Mama Yake Mzee Amemwita Naye Yuko Katika Swalaah; Akatishe Swalaah?

SWALI: JE MAMA YANGU MZAZI AKINIITA KWA SAUTI KUBWA WAKATI NIPO KWENYE SWALA KISHA NIKAKATISHA SALA HIYO NA KUMSIKILIZA JE INASWIHI KUFANYA HILO AU NIMALIZE KWANZA UKIZINGATIA NI MAMA YANGU NA NI MZEE SANA. NAOMBA JIBU HILI LINANITATIZA

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani kwa swali lako kuhusu mama mzee kukuita ukiwa katika Swalaah. Katika ufafanuzi wa kisa cha Jurayj ambaye alikuwa akiswali na hakumuitikia mama yake alipomuita, wanachuoni wanatufafanulia kuwa, endapo mtu akiwa anaswali Swalaah ya Sunnah basi anaweza kuifupisha au hata kuikata na kumuitikia mzazi wake. Ama ikiwa ni Swalaah ya faradhi hiyo hawezi kuikatisha ila anaweza kuifanya fupi kwa kusoma Surah fupi na rukuu fupi na sujuud fupi na kisha kuimaliza na kumuitikia mama yake au mzazi wake aliyemuita. Na Allaah Anajua zaidi




Vitambulisho: