslim], yatakikana kwa hajji kufaidika na masaa ya siku hii tukufu, na kujadidisha Tawba na kujihisabu nafsi yake wala asipoteze wakati wake kwa kuzunguka ovyo na kuzungumza upuzi na kufanya mijadala.

Usiku wa wa siku yakumi kuondoka kuelekea Muzdalifa na kulala hapo

1. Mahujaji wataondoka kutoka Arafa kuelekea muzdalifa baada ya jua kutwa, na nisunna kwa mahujaji kuondoka kwa utulivu na upole bila ya kuwaudhi watu, na aondoke hali ya kuleta talbiya na kumtaja mwenyezi mungu U.

2. Atakapofika muzdalifa atanza na swala ataswali Maghrib na ishaa kwa kuzikusanya na kupunguza swala ya isha, kabla kuteremsha mizigo na vitu vyake.

3. Nilazima kulala Muzdalifa usiku wake na ataswali alfajiri mapema, na haifai kuondoka muzdalifa kabla ya alfajiri ila kwa wenye udhuru, kama watu madhaifu katika wanawake, na watoto na kwa wale wanaofuatana nawao, ambao wanawatumikia wao yafaa kuodoka nawao mwisho wa usiku mwezi unapo zama.

4. Anapo maliza kuswali alfajiri inapendekezwa kwa mahujaji aende kwenye Mash’aril haram, na aeleke kibla na azidishe dhikri na dua hali yakuwa ameinuwa mikono yake na ataendelea kufanya hivyo mpaka kupambazuke sana, na sehemu yoyote atakapo simama muzdalifa yafaa, kwa neno lake Mtume (saw) (Nimesimama hapa na jam’u yote ni mahali pakisimamo) [Imepokewa na Muslim] na makusuduio ya Jam’u ni Muzdalifa.

5. Anapoondoka haaji kutoka muzdalifa inapendekezwa aokote vijiwe saba pekeyake kwa ajili yakutupa kwenye jamaraat, ama masiku yalio baki ataokota vijiwe mina au sehemu yoyote atakapo okota yafaa

Siku ya kumi ya Mfungotatu (Siku ya Idd)

1. Ataswali Alfajiri, kisha atajishughulisha na kumtaja Mwenyezi Mungu na kuomba dua mpaka kabla ya jua kuchomoza kwa muda mchache.

2. Ataondoka kutoka Muzdalifa kuelekea Mina kabla ya jua kuchomoza.na atazidisha njiani kuleta talbiya na afikapo wango wa muhassira atafanya haraka, nao ni wangwa kabla ya mina baina yake na Muzdalifa

3. Afikapo Mina ataenda kwenye Kiguzo cha mwisho upande wa mina, na cha kwanza kutoka upande wa makka atakapo fika hapo ataacha kuleta talbiya (labayka) na akirushie vijiwe saba kwa mfululizo, kimoja baada ya kingine, akipiga takbiri katika kila kijiwe anachokirusha. Na unaanza wakati unaopendekezwa kurusha vijiwe kuanzia wakati wa alfajiri ya siku ya iddi, na ikiwa atarusha kabla ya alfajiri mwisho wa usiku itasihi na itamtosheleza, na unaendelea wakati wa kutupa mpaka alfajiri siku ya kumi na moja

Maelekezo

- Muislamu ajiepushe na kuwaudhi ndugu zake Mahujaji wakati wa kutupa vijiwe jamaraat, nawakati wakufanya ibada nyinginezo za hija.

- Ahakikishe kuwa kijiwa kimeingie kwenye ndani ya birika, baadhi ya watu wanakosea wakidhani kuwa unapo rusha kijiwe ni kulenga kiguzo na kijiwe kisingie kwenye birika, na baadhi hutupa kijiwa akiwa mbali na birika na kijiwe kisingie kwenye birika basi mwenye kutupa namna hiyo huwa hakutekeleza wajibu wa kutupa.

- Na ni juu ya muislamu asivuke mipaka katika kurusha vijiwe asitupe jiwe kubwa au kurusha viatu, sunna ni kijiwe kiwe kikubwa kidogo kuliko dengu kwa Hadithi ya Jaabir bin Abdillah t Nakasema (Nimemuona Mtume (saw) Akilitupia jamara kwa kijiwe kidogo mfano wa koko ya tende) [ Imepokewa na Muslim. Na vjiwe vyakutupa ni vidogo atavishika kwa vidole viwili na kutupa].

- Na akitupa vijiwe vyote kwa mara moja hahisabiwi ila kijiwe kimoja, na lau ataviweka kwenye kitu avirushe vyote kwa pamoja haitasihi bali ni lazima kupatikane kurusha.

4. Atanyoa kichwa chake chote au atapunguza, na kunyoa ni bora, na Mwanamke atapunguza nywele zake kadri ya ncha za kidole,

5. Atateremka Makka atufu twaafu ya Ifaadhah, nayo ni twawafu ya Hija, na katika twawafu hii hakuna kufanya Raml kutembea haraka wala kufunguwa bega na baada ya kutufu ataswali rakaa mbili, na ubora katika twawafu hii avue nguo za ihraam na avae nguo zake zakawaida na ajipake manukato kwa kauli ya bibi Aisha t Nilikuwa nikimpa Mtume (saw) manukato kwa ajili ya kuhirimia kwake wakati wakuhirimia na wakati wakujitoa kwenye ihrama kabla ya kufanya twawafu. [Imepokewa na Bukhari na Muslim. ]

6. unaanza wakati wakufanya twawafu baada ya alfajiri ya siku iddi, na itamtosheleza kabla ya Alfajiri mwisho wa usiku aliyeondoka Muzdalifa mapema kwa sababu ya udhuru kama watu wazima, na yafaa kuchelewesha kufanya twawafu siku ya iddi lakini si bora kufanya hivyo.

7. Na baada ya kufanya Twawafu ya Ifaadhwa, atafanya sai kwa Mutamatti’ ama alie tia nia ya Qiraan na Ifraad kama walifanya sai katika twawafu ya Quduum hawatafanya sa’i baada ya twawafu ya ifaadhwa, na haji akimaliza kufanya twawafu ya ifaadha na akafanya sa’i kwa atakae kuwa na sai huwa ashakamilisha matendo ya siku ya Idd, na itamlazimu arudi mina akalale usiku wa kumi namoja

Kutupa vijiwe kwenye jamarul-Akaba.
kuchinja Mnyama wa tunu
Kunyoa na Kupunguza
Kufanaya Twawafu
Kufanya sai baina ya swafaa na marwa
Kulala Mina

Mpangilio wa Matendo katika Siku ya Iddi

Sunna katika mipangilio ya siku ya idd ni kama inavo fuata: Kutupa vijiwe, kisha kuchinja, kisha kunyoa au kupunguza, kisha kufanya Twawafu, kisha kufanya sai kwa mwenye sai, na lau atatanguliza moja katika mambo haya juu ya jengine yafaa na hakuna ubaya wowote, kwa sababu mtume (saw) Aliruhusu hilo, lau mtu atanyoa kwanza kisha akatupa mawe itasihi, na lau atachinja kwanza kisha akafanya Twawafu kisha akatupa vijiwe ni sawa, kwa sababu hakulizwa mtume kwa mwenye kutanguliza jambo na kuakhirisha jengine ila akisema (Fanya na hakuna ubaya) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Kuhalalishiwa Mara ya Kwanza na Kuhalalishiwa Mara ya Pili:-

- Kuhalalishiwa ya kwanza: Ni kuhalalishiwa yote yale yalokuwa ni haramu kufanya kwa mwenye kuwa katika ihram isipokuwa kufanya tendo la ndoa au kufunga ndoa itakuwa si halali kwake kufanya hivyo, na inapatikana mtu kuhalalishiwa kwa kufanya mawili katika yanao fuata: kutupa vijiwe kwenye jamaraat, kunyoa au kupunguza, kufanya Twawafu pamoja nakufanya sai kwa atake kuwa na sai

- Kuhalalishiwa mara ya pili: ni kuhalalishiwa kufanya yote yale yaliokuwa ameharamishiwa kufanya alipokuwa kwenye ihram, na hupatikana uhalali wapili kwa kufanya yale yalio tangulia yote pamoja.

- Kuchinja haina mafungamano na kuhalalishiwa, lau atachelewesha kuchinja mpaka siku ya pili siku ya kumi na moja, na akafanya yale mengine siku ya idd atakuwa amehalalishwa.

Masiku ya Tashriiq

Ni siku tatu, siku ya kumi na moja na siku ya kumi nambili na siku ya kumi na tatu katika Mwezi wa Mfungotatu zimeitwa kwa jina hilo kwa sababu nyama za Udh’hiya zikikatwakatwa na kuanikwa juani ili zikauke na Mtume Alisema kuhusu masiku haya (Jueni ya kuwa masiku haya ni masiku ya kula nakunywa na kumtaja Mwenyezi Mungu) [Imepokewa na Abuu Daud]

Siku ya Kumi na Moja na Usiku wake

Nilazima kwa mahujaji kulala mina usiku wa siku ya kumi namoja na siku yakumi na moja baada ya kupinduka juwa wataenda kutupa vijiwe katika jamarati zote kwa kila jamara atatupa vijiwe saba

- Namna ya kutupa Vijiwe

Atanza kwenye Jamarati ya Kwanza: atavirushia vijiwe saba kwa kufuatana, na atapiga takbiri (Allahu Akbar) kwa kila kijiwe, na nilazima ahakikishe kuwa kijiwe kimeingia kwenye lile birika, kisha atasongea mbele kidogo asimame amuombe Mwenyezi Mungu hali ya kuinuwa mikono yake juu.

-Kisha atarusha kwenye jamara ya katikati atatupa vijiwe saba kama alivyo fanaya kwenye jamara ya kwanza kisha atasimama amuombe Mwenyezi Mungu hali yakuinuwa mikono yake.

-kisha atarusha kwanye jamara ya mwisho atatupa vijiwe saba wala hataomba dua

Kiguzo kidogo
Kiguzo cha Mwisho
Kiguzo cha katinakati

Siku ya Kumi na mbili na Usiku wake

Nilazima kualala minaa usiku wa siku ya kumi na mbili, na mchana wake jua litakapo pinduka atatupa vijiwe kwenye jamarati zote kama alivyo fanya siku ya kumi na moja.

Ikiwa atataka kufanya haraka kuondoka siku hii, basi akisha maliza kutupa ataondoka mina kabla ya kutwa jua, ikiwa jua litazama nayeye yuko minaa basi itamlazimu kulala mina na kulazimaka kutupa vijiwe siku ya kumi na tatu, nao nikuzidisha kheri kama alivyo sema Mwenyezi Mungu U {Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika zile siku zinazo hisabiwa.Lakini mwenye kufanya haraka katika siku mbili (akaregea) si dhambi juu yake na mwenye kukawia pia si dhambi juu yake, kwa mwenye kumcha mungu} [Al-Baqara: 203]

Na makusudio kwa mwenye kufanya haraka siku mbili katika masiku ya tashriiq ni siku ya kumi na moja na siku ya kumi na mbili na mwenye kuchelewa na akatimiza siku ya kumi natatu.

Siku ya kumi na tatu na usiku wake

Na baada ya kupinduka jua siku ya kumi na tatu atatupa vijiwe kwenye jamarati zote kwa namna alivyo fanya katiku siku mbili zilizo pita, na unamalizika wakati wa kutupa baada ya kutwa jua siku hii

Kuchelewesha Kurusha

Lau mwenye kufanya hijja ataakhirisha kutupa vijiwe mpaka siku ya pili yake yafaa kwa sababu masiku ya tashriiq yote ni masiku ya kutupa.

Namna yakutupa kwa alie akhirisha kutupa

Ni aanze kutupa siku ya kwanza katika jamrati zote, kisha arudi atupe tena akianza jamaraat ya kwanza mpaka amalize zote, na harushi isipokuwa baada ya kupinduka jua

Twawafu ya kuaga

Anae fanya haji akitaka kutoka makka atafanya twawaafu ya kuaga, nayo ni wajibu miongoni mwa wajibu za hija, na hafanyi sai na hupomoka twawafu ya kuaga kwa mwanamke menye hedhi na nifasi

Kuichelewasha Twawafu ya Ifaadha mpaka kwenye Twawafu ya Kuaga

Lau mwenye kufanya hija ataichelewesha Twawafu ya Ifaadha mpaka kwenye Twawafu ya kuaga yafaa kufanya hivyo lakini si bora kufanya hivyo, na itamtosheleza twawafu ya ifaadha kwa sharti atie nia ya ifaadha itamtosheleza na twawafu ya kuaga hata kama atafanya sai baada yake.

Namna ya Kufanya Umrah

1. Atakayefanya Umra afikapo mahali pa kuhirimia, ataoga, atajitia manukato, atavaa mavazi ya kuhirimia na atanuilia Umra hali ya kusema: (Tunakuitikia kwa ibada ya Umra).

Kuoga
Manukato
Mavazi ya ihramu

2. Katike kuleta Labeka, Sheria imeweka aseme: (Tumekuitikia, ewe Mola, tumekuitikia! Huna mshirika tumekuitikia! Sifa njema na neema ni zako na ufalme! Huna mshirika!) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Na ataendelea kuleta Labeka mpaka aione Alkaba na alisalimie Jiwe Leusi.

3. Atakwenda aingie Msikiti wa Haram, aanze kwa mguu wake wa kulia na aombe dua ya kuingia msikitini.

4. Anaikata Labeka na aanze kutufu Alkaba, kuanzia kwenye Jiwe Leusi, alishike na alibusu – ikiwezekana- ikiwa haikuwezekana ataliashiria kwa mkono wake na atasema: (Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mkuu. Ewe Mola! Ninatufu Kwa kukuamini Wewe na kukiamini Kitabu Chako, na kwa kutekeleza ahadi Yako na kwa kufuata mwendo wa Nabii Wako Muhammad ﷺ).

5. Atafanya twawafu mara saba huku Alkaba ikiwa upande wake wa kushoto, akianzia kwenye Jiwe Leusi na kumalizia hapo.

6. Imesunniwa kwa mwanamume atembee kwa haraka katika mizunguko mitatu ya mwanzo.na afunguwe bega lake la mkono wa kulia

Masharti ya kutufu
Inashurutiswa kwa mwenye kufanya Twawafu: kutia nia na kujitoharisha na kusitiri tupu, na azunguke mara saba, na aanze kwenye jiwe leusi, na aijaliye Alkaba upande wake wa kushoto na afuatanishe bena ya mzunguko ila inapo kimiwa swala au ikiswaliwa janaza ataswali kisha ataendelea pale alipokoma kwenye twawafu yake, na aizunguke alkaba yote lau ataingia kwenye hijri haitosihi twawafu yake kwa sababu hijri ni katika Alkaba.

7. Ataomba atakalo katika kutufu. Na akikaribia Nguzo ya Upande wa Yamani aishike kwa mkono na apige takbiri. Akitoweza atoiashiria na hatopiga takbiri. Na akiwa baina ya Nguzo ya Upande wa Yamani na Jiwe Leusi aseme: (Mola wetu! Tupe jema la ulimwenguni na jema la Akhera na utuepushe na adhabu ya Moto) [Imepokewa na Abuu Daud]

8. Baada ya kutufu Alkaaba ataswali rakaa mbili nyuma ya Makaam Ibrahim - ikiwezekana kama haikuwezekana ataswali sehemu yoyote msikitini

Maelekezo

1. Ni juu ya muislamu kutoingia kwenye zahma pamoja na wenye kutufu ili asijitie kwenye tabu yeye na kuwatia wenzake, katika kutaka kulisalimia jiwe jeusi ama kulibusu, na vilevile hata fanya raml kufanya haraka katika kuzunguka alkaba ikiwa atawaudhi wenye kufanya twafu.

2. ataomba kwenye twawafu kwa atakavo weza, na twawafu haina dua maluum isipokuwa yale yalio tanguliya, na lau atasoma qur’ani katika twawafu yake hakuna ubaya wowote kufanya hivyo.

3. kufanya idhtibaa (kufungua bega) ni sunna katika Twawafu ya umra au twawafu ya quduum katika mizungu yote.

4. Na mwanamke ajiepushe kudhihirisha mapambo katika twawafu yake na kujipaka manukato, na kuinuwa sauti katika kuleta dhikri na dua

9. Atatoka kuelekea Jabali la Swafaa, akilikaribia atasoma neno la Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Hakika Swafaa na Marwah ni miongoni mwa sehemu za ibada ya Hija, basi anayehiji au kufanya Umra, si makosa kwake kusai baina hayo mawili. Na mwenye kujitolea kufanya mambo ya kheri, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushukuru, ni Mwingi wa ujuzi} [2: 158].

10. Atapanda juu ya Swafaa na ataelekea Kibla, atainua mikono yake na atamtukuza Mwenyezi Mungu na kumsifu na atasema: (Hapana mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Peke Yake, Asiye na mshirika. Ni Wake Yeye ufalme na ni Zake Yeye sifa njema. Na Yeye kwa kila kitu ni Muweza Tunarudi makwetu, tunatubia kwa Mola wetu, tunamuabudu, tunamsujudia na tunamsifu. Mwenyezi Mungu Ametimiza ahadi Yake, Amemnusuru mja Wake na Ameyashinda mapote Peke Yake) [Imepokewa na Bukhari.]

Kisha ataomba baada ya hapo, kisha airudie hiyo dhikiri mara ya pili, kisha aombe, kisha airudie dhikiri mara ya tatu.

11. Atashuka Swafaa akielekea Marwah, aharakishe mwendo wake anapokuwa baina ya alama mbili za rangi ya kijani [ Nazo ni alama mbili za mahali alipopakimbia Bibi Hajra kwa kusai baina ya Swafaa baina na Marwah], apande Marwah na atafanya namna hiyo akiwa Swafaa.

12. Atasai baina ya Swafaa na Marwah mara saba.

13. Baada ya kusai, mwanamume atapunguza nywele zake za kichwa kwa namna ya kuonekana wazi kuwa zimepunguzwa. Na mwanamke atapunguza kwenye pambizo zote za nywele za kichwa chake kadiri ya ncha ya kidole.

Na lililo bora kwa mwanamume ni kunyoa, kwa hadithi iliyothibiti kutoka kwa Abu Huraira t kwamba alisema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) Alisema: (Ewe Mola! Warehemu walionyoa. Wakasema: ” na waliopunguza pia?” Akasema: “Ewe Mola! Warehemu walionyoa.” Wakasema: “Na waliopunguza pia?” Akalikariri hilo mara tatu, kisha akasema “na waliopunguza pia”) [Imepokewa na Bukhari.].

14. Atajitoa kwenye ihramu yake.

Na kwa hivyo atakuwa amemaliza Umra yake.

Kufanya sai kati ya Swafaa na Marwa