Kuoga

30795

 

Maana ya Kuoga

Kuoga kilugha

Kueneza maji juu kitu

Kuoga kisheria

Kueneza maji mwilini kwa namna maalumu kwa kusudia kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu U

Yenye kuwajibisha kuoga

1. Kutokwa na manii

Na manii ni maji meupe, mazito yanatoka kwa kasi wakati wa matamanio, na yana harufu inayofanana na yai lililoharibika, kwa neno lake Mwenyezi Mungu : {Na mkiwa na janaba jitwahirisheni} [5: 6]

na neno lake Mtume ﷺ kumwambia Ali (RA). (Ukimwaga maji oga) [ Imepokewa na Abu Daud.].

Fadh’h almaa’: kutoka maji kwa kasi, na makusudio yake ni manii

- Maelezo

1. Lau mtu aota na asitokwe na manii, basi haimpasi kuoga. Na yanapotoka baada ya kuamka itamlazimu kuoga.

2. Akikuta manii na asikumbuke kuwa ameota itamlazimu aoge kwa ajili ya kutokwa na manii. Mtume ﷺ amesema: (Hakika Ulazimu wa kutumia maji unasababishwa na kutokwa na maji) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.], yaani: Kuoga kunalazimu kwa kutokwa na manii.

3.Lau ahisi kuwa manii yanataka kutoka kisha yasitoke, basi haimlazimu kuoga.

4.Lau atokwa na manii kwa hitilafu fulani mwilini mwake au ugonjwa bila ya matamanio, basi hana ulazima wa kuoga.

5.Akiwa na janaba akaoga, kisha akatokwa na manii baada ya kuoga, haimlazimu kuoga tena, kwa kuwa hayo kwa kawaida hutoka bila matamanio. Na kutoka shakani ni kutawadha.

6.Aamkapo usingizini mwenye kulala akapata urutuba(maji maji ya manii) ambao hajui sababu yake, huwa ni moja kati ya hali tatu:

a. Akate kuwa ni manii, na hapo itampasa kuoga, awe akumbuka kuwa ameota au hakumbuki.

b. Akate kuwa si manii, hapo haimpasi kuoga, na hukumu yake ni hukumu ya mkojo.

c. Awe na shaka baina ya kuwa ni manii au si manii. Hapo ni juu yake ajitahidi, akikumbuka chenye kutilia nguvu kuwa ni manii, basi ni manii. Na akikumba chenye kutilia nguvu kuwa ni madhii, basi ni madhii. Na akitokumbuka chochote itamlazimu kuoga kwa kuondoa shaka.

7.Aonapo manii na asikumbuke aliota lini, basi itamlazimu kuoga na kuzirudia Swala usingizi wa mwisho aliyoulala.

2.Kuundama

Nako ni kukutana tupu ya mwanamume na tupu ya mwanamke, kwa kuingia sehemu ya mbele yote ya dhakari kwenye tupu, hata bila ya kushusha manii, kwa kauli ya Mtume ﷺ: (Tupu ikishapita kwenye tupu, basi kuoga huwa kumeshalazimu) [ Imepokewa na Tirmidhi].

3. Kafiri kusilimu

Kwa kuwa Mtume ﷺ alimuamuru Qais bin ‘Aswim aliposilimu kuoga [ Imepokewa na Abu Daud.].

4. Kukatika damu ya hedhi na nifasi

Kwa hadithi ya ‹Aishah kwamba Mtume ﷺ alimwambia Fatimah binti Abi Hubaish (Hedhi ikija acha kuswali, na ikiondoka oga na uswali) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Na nifasi ni kama hedhi kulingana na maoni ya wanavyuoni kwa umoja wao.

5. Kifo

Kwa kauli yake Mtume ﷺ katika hadithi ya kumuosha binti yake zainab alipokufa: (Muosheni mara tatu, au tano, au zaidi ya hapo mkiona hivyo) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Namna ya kuoga

Linalolazimu katika kuoga ni kueneza maji kwenye mwili kwa namna yoyote ile. Lakini inapendekezwa afuate vile Mtume ﷺ alivyooga, nayo ni kama ilivyoelezwa na Maimunah, Mama wa Waumini  aliposema (Mtume aliweka chombo cha maji ya kujitwahirishia na janaba, akajimiminia maji kwenye kitanga cha mkono wa kushoto akitumia kitanga cha mkono wake wa kulia mara mbili au tatu, kisha akaosha tupu yake, kisha akapiga mkono wake kwenye ardhi au ukuta mara mbili au tatu, kisha akasukutua na akapaliza puani, akaosha uso wake na mikono yake, kisha akajimiminia maji kichwani mwake, kisha akaosha mwili wake, kisha akajiweka kando akaosha miguu yake) [ Imepokewa na Bukhari].

Asema Maimunah: (Nikamletea kitambaa, hakukitaka, akawa ajifukuta kwa mkono wake).

