Hukmu Ya Manyoa Ya Mbwa Anayefugwa Nyumbani

SWALI: Asalamu aleykum. Nimeowa mwanamke waki Irish mwenye tabia ya kuniongelesha kwa ukali na inanifanya mimi kuelekea kumchukia mwaka wa 5 na hali ni the same. Haniamina ilihali mimi ni muaminifu ana wivu kiasi cha kuitilafia shughuri au kazi zangu zakupatia rizki. Pia amefuga mbwa mdogo mwenye manyoya mengi nimewajibika kumsafisha kumuosha kumfundisha tabia kuto kunya na kukojoa ndani kuto panda kwenye viti au kitandani na kuto rukiarukia watu nime fauru bali yeye hupenda kumbeba hatimaye manyoya hutapakaa nyumba nzima. Nifanye nini ili niedelee kuwa muisilamu? Maasalam.

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu ufugaji wa mbwa majumbani. Hata hivyo, kabla ya kuingilia suala hilo ni muhimu ufahamu kuwa Muislamu anafaa aoe Muislamu ambaye wana ada, tabia na khulqa moja kwa kuwa mambo yao wameyaegemeza katika kufuata Qur-aan na Sunnah. Sijui huyu Muairish ni Muislamu au bado ni Mkristo au hana Dini au mshirikina. Ikiwa ni Muislamu basi huenda mwanzo ni wewe kumfundisha tabia za Kiislamu ili aweze kuishi nawe Kiislamu. Ikiwa ni Mkristo mbali na kuwa tumeruhusiwa ni lazima awe atatimiza masharti ya wewe kukubaliwa kumuoa na kulingana na maelezo yako ni kuwa bado kutekeleza hayo. Ama akiwa ni mshirikina au hana Dini basi umekatazwa na Uislamu kumuoa kabisa na hata ikiwa mmeoana basi hakuna ndoa nanyi mtakuwa mnazini tu. Tukija katika mas-ala ya kufuga mbwa nyumbani kwetu Uislamu umetukataza isipokuwa tu ikiwa mmemfuga nje ya nyumba kwa ajili ya kuwinda au ulinzi wa nyumba. Ikiwa ni kwa ajili hiyo shari’ah imekubali kumfuga huko na kuhakikisha kuwa umemtekelezea haki zake zote kama kumpatia chakula, maji, kumsafisha na kumpeleka kwa daktari akiwa mgonjwa. Ama kuhusu manyoa ya mbwa kwa mujibu wa Maulamaa wengi wanaona kuwa yakiwa makavu si najisi bali yanapokuwa na maji au unyevunyevu ndio huwa ni najisi. Lakini kwa mujibu wa baadhi ya Maulamaa wanaona hakuna dalili ya hilo na hivyo manyioa ya mbwa yawe makavu au yenye majimaji, basi hakuna unajisi. Unajisi uliotajwa ni mate yake. Hata hivyo, manyoa hayo yanaondoa unadhifu wa nyumba yakiwa yatatapakaa kote nyumbani. Unajisi wa mbwa ni zile sehemu ambazo zina unyevunyevu kama pua na mdomo. Na lau atanusa kitu au ataramba/atalamba itabidi kukitwaharisha hiko kitu ukioshe mara saba – sita kwa maji na mara moja kwa mchanga. Na ikiwa mbwa huyo atakuwa huru anazunguka katika nyumba atakavyo, basi hapo kutakuwa na matatizo ya kupatikana hayo yasiyofaa kama kulambwa vitu, kunuswa na mengineyo. Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi: Mbwa Wa Kufuga Je, Ni Najsi? Jinsi Ya Kuondosha Najisi Ya Mbwa Kwenye Nguo Na Allaah Anajua zaidi




Vitambulisho: