Kufunga Swawm Za Sunnah Mwezi Wa Rajab Ambazo Ana Mazoea Nazo Kuzifunga Kama Jumatatu Na Alkhamiys.

SWALI: Asalamu alaykum warahmatullah wabarakatu ALLAH subhana wataala awalipe dunian na akhera kwa kutuelimsha swali langu mimi ni huwa nafunga kila jumatatu na alhamisi vp kuhusu mwezi huu?

JIBU: AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho. Hakuna ubaya kufunga Swawm za Sunnah katika mwezi huu wa Rajab kama ulivyotaja kwa vile ni kawaida yako kufunga Jumatatu na Alkhamiys. Hata kwa ambaye alikuwa na mazoea ya kufunga Swawm za Ayyaamul-Biydhw anaweza kuendeleza Swawm zake mwezi huu. Lilokatazwa ni kuhusisha ‘ibaadah au ‘amali maalumu katika mwezi huu. Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate faida ziyada: Swawm Katika Mwezi Wa Rajab - Kufunga Mwezi Mzima Au Siku Maalumu Ni Sunnah? Na Allaah Anajua zaidi




Vitambulisho: