Kuhirimia

8073

 

Maana ya ihram

Kuhirimai kilugha

Ni kuzuia

Kuhirimia kisheria

Ni nia ya kuingia kwenye ibada ikifungamana na mojawapo ya matendo ya Hijja

Na haifungamani Iharamu ila kwa nia, Mtu hahisabiwi kuwa amehirimia kwa kule kuazimia kwenda hijja au Umra kwa sababu toka aliposafiri mji wake huwa ameazimia kuhiji au kufanya umra, na wala hawi ni mwenye kuhirimia kwa kuvaa ihram au kuleta talbiya bila kutia nia ya ibada ya hijja kwa neno lake Mtume (saw) (Hakika amali zote ni kwa nia na kila mtu hulipwa kama alivyo nuiya) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Mambo yanayo pendekezwa katika ihramu

1. Kuoga

Khaarijah bin Zaid bin Thaabit t alipokea kutoka kwa baba yake kwamba alimuona Mtume(saw) akivua nguo na kuoga kwa sababu ya kuhirimia Hija [Imepokewa na Tirmidhi.].

2. Kujisafisha

Nako ni kuondoa nywele za makapwa yake na kinena chake na kupunguza masharubu yake na kucha zake.

3. Kujitia manukato

Kwa hadithi iliyopokewa na ‹Aishah t kwamba alisema: (Nilikuwa nikimtia manukato Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya ihramu yake anapohirimia) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Wala hazitii manukato nguo zake, kwa kauli ya Mtume (saw): (Na msivae nguo yoyote iliyopakwa zafarani wala manukato ya wars [ Alwars: nimmea wa majano wenye harufu mzuri]) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Manukato

4. Kuvua nguo za kushona [Makhiitw: Kila nguo iliyoshonwa kwa kipimo cha kiungo au juu ya mwili wote, mfano wa kanzu na suruali.] kabla ya kuhirimia [Ama baada ya kuhirimia, ni lazima kwake avue nguo za mzunguko, kwa kuwa hizo ni miongoni mwa vitu] na kuvaa shuka ya chini na ya juu zilizo nyeupe na viatu.

Kwa kauli yake Mtume (saw): (Na ahirimie mmoja wenu akiwa na shuka ya chini na ya juu na viatu. Akikosa viatu, avae khofu mbili, na azikate mpaka kwenye vifundo vya mguu) [Imepokewa na Ahamad]

Ama mwanamke atavaa nguo anazo taka, wala hakuna nguo ya rangi maalumu, lakini ajiepushe na kufanana na Wanaume na nguo za mapambo, na wala havai nikabu na soksi za mikono [ Quffaaz: nguo inayovaliwa na mwanamke kufinika mkono] katika kuhirimia.ila akiwa kati ya wanaume ajnabi atateremsha nguo yake na kuufunika uso wake, kwa ilivyo thubutu kutoka kwa bibi Aisha t Amesema (Ulikuwa msafara unapo pita mpele yetu na sisi tukiwa na Mtume (saw) Kwenye ihraamu wakiwa mkabala na sisi akitermsha mmoja wetu jilbabu yake akifunika uso wake wakitupita tukifunuwa) [Imepokewa na Abuu Daud.]

Viatu alie kwenye ihram
Niqabu kwa aliye kwenye ihram
Soksi za mikono kwa mwanamke aliye kwenye ihram
Kikoi na nguo ya juu kwa aliye kwenye ihram

Mambo yaliyoharamishwa kwa ajili ya ihramu

1. Kufinika kichwa cha mwanamume kwa kitu chenye kuambatana nacho.

Kwa hadithi iliyopokewa na Ibnu Umar t kwamba mtu alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Huyu aliye kwenye ihramu atavaa nguo gani. Mtume wa Mwenyezi (saw) akasema: (Msivae kanzu wala vilemba wala suruali [ Nayo ni ile inayojulikana kama bantaal.] wala kanzu zilizoshikana na kofia [ Baraanis: kila nguo ambayo kofia yake imeshikana nayo.]) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Na amesema(saw) kuhusu mtu aliyekufa na yeye yuko kwenye ihramu: (Msimfinike kichwa chake kwa kitambara [ Laa tukhammiruu ra’sahu: Msimweke mtandio kichwani mwake, nao ni wakufinikia kichwa.], kwani atafufuliwa Siku ya Kiyama akileta Labbaika..) [Imepokewa na Bukhari.].

Ama ikiwa hakikushikana na kichwa kama kutumia mwavuli uo hema au sakafu ya nyumaba au gari hakuna ubaya wowote

Kofia kwa aliye kwenye ihramu
Kilemba kwa aliye kwenye ihramu
Kuvaa suruali kwa aliye kwenye ihramu
Mwavuli kwa aliye kwenye ihramu

2. Kuvaa nguo ya kushonwa kwa mwanamume

Maana ya nguo ya kushonwa: ni iliyoshonwa kwa kadiri ya mwili au sehemu ya mwili, kama vile suruwali, kanzu, khofu (soksi nzito), soksi, soksi za mkononi na mfano wake, kwa hadithi iliyopokewa na Ibnu ‘Umar iliyotangulia: (msivae kanzu, vilemba, suruali, Kanzu zilizoshikana na kofia wala khofo.) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Akitopata mwenye kutaka kuhirimia Hija isipokuwa kikoi, basi inafaa avae suruali mapaka atakapopata kikoi [ Kama mtu aliyesahau mavazi ya kuhirimia kwenye sanduku la safari ndegeni au melini na asiwe na kikoi, basi inafaa avue nguo zake na ahirimie akiwa amevaa suruali na alitatie shati lake liwe ni kama kishali, mpaka atapofika kwenye bandari atatoa mavazi y ake ya kuhirimia na atayavaa na halazimiwi na kitu chochote.]. Na akitopata viatu, inafaa avae khofu, kwa kauli yake Mtume(saw): (Akitopata viatu na avae khofu mbili na azikate mpaka zifike kwenye vifundi vya miguu) [Imepokewa na Ibnu Khuzaimah.].

Khofu (soksi nzito) kwa aliye kwenye ihramu
Buti
Kuvaa nguo ya kushonwa kwa aliye kwenye uhramu

3. Kuua kiwindwa wa barani au kumwinda

Kwa neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Msiuwe viindwa na nyinyi mmehirimia Hija} [5: 95].

Yaani na nyinyi muko kwenye ihramu ya Hijja na ‘Umra. Na neno lake Aliyetukuka: {Na mmeharamishiwa viindwa vya barani daima mnapokuwa katika hali ya ihramu} [5: 96].

Na maana ya kiwindwa cha barani ni kinachokuwa cha mwituni miongoni mwa wanyama na ndege.

Ama mnyama wa kufugwa si kiindwa. Hivyo basi inafaa kwa aliye kwenye ihramu kuchinja kuku, wanyamahoa (mbuzi, ngo’mbe, ngamia) na mfano wao. Ama kiindwa cha baharini kinafaa, kwa neno la Mwenyezi Mungu Aliyetukuka : {Mmehalalishiwa kiindwa cha baharini na chakula chake} [5: 96].

Ama mnyama aliye haramu kuliwa kama nyoka na nge. inafaa inafaa kwa aliye kwenye ihramu kumuua mnyama yoyote anayemshambulia iwapo hakuna njia nyingine ya kujikinga naye isipokuwa hiyo.

Nyoka
Ngekitumbo
Kiindwa cha bahari ni halali kwa aliye kwenye ihramu
Yafaa kuchinja mnyamahoa
Kiindwa cha bara miongoni mwa ndege

4. Kunyoa nywele, kuzipunguza au kuzisumua

Kwa neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Na msinyoe vichwa vyenu mpaka wafike wanyama wa kuchinjwa kwa ibada ya Hija mahali pake} [2: 196].

Makatazo haya yanakusanya nywele za mwili wote kwa kukisia nywele za kichwa.

Kunyoa au kupunguza

5. Kukata kucha

Sawa ziwe ni kucha za miguu au mikono.

Kukata kucha za mikono
Kukata kucha za miguu

6. Kujipaka Manukato mwilini na nguoni

Imekatazwa kwa mwenye kuhirimia Hija kutia manukato mwilini mwake au kwenye nguo yake baada ya kuingia kwenye ihramu, au kuyanusa kwa kusudia, kwa hadithi iliyopokewa na Ibnu ‹Umar iliyotangulia ambayo ndani yake yamo maneno haya: (wala msivae nguo yoyote iliyotiwa zafarani au wars [ Wars: ni mmea rangi ya manjano wenye harufu nzuri hutumiwa kwa kupaka.] ) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.],

na kwa hadithi ya ule aliyekufa katika hali ya ihramu ambayo alisema (saw): (Na msimtie manukato [ Tuhannitwuuhu: tumieni hanuutw. Nayo ni mafuta mazuri yanayochanganywa kafani za maiti.] ) [Imepokewa na Bukhari.].

Kuzipaka Manukato nguo za kuhirimia
Kujipaka manukato mwilini

7. Kufunga ndoa

Kwa hadithi iliyopokewa na Uthmaan (R.A.) kwamba Mtume wa Mwewnyezi Mungu (saw) alisema: (Aliye kwenye ihramu haoi wala haolewi wala haposi) [Imepokewa na Muslim.].

8. Kuundama

Nako ni kujamii kwenye tupu ya mbele, kwa neno la Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Yoyote anayeingia kwenye ibada ya Hija, basi asiuundame`} [2: 197].

Ibnu ‘Abbas t amesema: “Huko ni kujamii”. Nalo ni jambo kubwa zaidi lililoharamishwa kwa sababu ya ihramu.

9. Kustarehe kwenye sehemu isiyokuwa tupu

Kama vile kubusu na kushika, kwani hizo ni njia za kupelekea kuunadama kulikoharamishwa.

Mambo yaliyoharamishwa kwa mwanamke aliye kwenye ihramu

Mwanamke ni kama mwanamume katika mambo yaliyoharamishwa kwa sababu ya ihramu, na anatafautiana namwanamume katika mambo yafuatayo:

1- yeye afaa kuvaa nguo ya mzunguko.

2- anafaa kufinika kichwa chake.

3- Haifai kujifinika uso [ Niqaab: ni kile ambacho mwanamke anajifinikia uso wake kwacho.] na kuvaa soksi za mikono [ Quffaaz: kinachovawa mkononi.] kwa kauli ya Mtume (saw): (Na asijifinike uso mwanamke aliye kwenye ihramu na asivae soksi za mikono) [Imepokewa na Bukhari.]

Na mwanamke ajifinike uso wake mbele ya wanaume wa nje bila kuvaa nikabu nako ni kuteremsha nguo kichwani mwake. Na inafaa kwake kuvaa dhahabu.

Maelekezo

1. Swala inayoitwa Swala ya sunna ya kuhirimia haina asili katika Sheria, pia hakuna katika Sheria kujilazimisha na dua fulani katika kuhirimia.

2. Lau mtu asafiri kwa ndege na akakhofia asimakinike kuvaa nguo za ihramu anapofikia mahali pa Kuhirimia, basi atavaa nguo zake kutoka nyumbani au kwenye kiwanja cha ndege, na hatahesabiwa kuwa amehirimia mpaka atie nia ya ihramu kabla hajakaribia mahali pa kuhirimia.

3. Baadhi ya mahujaji wanaacha wazi mabega yao ua upande wa kulia wanapovaa nguo za ihramu, kunakoitwa idhtwibaa'. Hili si sahihi, kwani idhtwibaa' inafanywa wakati wa tawafu ya kufika Makka (quduum) peke yake. Ama tawafu nyinginezo atafinika mabega yake.

