Hukumu za kwenda haja

9967

 

Yanayopasa wakati wa kwenda haja

1.Kufunika uchi usionekane na watu wakati wa kwenda haja, kwa neno lake Mtume ﷺ: (Kuweka kizuizi baina ya macho ya majini na uchi wa binadamu angiapo chooni mmoja wenu ni aseme “Bismillah”) [Imepokewa na Tirmidh.].

2.Kujiepusha asiingiwe na najisi nguoni mwake au mwilini mwake, na akiingiwa na najisi yoyote aioshe. Kwa hadithi iliyothubutu kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alipita kwenye kaburi mbili na akasema: (Hawa wawili wanaadhibiwa. Na hawaadhibiwi kwa jambo kubwa. Ama huyu hakuwa akijihifadhi na mkojo) [Imepokewa na Abu Daud].

3.Kujiosha kwa maji au kujipangusa kwa mawe, kwa hadithi ya Anas bin Malik t kuwa alisema: (Mtume ﷺ alikuwa akiingia chooni, na mimi nikimbebea, pamoja na mtoto kama mimi, chombo cha maji na bakora, akachukua maji akajisafishia nayo) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Yanayoharamishwa wakati wa kwenda haja

1.Kuelekea kibla au kukipa mgongo wakati wa kwenda haja jangwani. Ama kwenye majengo, lililo bora zaidi ni kuacha kujilazimisha na hilo, kwa kauli yake Mtume ﷺ: (Mkienda haja kubwa msielekee kibula, na msikipe mgongo kwa kukojoa wala kwa haja kubwa, lakini elekeeni mashariki au magharibi) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

2.Kuingia haja kwenye njia ya watu kupita au kwenye kiuvuli na sehemu za wao kukaa. Mtume ﷺ amesema: (Ogopeni vitu viwili vinavyosababisha mtu kulaniwa. Wakasema: ni vitu gani hivyo ewe mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Ni(kitendo cha) yule anayeingia haja kwenye njia ya watu kupita au kwenye kivuli cha watu kukaa) [Imepokewa na Muslim.].

3.Kuingia na Msahafu chooni, kwa kuwa kitendo hiko kinaonesha dharau kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.

Kuingia chooni kwenye njia inayopitwa na watu
Kukidhi haja jangwani
Kukujoa kwenye maji yaliyotulia
Imethubutu kwamba kukojoa kwenye maji yaliyotulia kunapelekea kupatikana ugonjwa wa Bilharzia ambayo yanatokea yakisababishwa na aina ya vijidudu vinvyopasua mwili na kutoa damu kwenye kibofu cha mkojo,

Yanaopendekezwa wakati wa kwenda haja

1.Kujiepusha na watu wakati wa kwenda haja jangwani

2.Aseme angiapo chooni: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu. Ewe Mwenyezi Mungu! Mimi najilinda kwako kutokana na Mashetani wa kiume na wa kike” [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

3.Kutanguliza mguu wa kushoto angiapo chooni na mguu wa kulia atokapo.

4.Aseme anapotoka “Naomba msamaha wako” [Imepokewa na Abu Daud.].

 

Yanao chukiza kufanya wakati wa kwenda haja

1.Kusema wakati wa kwenda haja (chooni) au kuzungumza na watu isipokuwa kwa haja (dharura), kwa hadithi ya Ibn Umar  kwamba (mtu mmoja alipita kwa Mtume ﷺ naye yuwakojoa, akamsalimia Mtume, asimrudishie salamu) [Imepokewa na Muslim.].

2.Kuingia chooni na kitu chochote chenye utajo wa Mwenyezi Mungu, U isipokuwa akichelea kuwa kitaibwa na mfano wake, kwa kuwa Mtume ﷺ alikuwa akiingia chooni akiiweka pete yake.

3.Kushika tupu kwa mkono wa kulia au kutamba au kupangusa kwa mawe kutumia huo mkono, kwa kauli ya Mtume ﷺ: (Asishike mmoja wenu dhakari (tupu ya mbele) yake kwa mkono wa kulia wake akiwa yuwakojoa wala asijipanguse kwa mkono wake wa kulia baada ya kwenda haja) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

4.Kukojoa kwenye mpasuko na pango ili asidhuriwe na wadudu wanaotembea au adhuriwe na wao.

Kuzungumza wakati wa kukidhi haja
Kuingia chooni pamoja na kitu chenye utajo wa Mwenyezi Mungu
Kukojoa kwenye tundu
Kuingia na mswahafu kwenye choo cha kuoga.
Kukojoa kwa kusimama
Mtume ﷺ alikataza kukojoa kwa kusimama. Lakini akijiaminisha kuwa tatuko za mkojo hazitamfikia inafaa afanye hivyo, kwa hadithi ya Hudhaifah kuwa Mtume ﷺ alikwenda kwenye taka za watu akakojoa kwa kusimama” [Imepokewa na Bukhari.].

Kutamba kwa maji na kwa mawe

Kutamba  ( KUSTANJI )

Kuondoa athari ya chenye kutoka kwenye tupu ya mbele na ya nyuma kwa maji yenye kutwahirisha.

Kutamba kwa mawe

Kuondoa athari ya chenye kutoka kwenye tupu ya mbele au ya nyuma kwa mawe na mfano wake

Hukumu ya kutamba kwa maji na kwa mawe

Kutamba kumewekwa na sheria kwa hadithi ya Anas bin Malik t kwamba yeye alisema: (Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akiingia chooni, na mimi nikibeba, na mvulana mwingine pamoja na mimi, chombo cha maji na bakora, akajisafisha na maji) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Na inafaa kutamba kwa mawe peke yake kwa masharti mawili:

1.Mkojo au choo visipite zaidi ya mahali vinapotoka, vikipita basi itabidii atumie maji.

2.Kutamba kwa mawe kuwe ni kwa kufuta mafuto matatu mpaka kusafishika kwa tupu ya mbele au ya nyuma na iondoke athari ya najisi.

Hekima ya kutamba kwa maji na kwa mawe

1.Kujitwahirisha na kuondoa najisi.

2.Kuwa msafi na kujiepusha na visababisho vya magonjwa

Faida

Haihitajii kutamba kwa kutokwa na upepo.

Kutamba kwa maji ni bora kuliko kufuta kwa mawe, kwa kuwa huko kunatakasa zaidi na kutwahirisha zaidi

Masharti ya kitu kifutio (jiwe au mfanowake)

1.Kiwe twahara. Kwani haifai kwa kitu najisi.

2.Kiwe chafaa kutumiwa, kwani haifai kwa kitu kilicho haramu.

3.Kiwe ni chenye kusafisha mahali pa najisi.

4.Kisiwe ni mfupa au choo.imepokewa na Salman al- Farisi t asema: (Alitukataza Mtume ﷺ kuelekea upande wa kibla kwa kwenda haja kubwa au ndogo, kutamba kwa mkono wa kulia, au kutamba kwa mawe yasofikia matatu na kutamba kwa choo au mfupa).

5.Kisiwe ni kitu kinachoheshimiwa kama chakula au karatasi iliyoandikwa vitu vinavyohishimiwa.

Kutamba kwa mfupa
Kutamba kwa kitambaa
Kutamba kwa chakula
Kutamba kwa hanchifu
Kutamba kwa karatasi inayoheshimika
Kutamba kwa mawe
Kutamba kwa mkono wa kulia

Haifai kutamba kwa mkono wa kulia kwa kauli ya Mtume ﷺ aliyesema: (Na asishike mmoja wenu dhakari yake (tupu ya mbele) kwa mkono wake wa kulia na asijifute choo kwa mkono wake wa kulia) [ Imepokewa na Muslim.].