Hivyo basi namna ya kuoga ni:

1. Aoshe vitanga vyake vya mikono, mara mbili au tatu.

2. Aoshe tupu yake.

3. Apige mkono wake kwenye ardhi au ukutani, mara mbili au tatu.

4. Atawadhe kama vile anavyotawadha kuswali, bila ya kupukusa kichwa chake na kuosha miguu yake.

5. ajimiminie maji kichwani.

6. Aoshe mwili wake wote.

7. Ajiweke kando na aoshe miguu yake.

FAIDA

- Si lazima kwa mwanamke kufunguwa nywele zake anapo taka kuoga janaba au hedhi, Itamtosheleza kujimiminia maji na kuhakikisha kuwa maji yamefika kwenye ngozi ya kichwa.

- inapendekezwa kwa mwanamke anapo oga hedhi au nifasi achukuwe pamba au mfano wake na aiweke misk kisha ajiondoshe athari ya damu.

- Mtu anapo oga janaba inasihi kwake kuswali kwa josho hilo, sawa alitia nia ya kutawadha ama hakutia

Yanayoharamishwa kwa mwenye janaba

1. Kuswali:

Kwa neno lake Aliyetukuka: {Enyi mlioamini! Msikaribie Swala hali mmelewa, mpaka myajue mnayo sema, wala hali mna janaba isipo kuwa mmo safarini mpaka muoge}.[ Al-Nisaa 43]

2. Kuitufu Nyumba Tukufu (Alkaba):

Kwa neno lake Mtume ﷺ: (Kutufu Alkaba ni kama kuswali) [ Imepokewa na Nasai.].

3. Kugusa Msahafu:

Kwa neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Hawaigusi isipokuwa waliotwahirishwa} [56: 9].

Na neno la Mtume ﷺ (Haugusi Msahafu isipokuwa aliye twahara) [ Imeipokewa na Malik katika Muwatta’.].

4. Kusoma Qur›ani:

Imepokelewa kutoka kwa Sayyidna Ali(RA) akisema (alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akitoka chooni na akitusomea Qur’ani, na akila nyama pamoja na sisi. Na hakuwa akizuiliwa na kitu chochote kusoma Qur’ani isipokuwa janaba) [ Imepokewa na Tirmidhi].

5. Kukaa msikitini isipokuwa kwa mpita njia:

Kwa neno lake Aliyetukuka: {Enyi mlioamini! Msikaribie Swala hali mmelewa, mpaka myajue mnayo sema, wala hali mna janaba isipo kuwa mmo safarini mpaka muoge}. [ Al-Nisaa 43]

Kuswali
Kutufu Alkaba
Kushika Msahafu
Kusoma Qur›ani
Kukaa msikitini

Kuoga kunakopendekezwa

1. Kuoga kwa Ijumaa

Kwa kauli ya Mtume ﷺ: (Mwenye kutawadha kwa ajili ya kwenda Ijumaa, hilo ni jambo zuri, na mwenye kuoga, basi kuoga ni bora) [ Imepokewa na Abu Daud.]

2. Kuoga wakati wa kuhirimia kwa Umra au Hija:

Imepokewa kutoka kwa Zaid bin Thabit  kwamba yeye alimuona Mtume ﷺ akijiondoa na nguo za kawaida kwa ibada ya Hija na akaoga [ Imepokewa na Tirmidhi]

3. Kuoga baada ya kuosha maiti:

Kwa neno la Mtume ﷺ: (Mwenye kuosha maiti aoge) [ Imepokewa na Ibn Majah.]

4. Kuoga baada ya kila tendo la ndoa

imepokewa na Abu Rafi›  kwamba Mtume (SAW.) siku moja aliwapitia wake zake, na alikuwa akioga baada ya kumaliza kwa huyu na kwa yule. Mpokeaji asema: (Nikamwambia”Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! usiuoge mara moja? Akasema (SAW “ Hili ni safi zaidi, bora zaidi na twahara zaidi) [ Imepokewa na Abu Daud.].
Ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:
Ghuslu - Je, Inapasa Kufanya Ghuslu Baada Ya Kutokwa Na Manii Bila Ya Kujimai?

Makatazo

1- kuchelewesha kuoga janaba mpaka utoke wakati wa Swala.

2- kwa mwanamke aliyetwahirika na hedhi kuacha Swala ya wajibu. Na lau atwahirika kabla ya kutoka wakati wa adhuhuri kwa kadiri ya rakaa moja, basi itampasa aoge na aswali adhuhuri. Mtume ﷺ amesema (Mwenye kuwahi rakaa moja ya asubuhu kabla ya kuchomoza jua, basi amewahi Swala ya asubuhi. Na mwenye kuwahi rakaa moja ya alasiri kabla ya jua kuzama, basi amewahi Swala ya alasiri) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].