Kuliacha wazi bega la kulia katika kuvaa ihramu

Naswaha kwa Mahujaji wote

Akiazimia muislamu kusafiri kwenda hija au umra ni lazima afuate muongozo yanayo fuata:

1. ausie jamaa zake na watu wake kumcha mwenyezi mungu, nako ni kutekeleza maamrisho yake na kujiepusha na makatazo yake.

2. aandike watu anowadai na wanao mdai na ashuhudishe juu ya hilo

3. afanye haraka kutubia twaba iliyo yakweli kutokamana na madhambi yote Amesema Mwenyezi Mungu {Enyi Mulio amini tubuni kwa Mwenyezi mungu Toba iliyo ya kweli } [ATtahriim: 8]

4. Ikiwa atakuwa na dhuluma za watu kutokana na nafsi au mali au hishima awaregeshee wenyewe au awaombe msamaha kabla ya hajasafiri, kama ilivyo sihi kutoka kwa Mtume (saw) (Yoyote atake kuwa na dhuluma ya ndugu yake kutokamana na mali au hishama amuombe msamaha hapa duniani kabla yakutofaa dinari na dirhamu: ikiwa atakuwa na amali njema yatachukuliwa apewe Yule alie mdhulumu, na ikiwa hana mema yatachukuliwa maofu ya mwenzake abandikwe yeye) [Imepokewa na Bukhari.]

5. achague katika mali yake mali ya halali ya kuendea hijja au umra Amesema Mtume (saw) ( Hakika Mwenyezi mungu ni Mzuri hakubali ila kizuri) [Imepokewa na Muslim.]

6. Akusudie hijja yake au umra yake Radhi ya Mwenyezi Mungu U na Nyumba ya akhera na kujikurubisha kwake kwa linalo mridhisha Mwenyezi Mungu kutokamana na maneno na vitendo na atahadhari sana kukusudia hija yake mambo yakidunia kama kutaka kusifiwa na kujifakhiri kwa hilo.

7. Na yatakikana kwa mwenye kutaka kwenda hijja au umra kujifunza mambo muhimu yatakao kuifanya hija yake kuwa sahihi, kwa kuuliza asilo lijuwa na kuondosha mushkili, ili afanye ibada yake akiwa mjuzi, na jambo lakusikitisha ni kuwa baadhi ya watu wanaenda hija au umra bila ya kujifunza hukumu zake na kufanya mambo yenye kuharibu hija zao bila kujua.

Miongoni mwa hukumu za ihramu

Aliye kwenye ihramu akisumukwa na nywele tatu anapopangusa kichwa katika kutawadha au kuoga, hilo halimdhuru. Pia lau baadhi ya nywele za masharubu au ndevu zilisumuka au ukucha wake ukakatika, hilo halitamdhuru, isipokuwa akizisumua kwa kusudi. Na mwanamke analingana na mwanamume katika hilo la kutodhurika na kusumukwa na nywele au kucha.

Inafaa kwa aliye kwenye ihramu kufunga uzi mguuni mwake akihitajia hilo au kukiwa na maslahi ya kufanya hivyo.

- Uwekaji masharti katika nia

Ambaye ni mgonjwa, au anaogopea kutokewa na jambo lenye kumzuia kukamilisha ibada yake ya Hijja, ni sunna kwake aweke sharti wakati wa kuhirimia na aseme: «Tunaitikia mwito wako wa Umra (au Hija) iwapo kutatokea kitu chochote chenye kunifunga mimi nisimalize ibada yangu, basi mahali pangu pa kutahalali ni pale uliponifunga».

Aishah t amepokewa akisema kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliingia kwa Dhuba›ah binti Zubair akamwambia: (Huenda ulitaka kuhiji) Aksema: “Najikuta naumwa [ Waj›ah: mgonjwa mwanamke.]”. Akamwambia: (Hiji na ujiwekee sharti na useme ‘ Ewe Mola! Mahali pangu pa kujifungua na ihramu ni pale uliponifunga) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Akisema hivyo, kisha akapatikana na jambo la kumzuia, basi itafaa atahalali (ajifungue na ihramu) bila kulazimiwa na kitu.