Kuzuru Madina: fadhila zake na utukufu wake

7024

 

Majina ya mji wa Mtume wa Madina

1. Madina:

Amesema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka {Wanasema: lau tutarudi Madina watawatoa walio watukufu zaidi wale walio wanyonge zaidi} [63: 8].

2. Twaba:

Amepokewa Jabir bin Samurah t akisema: « Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema: (Hakika Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Ameipa Madina jina la Twaba) [Imepokewa na Muslim.].

3. Twayiba:

Amepokewa Zaid bin Tahabit t akisema kumpokea Mtume: (Hiyo ni Twayiba, inaondoa dhambi kama ambapo moto unaondoa uchafu wa fedha) [Imepokewaq na Bukhari na Muslim.].

Fadhila za Madina ya Mtume

1. Sa›d bin Abii Waqqaasw t amepokewa akisema kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: (Madina ni bora kwao lau walikuwa wanajua. Haiachi mtu yoyote kwa kutoipenda isipokuwa Mwenyezi Mungu humweka mtu bora kuliko yeye awe ni badala yake. Na yoyote atakayevumilia shida zake [ La’waa’: Shida na dhiki za maisha.] na usumbufu wake, nitakuwa ni muombezi wake au shahidi wake Siku ya Kiyama) [Imepokewa na Muslim.].

2. Abu Huraira t amepokewa akisema kwamba Mtume amesema: (Nimeamrishwa kwenye kitongoji [ Nimeamrishwa kwa kitongoji: nimeamrishwa nigurie hapo, niteremkie hapo na niishi hapo.] kinachokula vitongoji [ Kinachokula vitongoji: watu wake wata washinda watu wa miji mingine na kitakuwa ni kituo cha majeshi ya Kiislamu.], wanakiita Yathrib [ Wanakiita Yathrib: Watu wake walikiita Yathrib wakati wa jahilia, na sasa kinafaa kiitwe Madina.], nayo ni Madina, inawaondoa watu [ Kinawaondoa watu: Kinawatoa wabaya miongoni mwao.], kama vile kiriba [ Kiriba: ni kile kinachovuviwa na mfuzi wa chuma ndani ya moto.] kinvyoondoa uchafu wa chuma [ Uchafu wa chuma: uchafu wake na takataka zake.]) [Imepokewa na Bukhaeri na Muslim.].

Miongoni mwa mambo yanayo husu Mji wa Madina

1. Ni mji mtakatifu wa amani kuanzia eneo la ‘Ayr mpaka Thaur. nayo ni majabali mawili. miti yake haikatwi na wanyama wake hawawindwi.

Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: (Madina ni takatifu, kuanzia ‘Ayr mpaka Thaur. Basi yoyote mwenye kuzusha uzushi humo au akampa himaya mzushi, itamshukia yeye laana ya Mwenyezi Mungu, Malaika na watu wote) [Imepokewa na Bukhaeri na Muslim.].

Na Mtume Aliujalia mji wa Madina kuwa ni haram kama alivyo ujalia nabii Ibrahim Mji wa Makka, Amepokea Abdullah bin Zeyd kutoka kwa Mtume  (Hakika ibrahim u Alijalia Makka kuwa ni haram na akauwombea, na mimi nimeujalia mji wa madina kuwa ni haram kama alivyo ufanya Ibrahim Makka, na nimeombea katika mudi wake na pishi yake Mfano alivyo ombea nabii Ibrahim mji wa Makka) [Imepokewa na Bukhaeri.]

Tafauti ilioko baina haramu ya Makka na haramu ya Madini, nikuwa haram ya Makka imekuja nasi na kwa ijmai ya wanavyooni ama haram ya madina kuna khilafu baina ya wanachuoni lakini kauli sahahi ni kuwa ni haram

Jabali la Thaur
Jabali la ‹Ayr

2. Kuswali humo thawabu zake zinaongezwa mara nyingi zaidi

Amesema Mtume : (Swala moja kwenye msikiti wangu huu ni bora kuliko Swala elfu moja kwenye msikiti mwingine usiokuwa huo, isipokuwa Msikiti wa Haram) [Imepokewa na Bukhaeri.].

3. Ndani yake kuna bustani miongonimwa mabustani ya Pepo, na imesunniwa kuswali hapo:

Abu Huraira t alimpokea Nabii  akisema: (Baina ya nyumba yangu na mimbari yangu ni bustani miongoni mwa mabustani ya Peponi, na mimbari yangu iko juu ya Birika (hawdh) yangu) [Imepokewa na Bukhaeri na Muslim.].

Raudha tukufu

4. Masiih Dajali atakaekuja zama za mwisho hataingia humo, na janga la maradhi mabaya ya kuenea na kuua: [ Twaa›uun: maradhi mabaya.]

Anas bin Malik amepokewa akisema kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: (Dajali atakuja Madina awakute Malaika wanaulinda. Basi ugonjwa hatari wa kuambukiuza hautaingia humo wala Dajali hataingia, Mwenyezi Mungu Akitaka) [Imepokewa na Tirmidhi.].

5. Mtume  aliuombea mji wa Madina baraka:

Anas t alisema kwamba Nabii  alisema: (Ewe Mola! Ijaalie Madina baraka mara mbili zaidi ya ulivyoijaalia Makka) [Imepokewa na Bukhaeri na Muslim.].

