JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho Hukufafanua kama umekusudia Zakaatul-Fitwr au Zakaah ya Mali inayofika mwaka. Hata hivyo kwa hali zote inafaa kuwapa ndugu zako Zakaah ikiwa hali zao ni wenye kuhitaji. Kufanya hivyo utakuwa umefanya mambo mawili pamoja; utatimiza fardhi yako na pia utatimiza amri ya kuunga ukoo na jamaa. Na sadaka unayoitoa kwa jamaa wenyewe kuhitaji ni bora zaidi kuliko kumpa mtu wa nje hii ni kutokana na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Sadaka zenu kwa jamaa ni sadaka na pia ni kuunga ukoo)) Kwa maelezo zaidi soma Fataawa katika viungo vifuatavyo: Fataawa Za Zakaatul-Fitwr Na Allaah Anajua zaidi