Kutawadha

80031

 

Maana ya Kutawadha

Udhu katika lugha

Uzuri na usafi

Udhu katika Sheria

Kutumia maji kwenye viungo maalumu kwa nia ya kujitwahirisha

Hukumu ya kutawadha

Kutawadha: ima ni lazima na ima inapendekezwa:

a. Ni lazima kutawadha kwa mambo matatu

1. Kuswali

Mwenyezi Mungu U Anasema: {Enyi Mlioamini! Mnapo simama kwa ajili ya swala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni} [5: 6]

2. Kutufu Alkaba:

Kwa kauli yake Mtume ﷺ kumwambia mwanamke aliye katika hedhi: (Usitufu mpaka utwahirike) [ Imepokewa na Bukhari.].

3. Kushika Msahafu:

Kwa neno lake Mwenyezi Mungu U: {Hawaigusi isipokuwa wale waliotwahiriwa} [56: 79]

Kutawadha kwa ajili ya kuswali
Kutawadha kwa ajili ya kutufu
Kutawadha kwa ajili ya kushika Msahafu

b. Kutawadha kunasuniwa katika mambo mengine yasiyokuwa hayo

Kwa neno lake Mtume ﷺ aliposema: (Hajilazimishi na udhu isipokuwa mwenye Imani) [ Imepokewa na Ahmad].

Na kunapendekezwa zaidi kutawadha wakati wa kujadidisha udhu kwa kila Swala, kutawadha kwa kumtaja Mwenyezi Mungu na kuomba, wakati wa kusoma Qur’ani, kabla ya kulala, kabla ya kuoga, na kutokana na kumbeba maiti na baada ya kila tukio la kutangua udhu, hata kama hataki kuswali.

Kutawadha kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu
Kutawadha wakati wa kulala
Kutawadha wakati wa kusoma Qur›ani
Kutawadha kwa ajili ya kubeba maiti

Fadhila za kutawadha

1. Ni sababu ya kupendwa na Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu aliyetukuka Anasema:{Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wenye kutubia na anawapenda wenye kujitwahirisha} [2: 222].

2. Ni alama ya umma wa Mtume Muhammad ﷺ kwa kuwa watakuja Siku ya Kiyama wakiwa weupe wa nyuso na viungo vya kutawadha

Amesema Mtume ﷺ (Hakika ya umma wangu watakuja Siku ya Kiyama wakiwa weupe nyuso na viungo kutokana na athari ya kutawadha, basi yoyote miongoni mwenu anayeweza kurefusha weupe wake na afanye) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

3. Kunafuta dhambi na makosa

Amesema Mtume ﷺ alisema (Mwenye kutawadha akautengeza udhu wake, basi dhambi zake hutoka mwilini mwake mpaka hutoka chini ya kucha zake) [Imepokewa na Muslim.].

4.Huinua daraja

Amesema Mtume ﷺ (Je, siwaonyeshi nyinyi kile ambacho kwacho Mwenyezi Mungu hufuta dhambi na huinua daraja? Wakasema “Ndio, tuonyeshe” akasema: “Ni kueneza maji ya udhu kwenye viungo, na kukithirisha hatua za kwenga misikitini na kungojea Swala baada ya Swala. Hiyo ndiyo jihadi) [Imepokewa na Muslim.].

Namna ya kutawadha

1.Kuhudhurisha nia moyoni.

2.Kutaja jina la Mwenyezi Mungu kwa kusema “bismillah”

3.Kuosha vitanga viwili vya mikono (mara tatu)

4.Kupiga mswaki: na mahali pake ni wakati kusukutua.

5.Kusukutua na kupaliza maji puani na kuyatoa.(mara tatu)

Madhmadhah: kutia maji kinywani na kuyageuza.

Istinshaaq: kuvuta maji puani kwa pumzi.

Kusukutua na kupaliza puani huwa kwa teko moja.

Istinthaar: ni kuyatoa maji puani.

6.Kuosha uso (mara tatu) pamoja na kupitisha maji ndani ya ndevu.

Na mpaka wa uso kiurefu ni kuanzia mameleo ya nywele za kichwa mpaka chini ya kidevu, na kiupana ni kuanzia sikio mpaka sikio.

7.Kuosha mkono wa kulia kuanzia ncha za vidole mpaka kifundoni (mara tatu), kisha mkono wa kushoto kama hivyo.

8.Kupangusa kichwa kwa kuupasha maji mkono kisha kupukusa mwanzo wa kichwa mpaka kwenye kishogo chake kisha kuurudisha mwanzo wake mara nyingine (mara moja).

9.kupangusa katikati mwasikio kwa kidole cha shahada, na inje yake kwa kidole cha gumba (mara moja)

10.Kuosha mguu wa kulia hadi kwenye vifundo (mara tatu) kisha mguu wa kushoto hivyohivyo.

11.Dua baada ya kumaliza kutawadha kwa kusema: “ Nashuhudia kuwa hakuna mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake asiye na mshirika. Na nashuhudia kuwa Muhammad ni mja wake na mjumbe wake” “Ewe Mola! Nijaalie mimi ni kati ya wenye kutubia, na unijaalie mimi ni kati ya wenye kujitwahirisha” “Kutakasika ni kwako, ewe Mola! na shukrani ni zako. Nashuhudia kuwa hakuna Mola isipokuwa Wewe. na kuomba msamaha na natubia kwako” [Imepokewa na Nasai.].

Kuosha vitanga viwili vya mkono.(mara tatu)
Kusukutua (mara tatu)
Istinshaaq: (mara tatu)
Istinthaar: (mara tatu)
Kuosha uso (mara tatu)
Kutoa mwanya kwenye ndevu
Kuosha mikono kuanzia ncha za vidole mpaka vifundoni (mara tatu, )
Kupangusa kichwa
Kupangusa masikio mawili (mara moja)
Kuosha miguu hadi kwenye vifundo (mara tatu)

Masharti ya kutawadha

1.Maji yawe twahara.

2.Maji yawe yafaa kutumiwa, yasiwe ya kuiba, kwa mfano.

3.Kuondoa chochote chenye kuzuia maji kufika kwenye ugozi, kama vile mafuta ya mshumaa na mfano wake.

4.Kutoeneza maji katika kutawadha,

Kuondosha rangi

Faradhi za udhu

1.Kutia nia. Na mahali pake ni moyoni, wala haitamkwi. Na lau mtu afanya matendo ya kutawadha kwa lengo la kujiburudisha au kujinadhifisha, bila ya nia ya kutawadha, basi hilo halimtoshelezi.

2.Kuosha uso. Na miongoni mwa huko ni kusukutua na kupaliza puani.

3.Kuosha mikono miwili pamoja na vifundo viwili.

4.Kupangusa kichwa chote, pamoja na masikio mawili

5.Kuosha miguu miwili pamoja na vifundo viwili.

6.Kufuatanisha beina ya viungo

Sunna za udhu

1.Kuosha vitanga viwili vya mikono mara tatu mwanzo wa kutawadha.

2.Kupiga mswaki.

3.Kuosha viungo mara tatu tatu, isipokuwa kichwa na masikio mawili, kwani hivyo havioshwi isipokuwa mara moja.

4.Kuanzia kuliani: nako ni kuanza upande wa kulia katika kuosha viungo vya udhu.

5.Kurefusha vingaja: yaani kupitisha zaidi ya vifundo vya mikono katika kuosha.

6.Kutoa mwanya kwenye ndevu ili kufikisha maji kwenye ngozi ya uso.

6.Kufikisha maji baina ya vidole vya mikono na miguu.

8.Kusugua viungo kwa mkono, na haitoshi kunyunyiza maji.

9.Kutumia maji kwa kiasi, kwa kuwa mtume ﷺ: amesema (Kutakuwa na watu katika umma huu watakaopitisha kiasi katika kujitwahirisha) [Imepokewa na Abu Daud.] Yaani watatumia maji ya kutawadhia kwa kupita kiasi

10.Dua baada ya kutawadha. Mtume ﷺ alisema: (Hakuna yoyote miongoni mwenu atakayetawadha, akaeneza maji ya kutawadhia kwenye viungo, kisha akasema “Nakiri kwa moyo kibaini kwa ulimi kuwa hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa mungu moja na Muhammad ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Ewe Mola! Nijaalie niwe miongoni mwa wenye kutubia na unijaalie ni miongoni mwa wenye kujitwahirisha” isipokuwa atafunguliwa milango ya pepo minane, auingie autakao) [Imepokewa na Tirmidhi.].

11.Kuswali rakaa mbili baada ya kutawadha. Mtume ﷺ alisema: (Mwenye kutawadha kama hivi ninavyotawadha, kisha akainuka akaswali rakaa mbili bila kusema na nafsi yake, atasamehewa dhambi zake zilizotangulia) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Kupiga mswaki
Kurefusha viungo vya kutawadha
Kufikisha maji baina ya vidole

Vitanguaji udhu

1. Kila chenye kutoka kwenye mojawapo ya njia mbili, mfano wa mkojo, choo, upepo (kushuta) kwa kauli yake Mtume ﷺ (Mwenyezi Mungu hakubali Swala ya mmoja wenu akitokwa na hadathi mpaka atawadhe) [Imepokewa na Muslim.].

2. kulala usingizi mzito ambao mtu hafahamu chochote. Na hi inaingia hapa, kama kukosa fahamu, na kupotezwa fahamu kikamilifu.

3. Kula nyama ya ngamia, kwa hadithi ya Jabir bin samurah kwamba mtu alimuuliza Mtume ﷺ: (Je, tutawadhe kwa kula nyama za ngamia? Akasema: (Ndio) [Imepokewa na Muslim.]

4. kugusa tupu kwa mkono bila ya kizuizi, kwa hadithi iliyo pokelewa na busra binti swafawan (RA) kuwa alimsikia mtume ﷺ akisema (mwenye kugusa tupu yake na atawadhe) [ Imepokewa na Abu Daud.]

