Hedhi, inayofanana na hedhi na nifasi

26327

 

Hedhi

Maana ya hedhi

Hedhi kilugha

Ni kitu kutiririka na kupita

Hedhi kisheria

Ni damu inayotoka kwenye uzao wa mwanamke katika muda maalumu bila yasababu

Namna ya damu ya hedhi ilivyo

Ni nyeusi kama kwamba imechomeka kwa weusi wake mwingi, yaumiza, ina harufu mbaya, mwanamke akiwa nayo huhisi joto lingi

Miaka ya hedhi

Hakuna miaka maalumu ya kuanzia hedhi, kwani inatafautiana kulingana na tabia ya mwanamke, na mazingira yake na hewa yake, wakati wowote mwanamke aonapo damu ya hedhi, basi yeye ameingia hedhini

Muda wa hedhi

Hedhi haina muda maalumu. Miongoni mwa wanawake kuna anayeingia hedhini kwa muda wa siku tatu, na miongoni mwa wanawake kuna anayeingia hedhini siku nne. Na muda wa hedhi kwa wanawake wengi ni siku sita au saba, kwa neno lake Mtume ﷺ kumwambia Hamnah binti Jahsh, na alikuwa akiingia hedhini kwa siku nyingi: (Zingatia kile kinachokutoka, kwa siku sita au saba, kuwa ni hedhi, ujuzi wa kikamilifu uko kwa Mwenyezi Mungu, kisha oga) [ Imepokewa na Abu Daud.].

Maelezo

1. Asili ni kuwa mwenye mimba hapati hedhi, basi aonapo damu kabla ya kuzaa kwa muda mchache na ukafuatiwa na uchungu wa kuzaa, basi hiyo ni damu ya nifasi. Na ikitofuatana na uchungu wa kuzaa, au ikawa kabla ya kuzaa kwa muda mrefu, basi hiyo ni damu ya hedhi.

2. Ikitangulia au ikachelewa hedhi na wakati wake wa kawaida kwa mwanamke, kama wakati wake uwe ni mwanzo wa mwezi aione mwisho wake, au muda wake wa kawaida ukazidi au ukapungua, kwa mfano: iwe ada yake ni siku sita zikazidi zikawa saba. Basi na asijishughulishe na hilo, kwani popote aonapo damu, hiyo ni hedhi, na popote aonapo kuwa ametwahirika basi huo ni utwahara.

3. unajulikana kutwahirika kwa mwanamke, kwa kutokwa na Qassatul baydhaa nayo ni mtiririko mweupe unaotoka hedhi inapo simama, isipotoka, alama ya kutwahirika kwake ni kule kukauka, kwa kuweka pamba nyeupe kwa tupu yake na kisitoke chochote

Miongoni mwa hukumu za hedhi

1. Hukumu ya uvindu na umanjano

Maana ya uvindu na umanjano
Al-sufrah:

umanjano ni damu inayotoka kwa mwanamke.

Al-kudrah:

ni damu iliyochafuka iliyo baina ya umanjano na weusi

Hukumu ya uvindu na umanjano

Mwanamke akiona damu ya manjano au iliyochanganyika baina ya umanjano na weusi, au akaona umajimaji tu, huwa ni moja ya hali mbili:

1. Ima aione wakati wa hedhi au imeungana na hedhi kabla ya utwahara:

Katika hali hii itapewa hukumu ya hedhi, kwa hadithi ya Aishah t kwamba wanawake walikuwa wakimtumia kibakuli ambacho ndani yake kuna pamba yenye dowa rangi ya manjano, na yeye akiwambia: « musifanye haraka mpaka muone paku leupe” akikusudia kwa hilo kutwahirika na hedhi

2. Ima aione wakati wa twahara:

Katika hali hii huwa haizingatiwi kuwa ni kitu chochote, na haimpasi udhu wala kuoga, kwa hadithi ya Ummu ‹Atiyyah kwamba alisema: “Hatukuwa tukiizingatia damu iliyochafuka au iliyo manjano baada ya kujitwahirisha kuwa ni chochote) [ Imepokewa na Abu Daud.].

Alama ya kutwahirika
Namna ya umanjano
Namna ya mvurunduko

2. Hukumu ya kukatika katika kwa hedhi:

Mwanamke aonapo damu siku moja na kukatika siku moja na mfano wake, basi yeye ni mojawapo wa hali mbili

1. Hali hiyo iendelee na yeye kila wakati:

Basi hiyo ni damu ya istihadhah

2. Iwe yakatikakatika:

Kwa namna ya kwamba ikawa yamjia wakati mwingine na atwahirika wakati mwingine. Basi hukumu yake ni kama ifuatayo:

a. Kukatika damu kukipungua kwa siku moja, basi kipindi hiko kitahesabiwa kuwa ni katika kipindi cha hedhi.

b. Na akioona katika kipindi cha utwahara dalili za damu, kama kuona paku leupe, basi kipindi hiki ni cha utwahara, liwe ni dogo au kubwa, au liwe chini ya siku moja au zaidi.

Damu ya istihadhah

Maana ya istihadhah

Istihadhah

Ni kutiririka damu kutoka kwenye tupu ya mwanamke ikawa haikomi kabisa au ikatike kwa kipindi kichache.

Tofauti baina ya damu ya hedhi na ya istihadhah

Damu ya istihadhah Damu ya hedhi
Nyekundu nyepesi Nyeusi nzito
Haina harufu  Ina harufu mbaya yenye kuchukiza
Inaganda (inashikana) Haigandi (haishikani)
Inatoka kwenye kishipa cha uzao cha karibu Inatoka mwisho wa uzao
Damu ya kuashiria kasoro, ugonjwa na uharibikaji Damu ya afya na ya kawaida
Haina wakati maalumu Inatoka wakati maalumu

Hali za ailye kwenye istihadhah

Hali ya kwanza: awe na ada inayojulikana ya siku zake za hedhi kabla ya kujiwa na istihadhah:

Huyo atahesabu siku za kadiri ya ada yake kuwa ni hedhi na zinazosalia katika mwezi ni istihadhah, kwa hadithi ya ‘Aishah t kwamba Fatimah binti Abi Hubaish t alisema: (Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mimi sitwahiriki, je niache kuswali? Mtume akamwambia “La, hiko ni kishipa. Lakini acha kuswali kadiri ya siku zako za kuingia hedhini, kisha oga na uswali”) [ Imepokewa na Bukhari.].

Hali ya pili: Asiwe na ada inayojulikana, lakini anaweza kupambanua baina ya damu ya hedhi na damu ya istuhadhah:

Basi huyu atatumia upambanuzi wake, kwa ilivyothubutu kwamba Fatimah binti Hubaish t alikuwa kwenye damu ya istihadha, Mtume akamwambia: (Ikiwa ni damu ya hedhi, basi hiyo ni damu nyeusi inayojulikana. ikija, acha kuswali, na ikija ile nyingine tawadha na uswali, kwani damu hiyo ni kishipa) [ Imepokewa na Abu Daud.].

Hali ya tatu: Asiwe na ada maalumu na asiweze kupambanua:

Basi huyo atatumia ada za wengi wa wanawake, hivyo basi hedhi itakuwa ni siku sita au saba katika kila mwezi, ataanzia mwanzo wa kipindi anapoona damu, na siku zilizosalia zitahesabiwa ni istihadha. Hii ni kwa kauli yake Mtume ﷺ kumwambia Hamnah binti Jahsh t: (Basi hesabu kuwa wewe uko hedhini kwa siku sita au siku saba, uhakika unajulikana na Mwenyezi Mungu, mpaka ukiona kuwa umetwahirika na umetakasika, swali kwa masiku ishirini na tatu au masiku ishirini na nne na michana yake, na ufunge, kwani hilo linakutosheleza. Na ufanye hivyo katika kila mwezi, kama wanavyohidhi wanawake na kama wanavyotwahirika wanawake wengine, kulingana na nyakati zao za hedhi na utwahara) [ Imepokewa na Abu Daud.]

Hali ya nne: Awe na ada maalumu na aweze kupambanua:

Huyu atazingatia ada na siyo kupambanua, kwa kuwa ada ina udhibiti zaidi kwa mwanamke. Na anaposahau ada yake basi atatumia upambanuzi.

Maelezo

1. Iwapo mwanamke anajua wakati wa hedhi yake, lakini akawa amesahau idadi ya siku zake za hedhi, basi atashika hesabu ya ada ya wengi wa wanawake.

2. Iwapo mwanamke anajua idadi ya siku zake za hedhi, lakini akawa amesahau wakati wa hedhi yake, iwapo ni mwanzo wa mwezi au ni mwisho wake, atahesabu mwanzo wa mwezi idadi ya siku zake za hedhi. Akisema kuwa yamjia mwanzo wa mwezi lakini hawezi kujuwa ni lini wakati wake, atashika hesabu kuanzia mwanzo wa nusu idadi ya siku ilipokuwa hedhi yake ikimjia, kwa kuwa nusu ya mwezi ndio kadiri iliyo karibu zaidi ya kudhibiti wakati wake.

3. Kikipita kipindi cha hedhi, na mwanamke yuko kwenye istihadhah basi ataoga kisha atafunga kitambaa kwenye tupu yake. Na hukumu yake itakuwa ni ile ya twahara, ataswali na atafunga, na haitamdhuru damu itakayomtoka baada ya kutawadha kwa kuwa ana udhuru, na atafanya mojawapo ya mambo matatu katika twahara:

a. Atawadhe kwa kila Swala baada ya wakati kuingia. Hilo ni baada ya kuosha tupu yake na kuifunga kitambaa, kwa kauli ya Mtume ﷺ kumwambia Fatimah binti Hubaish t: (Kisha tawadha kwa kila Swala na uswali) [ Imepokewa na Abu Daud.].

b. Aicheleweshe Adhuhuri mpaka kabla ya Alasiri, kisha aoge na aswali Adhuhuri na Alasiri, na atafanya hivi katika Swala nyingine. Hii ni kwa neno lake Mtume ﷺ kumwambia Hamnah binti Jahsh t: (Na ukiweza kuchelewesha Adhuhuri na kuitanguliza Alasiri, ukaoga na ukakusanya baina ya Swala mbili: Adhuhuri na Alasiri, na ukachelewesha Magharibi na akaianguliza Swala ya Isha, kisha uoge na ukusanye Swala mbili, basi fanya hivyo. Na ukiweza kuoga wakati wa wa swala ya Alfajiri basi fanya hivyo, na ufunge, kama waeza kufunga) [ Imepokewa na Abu Daud.].

4. Mwanamke akitokwa na damu kwa sababu yoyote ile, kama operesheni, na ikatiririka, basi yeye ni mojawapo wa hali mbili:

a. Ijulikane kuwa hatapata hedhi. Huyu hazipitishwi kwake hukumu za istihadhah, wala haachi kuswali wakati wowote, na ile damu ni ya ugonjwa na kuharibika kwa kitu, na atatawadha kwa kila Swala.

b. Ijulikane kuwa yeye inamkinika kuingia hedhini. Huyu hukumu yake ni ya istihadhah.

5. nafaa kumuingilia mwanamke aliye kwenye istihadhah.kwa kuwa Sheria haikumkataza.

Nifasi

Maana ya Nifasi

Nifasi

Ni damu inayotoka kwenye uzao wa mwanamke kwa sababu ya kuzaa

Muda wa Nifasi

Hakuna mpaka wa uchache wa nifasi. Ama wingi wake kwa kawaida ya wengi ni siku arubaini, isipokuwa akiona utwahara kabla ya hapo, Basi ataoga na aswali.
Ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:
Ghuslu - Muda Wa Kutwaharika Na Damu Ya Nifasi

Miongoni mwa hukumu za nifasi

1. Mwanamke akizaa na asione damu- na hii ni hali ya nadra sana- atatawadha na ataswali, na halazimiki kuoga.

2. Damu ikipita siku arubaini, na ikawa ada yake ni kukatika kwa kumalizika siku ya arubaini, au zikadhihiri alama za kukaribia kukatika, atangojea mpaka ikatike. Iwapo damu itaendelea, basi yeye ana istihadhah na itamthibitikia yeye hukumu za istihadhah.

3. Akitwahirika kabla ya siku ya arubaini, kisha damu ikamrudia ndani ya siku arubaini itamlazimu aangalie: .

a. Akijua kuwa ni damu ya nifasi, basi ni damu ya nifasi.

b. Na akijua kuwa si damu ya nifasi, basi hukumu yake ni kuwa yuko katika twahara.

4. Haithubutu damu kuwa ni ya nifasi isipokuwa akiwa amezaa kitu chenye umbo la binadamu, akiwa amezaa tisha- naye ni mtoto aliyetoka kwenye uzao wa mwanamke kabla ya umbo lake kukamilika- ambalo halijafafanuka kwake umbile la binadamu. Nalo lina hali tatu:

a. Iwe ni kabla ya siku arubaini za kwanza (za kushika mimba). Bila ya hivyo, hii itakuwa ni damu iliyoharibika, hivyo basi ataswali na atafunga.

b. Iwe ni baada ya siku thamanini. Na hii ni damu ya nifasi.

c. Iwe muda wake wa kukaa matumboni ni baina ya siku arubaini na thamanini. Na hii itatazamwa: Iwapo imeonesha alama ya kuwa ni kiumbe, basi hiyo ni damu ya nifasi. ikitokuwa hivyo, basi ni damu iliyoharibika

Yanayoharamishwa kwa ajili ya hedhi na nifasi

1. Kujamiana

Kwa neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie, huo ni uchafu basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi.wala msiwaingilie mpaka watahirike. Wakisha twahirika basi waendeni alivyo kuamrisheni mwenyezi mugnu.} [2: 222]

Na kwa kauli ya Mtume ﷺ ilipoteremka aya hii: (Fanyeni kila kitu isipokuwa kuundama) [ Imepokewa na Muslim.].

