JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kufaa kushika msahafu na kusoma kwayo katika Swalah za Sunnah. Hakika ni kuwa inajuzu kwa Muislamu kushika msahafu na kusoma kwayo akiwa anaswali Swalah za Sunnah bila ya tatizo lolote na hasa ikiwa ni Swalah ya usiku (kama Tahajjud) ambayo inahitajika kuwa ndefu kiasi. Na Allaah Anajua zaidi.