JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Kuhusu wagonjwa wenye kuhitaji kusafishwa mafigo (kidney dialysis) ni kwamba Halmashauri (Jopo) Ya Kudumu Ya Utafiti Wa Kiislaam imetowa Fatwa kwamba kusafisha mafigo (kidney dialysis) inabatilisha (inavunja) Swawm. Hivyo basi mwenye ugonjwa huo, hapasi kufunga siku anazofanya usafishaji huo wa figo. Akiweza atalipa siku hizo baada ya Ramadhaan, na ikiwa hawezi kulipa kutokana na hali ya afya yake, basi alishe maskini mmoja kila siku. Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo kuhusu kafara ya Swawm: Kulipa Swawm Na Kafara Hakuweza Kufunga Kwa Muda Wa Miaka Minne Kwa Sababu Ya Ugonjwa Mwenye Deni La Swawm Ikiwa Ana Ugonjwa Wa Kuhitaji Kutumia Dawa Kwa Wakati Bila Kuacha, Afanyeje? Fidia Asiyeweza Kufunga Anaweza Kulipa Baada ya Ramadhaan? Na Allaah Anajua zaidi