JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu mama kumnyonyesha mtoto akiwa na janaba. Hakika hakuna katazo lolote katika Uislamu ambalo linakataza jambo hilo. Hivyo, unaweza kumnyonyesha mtoto wako ukiwa na janaba au hata hedhi na hakuna tatizo lolote.
Na Allaah Anajua zaidi
Ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:
Ghuslu - Maana Ya Janaba, Na Kuoga Janaba Kwa Asiyeoa