Kula nyama ya ngamia
Usingizi mzito

Maelezo

1. Muislamu akiinuka kutoka usingizini na akataka kutawadha kwenye chombo, basi asichote humo kwa mikono yake mpaka aioshe mara tatu, kwa kauli yake Mtume ﷺ: (Akiamka mmoja wenu kutoka kwenye usingizi, basi na asiuvike mkono wake chomboni mpaka auoshe mara tatu, kwani hujui mkono wake ulilala wapi) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

2. Inapasa mtu awe na pupa la kuyafikisha maji kwenye kila kiungo kinacholazimu kuoshwa, hasahasa kwenye sehemu za baina ya vidole vya mikono na miguu, na baina ya ndevu na mashikio, pia visukusuku, vifundo na visiginyo kwa kauli yake Mtume ﷺ: (Ole wa motoni kwa visiginyo) [Imepokewa na Muslim.].

3. Asili ni kujengea yakini. Lau mtu alikuwa na yakini kuwa alitawadha kisha akafanya shaka kuwa udhu wake umetanguka, basi atajengea yakini yake nayo ni kuwa ana udhu. Na lau alikuwa na yakini kuwa hana udhu, kisha akafanya shaka: ametawadha au la? Basi yakini ni kuwa yeye hakuwa naudhu.

4. Muislamu anapotawadha, akaosha viungo vinavotakikana kuoshwa kwa mwenye kutawadha, mara mojamoja au mara mbilimbili, au vingine mara moja na vingine mara mbili au mara tatu, udhu wake ni sahihi.

5. Mtu akiswali bila ya udhu kwa kusahau, itamlazimu kurudia Swala anapokumbuka.

6. Mtu akitawadha kisha akaingiwa na njisi, basi ataiondoa najisi wala harudii kutawadha, kwa kuwa kuingiwa na najisi hakutangui udhu.

Kutia mkono chomboni baada ya kuinuka kutoka usingizini
Baina ya ndevu na masikio
Kisiginyo
Kufikisha maji kwenye vidole vya miguu
Udhu na afya kwa jumla

Kwenye makala yaliyotolewa kwenye jarida la Source

Linalotolewa na Umoja wa Mtaifa kuna maneno haya “Hakika kule kuoga kimpango na kutawadha kwa ajili ya kuswali katika jamii za Kiislamu kumesaidia sana kupunguza ueneaji ugonjwa wa trakoma ambao unaonekana kuwa ni sababu msingi ya upofu katika nchi za ulimwengu wa tatu..Na kuna watu wanaokaribia milioni mia tano wenye ugonjwa huu katika sehemu mbalimbali za ulimwengu ambao inawezekanakwao kujiepusha na upofu lau wafuata njia ya Uislamu katika usafi unaompasa kila Muislamu kabla ya kuswali. Na imetazamwa na kuonekana kwamba kwenye jamii za Kiislamu zenye kushikamana na Dini kupungua kiwango cha kupatikana na ugonjwa huu, bali imefikia daraja ya kukosekana” [ Utabibu wa kimtume ukiangaziwa na elimu ya kisasa (Ghiyath al-Ahmad).].

Ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:
Ghuslu - Wudhuu Unatenguka Akimgusa Mkewe?

Makatazo

1. Kuleta nia kwa sauti wakati wa kutawadha.

2. Kutumia maji kwa kupita kiasi.

3. Kuzidisha maosho matatu katika kutawadha, kwa riwaya iliyopokewa kuwa mbedui alikuja kwa Mtume ﷺ kumuuliza juu ya kutawadha, akamuonesha udhu mara tatutatu kisha akasema: (Kutawadha ni namna hii. Na mwenye kuzidisha hapo amekosea, amepita mpaka na amedhulumu) [Imepokewa na Abu Daud.].

Lakini inafaa kuongeza zaidi ya maosho matatu iwapo atakuwa hakukisafisha kiungo kwa maosho matatu, kama mtu aliyeingiwa na mafuta au kitu kingine mkononi.

4. Kutoeneza maji katika kutawadha, kwa riwaya iliyopokewa kuwa mtu alitawadha, akaacha paku kadiri ya ukucha kwenye nyayo, Mtume ﷺ akaliona na aksema: (Rudi utawadhe kwa uzuri)[ Imepokewa na Muslim.] akarudi kisha akaswali.

Na inaingia kwenye kukosa kueneza maji ya udhu:

a- kutoosha vifundo viwili vya miguu

b- kutoosha visukusuku kwa sababu ya wembamba wa mikono ya kanzu.

c- kutoosha weupe ulioko baina ya masikio na ndevu.

d- Kutoosha kitanga cha mkono wa kushoto pamoja na mkono wa kushoto.

e- mwenye kutawadha naye una mapaku ya mafuta.

f- kutawadha kwa mwanamke na juu ya vidole vyake pana pambo lenye kuzuia maji kufika kwenye ngozi.

g- kutofikisha maji kwenye vidole vya miguu iwapo maji hayapiti baina ya vdole.

5. Kupangusa shingo:

Si miongoni mwa matendo ya kutawadha,

6. kuleta dhikiri ambazo hazikuja katika Sheria, mfano:

a- kuomba dua maalumu katika kuosha kila kiungo.

b- kumwambia “zamzam” mwenye kutawadha.

Utumizi wa maji wa kupita kiasi