Hukumu za Najisi

18738

 

Maelezo ya Najisi

Najisi kilugha

Uchafu

Najisi kisheria

Uchafu ambao Sheria imeamuru uondolewe

Sampuli ya vitu Najisi

1. Mkojo wa binadamu na choo chake

Kwa Hadithi ya Mbedui aliyekojoa msikitini, Mtume (s.a.w) akamwambia (Hii misikiti haifai ikojolewe au ichafuliwe. Linalopasa ni kutajwa Mwenyezi Mungu, kuswaliwa na kusomwa Qur’ani) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim].

2. Damu ya Hedhi

Kwa ilivyothubutu kuwa Khaulah binti Yasaar alimjia Mtume (s.a.w) akasema: « Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mimi sina isipokuwa nguo moja, na ninaingia hedhini nikiwa nimeivaa. Mtume (s.a.w) akasema: (Ukitwahirika osha pale mahali pa damu kisha uswali ukiwa na hiyo nguo) [Imepokewa na Abu Daud] .

Na damu isiyokuwa ya hedhi ni twahara, iwe ni damu inayotiririka au isiyotiririka, kwa hadithi iliyothubutu kuwa mmoja wa washirikina alimfuma mmoja wa Waislamu kwa mshale naye yuwaswali ukampata, akaushopoa na akaendelea kwenye Swala yake na damu ikimtiririka.
Ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:
Ghuslu - Nifaas Na Hedhi

3. Mkojo na choo cha wanyama wasio liwa

Kwa hadithi iliyosimuliwa na Ibn Mas›uud t kwamba Mtume (SAW) alienda chooni akaniamuru nimletee mawe matatu. Nikapata mawe mawili, nikatafuta la tatu nisipate, nikachukua choo kikavu cha mnyama nikamletea. Akachukua mawe mawili na kile choo akakitupa na akasema “Hiki ni najisi [ Riks: najisi.] ” [ Imepokewa na Bukhari.].

Ni hukmu gani ya Mkojo na choo cha wanyama wanaoliwa ?
Mkojo wa mnyama anayeliwa na choo chake ni twahara, kwa kuwa ilithubutu kutoka kwa Anas bin Malik  kwamba kuna watu walikuja Madina, na hewa yake isiwafae - yaani walishikwa na ugonjwa huko -. Mtume(s.a.w) akawapeleka kwenye ngamia wa Zaka wapate kunywa mikojo na maziwa ya hao ngamia [Imepokewa na Bukhari.].

4. Mfu

Naye ni aliyekufa mwenyewe bila kuchinjwa kisheria, kwa kuwa Mwenyezi Mungu U Aliyetukuka Alisema: {Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa mimi kitu kilicho haramishwa kwa mja kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu au damu inayo mwagika au nyama ya nguruwe kwani hiyo ni uchafu} [6: 145].

Na kinaingia katika maana ya mfu kile kilichokatwa kutoka kwa mnyama aliye hai kabla hajachinjwa.

Na vinavyovuliwa katika mfu ni:

1. Mfu wa Samaki na Parare

Kwa neno lake Mtume (s.a.w): (Tumehalalishiwa mfu aina mbili, na damu aina mbili. Ama aina mbili za mfu, ni samaki na parare, na ama aina mbili za damu, ni ini na wengo) [Imepokewa na Ahmad]

2.Mfu asiye na Damu inayotiririka kama vile Nzi:

Kwa kuwa Mtume (s.a.w) alisema: (Anapoingia nzi kwenye chombo cha mmoja wenu, basi na amzamishe kisha amtoe na kumtupa, kwani kwenye mojawapo ya mabawa yake kuna ponyesho na katika lingine kuna ugonjwa) [ Imepokewa na Bukhari.].

Mfu
Samaki
Parare
Nzi

5. Nyama ya Nguruwe

Kwa kuwa Mwenyezi Mungu U Aliyetukuka Amesema: {Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa mimi kitu kilicho haramishwa kwa mja kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu au damu inayo mwagika au nyama ya nguruwe kwani hiyo ni uchmfu } [6: 145].

Nguruwe

6. Ute wa Mbwa

Mbwa ni najisi yeye mzima. Na unajisi wa ute wake umefanywa mzito, kwa kuwa Mtume (s.a.w) alisema: (Kutwahirika kwa chombo cha mmoja wenu iwapo mbwa amekiramba ni kukiosha mara saba, mara mojawapo kwa mchanga) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim].

