Haifai Kufunga Swawm Ayyamut-Tashriyq (Masiku ya 11-13 Dhul-Hijjah)

SWALI: je haifai kufunga yaumul baidh katika mwezi wa dul-hijja na kadhalika sunna ya ijumatatuna alhamisi kwa sababu nilivyo soma katika nasiha za ijumaa, nimefaham ni kwa ajili ya mahujaji tu sio kwa watu waliokua katika mchi zao.

JIBU: AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho. Swiyaam masiku hayo ya Ayaamul Biydhw (terehe 13, 14, 15 za Kalenda Ya Kiislamu) haitowezekana kwani siku ya kwanza ya Ayaamul-Biydhw inaanza tarehe 13 Dhul-Hijjah ambayo ni miongoni mwa siku za Ayaamut-Tashriyq (tarehe 11, 12, 13 Dhul-Hijjah). Inakatazwa kufunga kwa sababu hizi ni siku za kusherehekea na kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa wingi. Makatazo haya ni kwa walio Hajj na wasio vilevile. Dalili ni Hadiyth ifuatayo: عن أبي هريرة رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَعَثَ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ حُذَافَةَ يَطُوفُ فِي مِنًى أَنْ: ((لَا تَصُومُوا هَذِهِ الْأَيَّامَ فَإِنَّهَا أَيَّامُ أَكْلٍ وَشُرْبٍ وَذِكْرِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ)) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam) alimtuma 'Abdullaah bin Hudhaafah azunguke Minaa na atangaze: ((Msifunge siku hizi, kwani hizi ni siku za kula na kunywa na kumdhukuru Allaah Aliyetukuka Jalali)) [Ahmad] Hizo ndizo siku zilizotajwa kwa ajili ya kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kama Anavyosema: وَاذْكُرُوا اللَّـهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ ۚ Na mdhukuruni Allaah katika siku za kuhesabika. [Al-Baqarah: 203] Kwa hiyo haifai kufunga swiyaam katika siku hizi hata kama mtu alikuwa na ada ya kufunga Sunnah za Jumatatu na Alkhamiys au Ayyaamul-Biydhw. Lakini anaweza mtu kufunga tarehe 14, 15 na 16 kupata fadhila za kufunga siku tatu kwa mwezi, bonyeza kiungo kifuatacho upate faida: Hukmu Ya Kufunga Swiyaam Tarehe 13 Dhul-Hijjah Kwa Niyyah Ya Swiyaam Ayyaamull-Biydwh (Masiku Meupe) Na Allaah Anajua zaidi




Vitambulisho: