Kupukusa khofu mbili, soksi mbili, utata, bendegi na mfano wa hivyo

14270

 

Kwanza: kupukusa khofu mbili na soksi mbili

Maana ya Khofu na Soksi

Khofu

Ngozi inayovaliwa miguuni

Soksi

Kinachovaliwa miguuni cha pamba na mfano wake

Hukumu ya kupangusa khofu mbili na soksi mbili

Sheria imeweka upangusaji wa khofu mbili na soksi mbili, kwa hadithi nyingi mikongoni mwazo ni riwaya iliyopokewa na Anas bin Malik t alipoulizwa kuhusu upangusaji wa khofu mbili, alisema: Mtume ﷺ alikuwa akipukusa juu ya hivyo) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Masharti ya kupangusa khofu mbili na soksi mbili

1.Kuzivaa baada kujitwahirisha kikamilifu. Mughirah amepokewa akisema: (Nilikuwa na Mtume ﷺ safarini, nikafanya haraka kumvua khofu zake, akasema: “Ziache, kwa kuwa mimi nilizivaa katika hali ya utwahara” akapukusa juu yake) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

2.Ziwe ni zenye kusitiri miguu mpaka kwenye vifundo, zikiwa chini ya vifundo viwili hazipukuswi, kwa kuwa vifundo si katika nyayo.

3.ziwe zimetengezwa kwa vitu vilivyo twahara.

4.Ziwe zinafaa kutumiwa na zisiwe ni miongoni mwa vitu haramu kama hariri kwa wanaume.

5.Kule kupukusa kuwe ndani ya muda uliowekwa. Kwani Mtum ﷺ aliweka muda maalumu wa kupukusa (usiku na mcha kwa mkazi na siku tatu kwa msafiri). Haifai kupitisha muda huo.

6.Kupukusa kuwe kwenye kujitwahirisha kutokana na kutangukiwa na udhu na sio tukio kubwa la ukosefu wa twahara. Imepokewa na Swafwan bin Assal (R.A.) kuwa alisema (Alikuwa Mtume ﷺ akituamrisha tukiwa safarini tupukuse khofu zetu, na tusizifue siku tatu, kwa kwenda haja, kukojoa na kulala isipokuwa kutokana na janaba) [ Imepokewa na Bukhari.], yaani mwenye janaba ni juu yake azivue khofu mbili kwa kuoga kisha azivae mara nyingine.

Namna ya kupangusa khofu mbili na soksi mbili

Atapukusa juu ya khofu kwa mikono yake miwili ikiwa majimaji, kuanzia kwenye vidole vya miguu yake mpaka kwenye muundi wake mara moja. Atapukusa mguu wakulia kwa mkono wa kulia na mguu wa kushoto kwa mkono wa kushoto.

Wala hapukusi chini ya khofu wala kisiginyo chake. Ali t amesema: (Lau Dini ilikuwa ni kwa maoni ingekuwa kupukusa chini ya khofu ni bora kuliko juu yake. Na kwa hakika nilimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu akipukusa juu ya khofo zake) [ Imepokewa na Abu Daud.].

Kupangusa kwa mikono yake miwili

Muda wa kupangusa khofu mbili na soksi mbili:

Usiku na mchana kwa mkazi na siku tatu pamoja na masiku yake kwa msafiri.

Dalili yake ni neno la Ali  (Mtume amemwekea msafiri siku tatu na masiku yake, na amemwekea mkazi wa mji usiku mmoja na mchana wake) [ Imepokewa na Nasai].

Hesabu ya muda wa kupangusa

Muda unaanzia mwanzo wa kupangusa baada ya kutangukiwa na udhu. Avaapo soksi mbili akiwa kwenye hali ya utwahara, kisha akaukosa twahara kwa mara ya kwanza, basi kuanzia kupangusa huku kutahesabiwa usiku na mchana (masaa ishirini na nne). Mfano wake ni mtu aliyetawadha, akaosha miguu yake kisha akavaa soksi zake, akaswali alfajiri, na wakati wa saa nne asubuhi alitokewa na vitanguo, na udhu wake ukatanguka. Ilipofika saa tano asubuhi alitawadha na akaswali Dhuha na akapukusa soksi zake. Hapa yafaa kwake yeye kuendelea kuvaa soksi mbili na kupukusa juu yake mpaka saa tano asubuhi ya siku ya pili.

Hayo ni kwa mkazi ama msafiri ni kwa muda wa siku tatu na masiku yake

Venye kutangua upangusaji wa khofu mbili na soksi mbili

1.Kumalizika muda wa kupukusa.

2.kuzivua soksi mbili au mojawapo.

3.kupatikana na tukio kubwa la kutangua twahara. Imepokewa kutoka kwa Swafwan bin Assaal t: (Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akituamrisha tukiwa safarini tusivue khofu zetu kwa siku tatu na masiku yake isipokuwa kutokana na janaba, lakini kutokana na choo, mkojo na kulala) [ Imepokewa na Tirmidhi].

Kupangusa chini ya khofu
Kupangusa kisiginyo
Kuvua soksi kunatangua upangusaji

Pili: Kupukusa juu ya kitata, bendeji na plasta

Maana ya utata, bendeji na plasta

Kitata

Ni kile kinachofungwa mahali palipovunjika kiwe ni tambara zito au vipande vya mti au mfano wake

Bendeji

Ni kitu kinachotatiwa kwenye jaraha au mahali palipochomeka au kinginecho kwa kitambaa au mfano wake ili kujitibu nacho.

Plasta

Ni kile kinachobandikwa kwenye jaraha na mfano wake kwa kujitibu.

Dalili ya kusihi kupangusa juu ya vitata kisheria

Amepokewa Jabir t alisema: (Tulitoka kwenda safari, na mmoja wetu akagongwa na jiwe kichwani mwake likampasua. Kisha akaota (usingizini). Akawauliza wenzake: “Je mnanipatia ruhusa yoyote kisheria ya mimi kutayamam?” Wakasema “Hatukupatii madamu wewe unaweza kutumia maji”. Akaoga na akafa. Tiliporudi kwa Mtume ﷺ alielezwa habari hiyona akasema: “Wamemuua! Mwenyezi Mungu Awaue. Si wangeuliza ikiwa hawajui? Kwani dawa ya kutojua ni kuuliza.” Hakika ingalimtosha yeye kutayamamu na kufunga kitamba kwenye jaraha lake, kisha akapukusa juu yake, na kuosha sehemu zisaliezo za mwili wake) [ Imepokewa na Abu Daud.].

Masharti ya kupangusa juu ya vitata, bendeji na plasta

1.Imesharutishwa katika bendeji au vitata visizidi sehemu inayotakikana kutibu pamoja na sehemu za kandokando yake zinazohitajika kuthibitisha vitu hivi.

2.Haisharutishwi katika kufunga bendeji au vitata awe mtu yuko kwenye twahara, vilevile haisharutishwi muda maalumu, madamu vinahitajika kusalia basi yafaa kupukusa juu yake wakati wakujitwahirisha na tukio kubwa na dogo la ukosefu wa utwahara. Na wakati wowote ule mahitaji yake yameondoka ni lazima kuvivua na kukiosha kiungo husika wakati wa kujitwahirisha.

3.Kuhusu mabendeji na vitata na mfano wahivyo ambavyo ni rahisi kuzirudisha itatazamwa:

a. Ikiwa kuvitoa na kuosha sehemu za chini yake ni sahali bila madhara au kusababisha jaraha kuchelewa kupoa, basi atavitoa aoshe sehemu za chini yake, kisha avirudishe.

b. Iwapo si rahisi kuvitoa na kuosha sehemu za chini yake bila kudhurika au kuchelewa kupoa, atapukusa juu yake wakati wa kuosha kiungo kile ambacho vitu hivyo viko juu yake.

Namna ya kuhisabu muda wa kupangusa

Namna ya Kupangusa juu ya vitata
Namna ya kupangusa juu ya bendeji
Namna ya kupangusa juu ya bendeji 

Ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:
Swalah Kwa Khofu Ya Kuweko Najasa Ya Mbwa