Na kuramba ni atiapo mbwa ulimi wake ndani ya chombo na kuutikisa, anywe au asinywe.

Ute wa mbwa

7. Madhii

Nayo ni maji meupe mapesi yenye kunata, yanayotoka wakati wa kucheza na mke au kufikiria kuundama, si kwa matamanio ya nguvu wala hayatoki kwa kasi, na hayafuatiwi na hali ya kulegea, na wakati mwingine mtu hahisi kamwe kuwa yametoka. Hii ni kwa kuwa Mtume (s.a.w) katika hadithi iliyopokelewa na Ali bin Abi Twalib t alipomuuliza mtume s.a.w kuhusu madhii, alisema: (Tawadha na uoshe dhakari yako) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim].

8. Wadii

Nayo ni maji meupe mazito yanayotoka baada ya kukojoa.

twahara wa Manii

Manii: ni maji meupe, mazito, yanayotoka kwa matamanio ya nguvu kwa kasi, na yanafuatiwa na ulegevu, na yana harufu inayofanana na yai lililoharibika.

Nayo ni twahara, kwani lau yangekuwa najisi Mtume (s.a.w) angeamrisha yaoshwe.

Na inatosheleza, katika kuondoa manii, kuyaosha yakiwa majimaji, na kuyakangura yakiwa makavu, kwa hadithi ya Aishah t kuwa alisema: (Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) akiosha manii kisha akitoka kwenda kuswali kwa nguo hiyo na mimi nikiona athari yamuosho katika ile nguo) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Na katika riwaya ya Muslim: (Nilikuwa nikiyakangura manii kwenye nguo ya Mtume (s.a.w) kisha akiswalia) [ Imepokewa na Muslim.].

Kuyaosha yakiwa majimaji
Kuyakangura yakiwa makavu

Njia za Kutwahirisha Najisi

1. Kutwahirisha Ardhi Iliyonajisika

Ardhi ikinajisika, najisi hiyo huondolewa iwe ni kwa maji au kinginecho. Katika hadithi ya mbedui aliyekojoa msikitini, Mtume (s.a.w): (Muwacheni na mwageni kwenye mkojo wake ndoo ya maji) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Na iwapo najisi ni majimaji ya kutiririka kisha ikakauka basi kwa hivyo huwa ishatwahirika kulingana na hadithi ya Abuu Qilaabah t kuwa alisema: “Ardhi ikikauka huwa imetwahirika” [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Najisi majimaji kinachomiminika ardhini
Kutwahirisha Ardhi Iliyonajisika
Kukauka kwa najisi majimaji
Pombe

Pombe ni twahara kinje ingawa kimaana ni najisi na kuwa kulinywa ni miongoni mwa dhambi kubwa, isipokuwa ya kwamba hakuna dalili kuwa ni najisi.

Ama neno lake Mwenyezi Mungu U {Enyi mlio amin!bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya shetani basi jiepusheni navyo } [5: 90]

Lililokusudiwa ni uchafu wa kimaana na sio uchafu wa kidhahiri, kama ilivyo kamari na masanamu. Hukumu inayochukuliwa hapa ni kuwa utumiaji wa mafuta mazuri yenye alkoholi unafaa, kwa kuwa alkoholi inatolewa kwenye pombe.

Pombe

2. Kuyatwahirisha Maji Yaliyonajisika

Yanatwahirika kwa kuongeza maji mengi ndani yake mapaka athari ya najisi iondoke. Pia yanatwahirika kwa kuyasafisha kwa njia za kiteknolojia za kisasa.

Kutwahirisha kwa vitu vya kisasa
Kutwahirisha kwa kuongeza maji

3.Kuitwahirisha Nguo Iliyonajisika

Huoshwa kwa maji, ikangurwe ikamuliwe mpaka Najisi Iondoke

Kutwahirisha nguo iliyonajisika

4.Kuyatwahirisha matandiko

Huoshwa kwa maji au kwa visafishaji vya kisasa, Na hukangurwa mpaka najisi iondoke.

Kutwahirisha matandiko

5. Kuitwahirisha Ngozi ya Mfu

1. Ngozi ya mfu wa mnyama anaeliwa

Hutwahirishwa kwa kuitia rangi kwa kauli yake Mtume (s.a.w): (Ngozi ikitiwa rangi huwa imetwahirika) [ Imepokewa na Muslim.].

Na dibaagh ni kutengeneza ngozi kwa baadhi ya madawa mpaka zilainike na uvundo wake uondoke. Ama mnyama anayeliwa awapo si mfu na akawa amechinjwa kwa njia ya kisheria, basi ngozi yake ni twahara

2. Ngozi ya Mfu wa Mnyama Asieliwa

Kwa Yule mnyama ambae haiwi halali kuchinjwa kwake ngozi yake haitotwahirika kwa kukaushwa hata kama katika uhai wake alikuwa twahara

Mnyama anayeliwa
Kupaka rangi ngozi
Mnyama asiyeliwa

6. Kutwahirisha mkojo wa mtoto wa kike na mkojo wa mtoto wa kiume ambaye hajala chakula

Mkojo wa mtoto wa kike huoshwa. Ama mkojo wa mtoto wa kiume, inatosha kunyunyiza maji juu yake, kwa kauli yake Mtume (s.a.w): (Mkojo wa mtoto wa kike huoshwa, na mkojo wa mtoto wa kiume hunyunyizwa maji) [Imepokewa na Abu Daud.]

Kunyunyiza Maji mkojo wa Mtoto wa Kiume
Kuuosha Mkojo wa Mtoto wa Kike

7. Kukitwahirisha kilichorambwa na Mbwa

Huoshwa mara saba, mara ya kwanza yake ni kwa mchanga, kwa kauli yake Mtume (s.a.w): (Utwahara wa chombo cha mmoja wenu iwapo mbwa amekiramba ni kukiosha mara saba, mara ya kwanza yake ni kwa mchanga) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim].

8. Kuyatwahirisha Madhii na Wadii

Ataosha dhakari yake na atatawadha, kwa kauli yake Mtume (s.a.w) katika hadithi ya Ali bin Abii Twalib: (Tawadha na uoshe dhakari yako) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Ama kuitwahirisha nguo, inatosha kunyunyiza maji mahali palipo na madhii au wadii, kwa hadithi ya Sahl bin Hanif kuwa yeye alimuuliza mtume (s.a.w): “Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nguo yangu ikiiingiwa na chochote katika vitu hivyo itakuwaje?” Akasema: (Inakutosheleza utie maji kwenye kitanga cha mkono uyamimine nguoni mwako mpaka uone kwamba yameviondoa) [ Imepokewa na Abu Daud.].

9. Kutwahirisha Damu ya Hedhi

Ni kuiosha kwa maji. Na haidhuru ikisalia athari yake, kwa kauli yake Mtume (s.a.w): (Yanakutosheleza maji, na athari yake haikudhuru) [Imepokewa na Abu Daud.]

10. Kuvitwahirisha Viatu

Husuguliwa chini mpaka iondoke athari ya najisi, kwa kauli yake Mtume (s.a.w): (Mmoja wenu anapokanyaga uchafu kwa kiatu chake, basi mchanga unakitwahirisha) [ Imepokewa na Abu Daud.].

Kutwahirisha viatu kwa kuvisugua kwenye Ardhi

11. Kuitwahirisha Nguo ndefu ya Mwanamke

Najisi ikipakana na ukingo wa nguo ya mwanamke, basi inamtosheleza yeye atembee mahali twahara na ardhi itaitwahirisha, kwa kauli yake Mtume (s.a.w) (Kitaitwahirisha kilicho baada yake) [ Imepokewa na Abu Daud.].

Kuitwahirisha Ardhi nguo ya mwanamke

12. Kuvitwahirisha Vyakula Vikavu

Vinatwahirika kwa kuiondoa najisi na zile sehemu zilizo pambizoni mwa hivyo vyakula, na kinachosalia kitakuwa twahara, kwa ilivyothubutu kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) aliulizwa kuhusu panya aliyeingia ndani ya samli, akasema: (Vitupeni! Na vile vilivyo pambizoni mwakeviondoeni namule samli yenu). [ Imepokewa na Bukhari.]

Samli iliyoingia Panya Aliyekufa

13- Kutwahirisha Vitu Vigumu kama Viyoo na Gilasi

Itapanguswa mpaka athari ya najisi iondoke.`

Kutwahirisha Ukoa kwa Kuupangusa
Maelezo kuhusu Najisi

1- Asili ya vitu ni twahara isipokuwa vile ambavyo kuna dalili ya unajisi wake.

2- Najisi ikiingia kwenye kitu na isijulikane ilipo, basi chote kitaoshwa.

3- Najisi ikigeuka ikawa kitu kingine, kama vile kikichomwa choo cha punda kikawa jivu, basi itakuwa twahara.

Kugeuka choo kuwa jivu kunakukifanya kitwahirike