Hukmu Ya Kupunguza Swalaah Ya Safari Na Kufafanisha Na Kafara Ya Kiapo

SWALI: Assalam Alaykum! Nilikua nasoma kitabu cha usuli Fiqh "Bidaayatul mujtahid wa nihaayatul muqtasid cha Ibn Rushd". Katika kipengele cha hukumu ya kupunguza katika Salaatu safar, baadhi ya wazuoni wamesema "ni wajibu ulio khiyarishwa kwa msafiri kama ilivyo kafara ya 'yamini' (i.e waajibun mukhayyarun lahu ka kafaaratul'yamiini) sasa hii kafara ya yamini ndio ipi? Ahsante!

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani kwa swali lako kuhusu kafara ya yamini. Kafara ya yamini ni kama Alivyosema Allaah Aliyetukuka katika Qur-aan: 1. Kulisha masikini kumi. 2. Au kuwavisha hao masikini kumi. 3. Au kuacha mtumwa huru. 4. Mwenye kutopata basi afunge siku tatu Rejea Suratul Maaidah [5]: 89. Kwa mujibu wa makusudio ya muandishi kama ulivyoandika, basi yatakuwa makusudio ni; kama vile msafiri alivyokhiyarishwa kuswali Swalaah kamili au kupunguza na mwenye kula yamini aweza kuchagua jinsi ya kufanya kafara yake. Na Allaah Anajua zaidi




Vitambulisho: