JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani kwa swali lako kuhusu kusumbuliwa kwako na ute unaokutoka kwa miaka mingi sasa. Hakika ni kuwa unyevunyevu ambao unawatoka wanawake ni kitu cha kawaida kabisa. Kwa hiyo kutokwa na huo ute hakuna tatizo kabisa isipokuwa ikiwa kinachotoka ni manii au madhii. Ikiwa ni kama ulivyouliza, basi kutakuwa hakuna haja kishari’ah kujitwahirisha kama mtu mwenye janaba. Hivyo jambo kama hilo lisikutie wasiwasi na kukosesha raha. Ukifika wakati wa Swalaah unaweza kujiosha sehemu hizo na kisha ukachukua Wudhuu wako lakini hilo si lazima ila ni bora kufanya hivyo kwa usafi wako na kuchunga usafi wa unayemsimamia mbele yako wakati wa Swalaah zako. Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate manufaa zaidi: Tofauti Baina Ya Manii Na Madhii Na Hukumu Zake Za Ghuslu Hukmu Ya Wadii Na Madhii Mwanamke Akitokwa Na Majimaji, Je, Aoge Janaba? Ni Lazima Kujisafisha Sehemu Za Siri Unapotaka Kufanya Wudhuu? Na Allaah Anajua zaidi