Masharti ya kufanya Swala iwe sahihi

26271

 

 

Kwanza: kuingia wakati

Swala ya faradhi ina wakati ambao haiswihi kabla yake, wala baada yake isipokuwa kwa dharura. Asema Mwenyezi Mungu aliyetukuka: { Hakika Swala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalum} [4: 103],

yaani imefaradhiwa katika vipindi maalumu.

Nyakati za Swala ni: .

1. Wakati wa Alfajiri:

Ni kuanzia kutoka alfajiri ya kweli, nao ni ule weupe unaokuwa kwenye pambizo upande wa Mashariki, mpaka kuchomoza jua.

2. Wakati wa Adhuhuri:

Ni kuanzia kupinduka jua mpaka kivuli cha kitu kiwe mfano wake, baada ya kile kivuli cha kupinduka jua. Hivyo ni kwamba jua likichomoza kitu kinachosimama huwa na kivuli upande wa magharibi, kisha kivuli hiko huenda kikipungua kila jua likipanda mpaka kivuli kisimame. Kisha kivuli kinaanza kuongezeka, na ongezeko hili lianzapo hua ndio wakati wa kupinduka.

3. Wakati wa Alasiri:

Ni kuanzia wakati wa Adhuhuri kuisha mpaka kivuli cha kitu kiwe ni mara mbili yake baada ya kivuli cha kupinduka jua.

4. Wakati wa Magharibi:

Ni kuanzia jua linapozama mpaka yapotee mawingu mekundu, nayo ni ule mwangaza mwekundu unaokuwa kwenye pembe za mbingu pale jua linapozama.

5. Wakati wa Isha:

Ni kuanzia kipindi cha Magharibi mpaka nusu ya usiku, kwa neno lake ﷺ: (Wakati wa Swala ya Isha ni mpaka usiku wa kati) [ Imepokewa na Muslim.].

Na katika zama hizi, inawezekana kujua nyakati za Swala kwa urahisi kwa njia ya kuweka jaduali za kujulisha nyakati.

Swala ya Alfajiri
Swala ya Adhuhuri
Swala ya Alasiri
Swala ya Magharibi
Swala ya Isha
Yasiofaa

- Kuswali na nguo ya kubana yenye kusifu uchi wa mtu, au nguo nyembamba yenye kuonyesha, au kuswali na huku akiwa tupu yake inaonekana, au na isbaal nao ni mtu kuswali na nguo yake imevuka vi fundoni.

- Kuswali na nguo yenye picha, au kuswali sehemu zilowekwa picha za roho, au kuswalia mswala wenye picha na michoro.

- Kuswali katika Msikiti wenye Makaburi, kwa neno lake Mtume ﷺ (Jueni kuwa watu walio kuwa kabla yenu wakiyafanya makaburi ya manabii wao na watuwema wao misikiti, basi musiyafanye makaburi yeni misikiti mimi nawakataza hilo) [ Imepokewa na Muslim.]

Faida

1. Mwenye kuwahi rakaa moja kabla ya kutoka wakati huwa amewahi Swala, kwa kauli yake Mtume ﷺ: (Mwenye kuwahi rakaa moja ya Swala huwa amewahi Swala) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

2. Ni lazima kutekeleza Swala kwa haraka iwapo wakati wake umepita kwa kulala au kwa kusahau, kwa neno lake Mtume ﷺ: (Mwenye kuisahau Swala basi ni juu yake aiswali anapoikumbuka, hakuna kafara yake isipokuwa hiyo) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Pili: Kutwahirika na hadathi

1. Kutwahirika na hadathi ndogo (tukio la kutokuwa na udhu):

Nako kunapatikana kwa kutawadha. Mtume ﷺ anasema: (Mwenyezi Mungu hatakubali Swala ya mmoja wenu akitokewa na tukio la kutokuwa na udhu mpaka atawadhe) [ Imepokewa na Bukhari].

2. Kutwahirika na hadathi kubwa:

nako kunapatikana kwa kuoga, kwa neno la mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Na mkiwa na janaba jitwahirisheni} [5: 6].

Na yoyote atakayekumbuka akiwa katika Swala kuwa hana udhu au ametokewa na jambo la kuharibu udhu katikati ya Swala, basi Swala yake itatanguka Na itamlazimu ajitoe Swalani ili ajitwahirishe na bila ya kutoa Salamu, kwa kuwa swala ishatanguka na bado haijamalizika, na utoaji salamu ndio mwisho wa Swala.

Tatu: Utwahara wa Nguo, mwili na mahali

1. Utwahara wa nguo,

kwa neno lake Mwenyezoi Mungu aliyetukuka: {Na nguo zako twahirisha} [74: 4].

Utwahara wa nguo

2. Utwahara wa mwili,

kwa ilivyothubutu kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ aliipita kwenye kaburi mbili akasema: (Hakika wawili hawa wanaadhibiwa. Na hawaadhibiwi kwa jambo kubwa. Ama huyu alikuwahajiepushi [ Laa yastanzihu min al-baul: hajiepushi na hajikingi na mkojo.] na mkojo usimuingie) [ Imepokewa na Abu Daud.].

3. Utwahara wa mahali,

kwa hadithi ya mbedui aliyekojoa msikitini. Mtume ﷺ alisema: (Muacheni na umwagieni [ Hariiquu: mwageni.] mkojo wake ndoo [ Dhanuub: ndoo kubwa iliyojaa maji.] ya maji) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Utwahara wa Mahali pa kuswali

Swala na Najisi

Mwenye kuswali naye ana najisi bila ya kuijua au akaisahau, basi Swala yake ni sahihi. Kwa kuwa ilithubutu kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ aliswali akavua viatu vyake, na watu wakavua viatu vyao. Alipoondoka alisema ﷺ: (kwa nini mlivua viatu vyenu? Wakasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tulikuona ukivua viatu vyako na sisi tukavua”. Mtume akasema: “Jibrili alinijia akanipasha habari kwamba viatu vina uchafu. Basi anapokuja mmoja wenu msikitini, avigeuze viatu vyake avitazame. Akiona kuwa vina uchafu, basi na avisugue chini kisha aswali navyo) [ Imepokewa na Abu Daud.].

Yoyote atakayejua kuwa ana najisi akiwa katikati ya Swala, itamlazimu kuiondoa, kisha aendelee na Swala yake na ajengee juu ya kile alichokiswali, kwa hadithi iliyotangulia. Akitoweza kuiondoa, swala yake itatanguka.

Ardhi yote ni Msikiti

Ardhi yote ni msikiti, kwa kuwa kuswali hapo inafaa. Mtume ﷺ amesema: (Nimefanyiwa ardhi kuwa ni mahali pa kuswali na mahali pakujitwahirishia. Basi mtu yoyote miongoni mwa umma wangu aliyeingiliwa na kipindi cha Swala na aswali) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Kinachovuliwa hapo ni kuswali kwenye sehemu zilizokatazwa, kama vile kuswali makaburini (Kinachovuliwa hapo ni Swala ya maiti.) na chooni, kwa kuwa Mtume ﷺ alisema: (Ardhi yote ni mahali pa kuswali, isipokuwa makaburini na chooni) [ Imepokewa na Tirmidhi.].

Na pia sehemu ya malazi ya ngamia kwa kauli yake Mtume ﷺ: (Musiswali katika malazi ya ngamia) [ Imepokewa na Tirmidhi.].

Na hapo ni mahali pa ngamia kulala na kukusanyika.

Kuswali makaburini
Kuswali chooni

Nne: Kusitiri tupu

Tupu ya mwanamume: ni kuanzia kitovuni hadi gotini.

Tupu ya mwanamke: ni mwili wake wote isipokuwa uso na vitanga vya mikono.

Kufinika mabega

Inamlazimu mwenye kuswali avae nguo yenye kufinika mabega yake na shingo yake, kwa kuwa Mtume alisema: (Asiswali mmoja wenu kwa nguo moja bila ya kuwa imefinika mabega yake) [ Imepokewa na Tirmidhi.].

isipokuwa yeye hakuwa akiswali juu yake Swala za faradhi) [ Imepokewa na Tirmidhi.].

Tano: Kuelekea Kibla

Na kibla ni alkaaba tukufu

Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Amesemna: { Elekeza uso wako upande wa msikiti wa Haram. Na popote mlipo, elekezeni nyuso zenu upande wake} {Al-Baqara: 144}.

Na inalazimu kuchunga baadhi ya mambo:

1. La wajibu kwa mwenye kuswali ndani ya msikiti wa Haram aielekee alkaba yenyewe. Ama yule anayeswali akiwa mbali na Alkaaba, basi ataelekea upande wa hiyo Alkaba na sio kuielekea yenyewe, kwa kuwa hawezi kuielekea yenyewe. Kwa hivyo, Mtume ﷺ alisema: (baina ya mashariki na magharibi ni kibla) [ Imepokewa na Tirmidhi].

2. Swala ya Sunna kwa aliyepanda mnyama, kibla chake ni ule upande ambao kile kipando kinaelekea, kwa kuwa ilithubutu kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akiswali [ Yusabbihu: anaswali Swala ya Sunna.] juu ya kipando chake akielekea popote pale kile kipando kinapoelekea, na alikiswali witri juu yake, isipokuwa yeye hakuwa akiswali juu yake Swala za faradhi) [ Imepokewa na Abu Daud.].

- Asiyejua Kibla Atafanya Nini?

Asiyejua kibla akiwa kwenye jengo au mahali penye watu walio karibu, atauliza au atajijulisha kibla kwa vibla vya misikiti au dira au jua au mwezi au vinginevyo. Akitoweza kujua basi atajitahidi na atafuata lile lenye nguvu katika dhana yake, kwa neno lake Mwenyezi Mungu: {Muogopeni Mwenyezi Mungu vile mnavyoweza} [64: 16].

Mwenye kuswali ndani ya msikiti wa Haram
Mwenye kuswali akiwa mbali na Alkaba