JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani kwa swali lako kuhusu madhii. Hakika ni kuwa madhii humtoka mtu akiwa na matamanio ya kutaka kufanya tendo la ndoa. Hakika hakuna kipimo cha kuweza kujua kuwa madhii yamekutoka isipokuwa ule utokaji wake hukujulisha hilo kwani madhii humtoka mtu akiwa macho tofauti na manii ambayo yanaweza mtu akiwa amelala au yuko macho. Ikiwa hali ni hiyo, yanapotoka utahisi na hivyo kujua sehemu yalipoingia. Ikiwa hukuweza kutambua yameingia katika sehemu gani ya nguo, japokuwa jambo hilo ni muhali, ni wewe kuinyunyiza nguo yote kwa maji au kuiosha. Kwa kufanya hivyo utaondoa tatizo linalokukabili. Manii yanapomtoka mtu akiwa amelala au yuko katika kitendo cha jimai basi hata yakiwa kidogo anapaswa kuoga ili awe safi kwa ajili ya ‘Ibaadah kadhaa. Kwa hiyo, ile hali ya kutokwa na manii tu inakubidi uoge. Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate manufaa zaidi: Tofauti Baina Ya Manii Na Madhii Na Hukumu Zake Za Ghuslu Hukmu Ya Wadii Na Madhii 008 Nini Hukumu Ya Majimaji (utoko) Yanayotoka Kwenye Utupu Wa Mwanamke Na Kile Kiitwacho Unyevunyevu Wa Utupu Wa Mwanamke? Mwanamke Akitokwa Na Majimaji, Je, Aoge Janaba? Na Allaah najua zaidi