6. kuwinda Makka mtu hupata madhambi na atalipa na kuwinda Madina mtu hupata madhambi lakini halazimiki na kitu chochote na madhambi ya kuwinda makka ni makubwa zaidi kuliko kuwinda Madina [Tazama Almumti’ juzuu ya 7-ukurasa 257]

Hukumu ya kuzuru Msikiti wa Mtume ﷺ

Kuuzuru Msikiti wa Mtume  si miongoni mwa masharti ya Hija wala nguzo zake wala wajibu zake. Hilo ni sunna, na inafaa ifanywe wakati wowote.

Na ni wajibu liwe lengo la ziara ni kuswali kwenye huo Msikiti na sio kaburi. Abu Huraira t amepokewa akisema kumpokea Mtume  kuwa alisema: (Hakufungwi safari isipokuwa kwenda kwenye misikiti mitatu: Msikiti wa Haram, Msikiti wa Mtume ﷺ na Msikiti wa Aqswa) [Imepokewa na Muslim.].

Amesema Shekhe wa Uislamu Ibnu Taimiyya: “Iwapo lengo lake la safari ni kuzuru kaburi ya Mtume  na sio kuswali kwenye Msikiti wake…. Basi msimamo wa maimamu na wengi wa wanavyuoni ni kuwa hili halikuwekwa na Sheria wala halikuamrishwa…Na hadithi kuhusu kuzuru kaburi ya Mtume  zote ni dhaifu kwa itifaki ya wajuzi wa Hadithi, bali ni hadithi zilizobuniwa. Hakuna yoyote miongoni mwa wakusanyaji wa vitabu vya sunna za Mtume  aliyepokea hadithi hizo, na hakuna yoyote aliyesimamisha hoja kutegemea hadithi yoyote katika hizo” [Majmuu’ al- Fataawaa, juzu. ii, uk. 26].

Hukumu za ziara na adabu zake

1. Mwenye kuzuru afikapo msikitini ni sunna kwake atangulize mguu wake wa kulia na aseme: (Ewe Mola! Nifungulie milango ya rehema zako) [Imepokewa na Muslim.].

2. Ataswali rakaa mbili za kuuamkia msikiti, na ikiwa ataziswali kwenye sehemu ya Raudha (Bustani ya Pepo) basi ni bora zaidi.

3. Ni sunna kuizuru kaburi ya Mtume  na marafiki zake wawili: Abu Bakr kisha ‘Umar.

4. Ni sunna kwa mwenye kuuzuru Msikiti wa Mtume  aswali Swala Tano ndani ya Msikiti wa Mtume, na amtaje Mwenyezi Mungu na kumuomba kwa wingi na kuswali sunna ya ziada hasa-hasa kwenye sehemu ya Raudha tukufu.

5. Ni sunna azuru msikiti wa Baqii’ kwa ajili ya kuswali humo, ingawa kuuzuru siku ya Jumamosi ni bora zaidi, kwa hadithi iliyopokewa na Ibnu ‘Umar t kuwa alisema: (Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  akienda kwenye msikiti wa Qubaa’ akiwa anapanda na akiwa anatembea, na akiswali hapo rakaa mbili). Na katika tamshi lingine: (Alikuwa akiujia msikiti wa Qubaa, yaani: siku ya Jumamosi) [Imepokewa na Muslim.].

6. Ni sunna kuzuru makaburi ya Baqii’ [ Baqii’: ni mahali ambapo Mswahaba wengi walizikwa hapo.], makaburi ya mashahidi na kaburi ya Hamza, kwa kuwa Nabii  alikuwa akiwazuru na kuwaombea na kusema: (Amani iwashukie nyinyi watu wa nyumba za Waumini na Waislamu. Na sisi, Mwenyezi Mungu Akitaka, ni wenye kukutana na nyinyi. Tunajiombea Mwenyezi Mungu uzima na tunawaombea na nyinyi) [Imepokewa na Muslim.].

Makosa na matanabahisho katika kuzuru

1- Kusafiri na kujisumbua kwa safari kwa lengo la kuzuru kaburi na sehemu za turathi zilizoko Madina. Lililowekwa na Sheria ni kufunga safari kuuzuru Msikiti wa Mtume , na ziyara ya kaburi yake inaingia ndani.

2- Kuelekea upande wa kaburi Wakati wa kuomba dua

3- Kumuomba Mtume  na kutaka haja kwake, badala ya Mwenyezi Mungu Aliyeshinda na Aliyetukuka, ni miongoni mwa ushirikina mkubwa kabisa.

4- Kujipukusa na kuta za Chumba alichozikwa Mtume ndani yake kwa lengo la kupata baraka ni miongoni mwa mambo ya uzushi yaliyoharamishwa na ni miongoni mwa njia zinazopelekea kwenye ushirikina.

5- Kuinua sauti kwenye kaburi ya Mtume  na kisimamo kirefu, na kukariri salamu kwa mbali kila anapoingia na kuweka mkono wa kulia juu ya wa kushoto juu ya kifua wakati wa kutowa salamu kama vile anavyo fanya akiwa kwenye Swala.