Maelezo

1. Mwenye kumuingilia mkewe na hali yuko katika hedhi hupata dhambi na itamlazimu kafara na huyo mke pia atoe kafara iwapo aliridhia.

Na kafara ni kutoa sadaka kadiri ya dinari moja au nusu dinari ya dhahabu, kwa hadithi ya Ibnu Abbas kumpokea Mtume ﷺ juu ya mtu anayemuingilia mkewe na hali yuko kwenye hedhi kuwa alisema: (Atatoa sadaka Dinari moja au nusu dinari) [ Imepokewa na Muslim.].

Dinari moja ni grama nne na robo za dhahabu.

2. Aliyoko hedhini akiingia twaharani, haifai kwa mumewe kumuundama (kumuingilia) mpaka aoge, kwa neno la Mwenyezi Mungu Aliyetukuka {Na msiwakaribie mpaka watwahirike} yaani: kutokana na damu.

Kisha akasema: {wakijitwahirisha} yaani: wakaoga.

Kisha akasema {Wajieni kupitia pale alipowaamrisha nyinyi Mwenyezi Mungu} [2: 222], yaani: kuundama.

2.Kuswali

Kwa neno lake Mtume ﷺ: (Ikija hedhi acha kuswali, na ikiondoka Safisha damu kwa kuoga kisha uswali) [ Imepokewa na Abu Daud.].

Maelezo

1. Mwanamke haimlazimu kulipa swala akitwahirika, Kwa hadithi iliyothubutu kutoka kwa ‹Aishaah t kuwa aliulizwa juu ya aliyekuwa na hedhi kulipa Saumu na kutolipa Swala, akasema: (Tulikuwa tukipatikana na hilo tukiamrishwa kulipa saumu na hatukuwa tukiamrishwa kulipa Swala) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

2. Iwapo mwenye hedhi atawahi rakaa nzima ya wakati wa Swala, itamlazimu aswali, iwe ni rakaa ya mwanzo ya wakati au ya mwisho wake. Ikiwa atawahi sehemu ya wakati ambayo haikundukii rakaa moja, basi haimlazimu kuswali, kwa kauli ya Mtume ﷺ: (Mwenye kuwahi rakaa moja ya Swala amewahi swala) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

3. Kufunga Saumu

Kwa kauli yake Mtume ﷺ: (Kwani akiingia katika hedhi si ataacha kuswali na kufunga? Wakasema (wanawake): “Ndiyo”) [ Imepokewa na Bukhari.].

Maelezo

Akitwahirika mwenye hedhi kabla ya Alfajiri na akafunga, basi Saumu yake itakuwa sahihi, ingawa hakuoga mpaka baada ya Alfajiri

4. Kushika Msahafu

Kwaneno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Hawaigusi isipokuwa walitwahirishwa} [56: 79]

Na kwa neno lake Mtume (Hawagusi Mswahafu ila aliye twahara) [ Imepokewa na Malik katika Muwatta’].

5. Kutufu Alkaaba

Kwa neno la Mtume ﷺ kumwambia ‹Aishah t: (Fanya kile anachokifanya mwenye kuhiji isipokuwa usitufu Alkaaba mpaka uwe twahara) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

na kwa haditi ya Ibn ‘Abbas t alisema: (Wameamrishwa watu iwe mwisho wa kukutana kwao na Alkaaba ni kutufu, isipokuwa mwanamke mwenye hedhi amehafifishiwa hilo) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

6. Kukaa msikitini isipokuwa mpita njia

Kwa neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Enyi mlioamini! Msikaribie swala hali mmelewa, mpaka myajue mnayo yasema, wala hali mna janaba isipo kuwa mmo safarini mpaka muoge} [4: 43]

na kwa neno la Mtume ﷺ (Mimi simhalalishii msikiti mwenye hedhi wala mwenye janaba)

Maelezo

1. Si makosa kwa mwenye hedhi kupita msikitini akijihifadhi na asichelee kuuchafua msikiti, kwa ujumla wa maneno ya Mwenyezi Mungu Aliyetuka: {Isipokuwa wapita njia} [4: 43]

2. Ni haramu kwa mwenye hedhi kukaa kwenye eneo la kuswalia Idi, kwa neno lake Mtume ﷺ (Na wajiepushe na kuhudhuria mahali pa kuswali Idi) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

7.Talaka

Ni haramu kwa mume kumuacha mkewe akiwa na hedhi, kwa neno lake mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Ewe Nabii mkiwataliki wanawake, watalikini mkizingatia eda lao } [65: 1].

Yaani waelekee kwenye eda maalumu wakati wa kuachwa.

Na talaka ya mwenye hedhi inapita ingawa ni haramu na ni uzushi katika Dini.
Ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:
Ghuslu - Vipi Kukoga Janabah, Nifaas Na Hedhi