Ni kitu kinachomlazimu mwnye kuhiji au mwenye kufanya Umra kwa sababu ya kuacha tendo la wajibu au kufanya tendo lililokatazwa
Ni kitu kinachomlazimu mwnye kuhiji au mwenye kufanya Umra kwa sababu ya kuacha tendo la wajibu au kufanya tendo lililokatazwa
Mwenye kuacha wajibu miongoni mwa wajibu za Hija au Umra, kama aliyeacha kulala Muzdalifa au kunyoa au nyinginezo, itamlazimu fidia, nayo ni kuchinja mnyama.
Na mnyama anayekusudiwa ni fungu moja kati ya mafungu saba ya ngamia au ng›ombe au ni mbuzi aliyemaliza mwaka mmoja au kondoo aliyepita miezi sita. Atachinja katika Haramu ya Makka na nyama yake atagawia mafukara wa Makka.
Akikosa mnyama wa kuchinja, atafunga siku kumi: siku tatu akiwa Hija ikiwezekana, na siku saba arudipo kwa watu wake. Mwenyezi Mungu U Anasema: {Asiyepata (cha kuchinja) atafunga siku tatu huko Hija na siku saba mtakaporudi. Hizo siku kumi kamili. Hukumu hiyo ni kwa yule watu wake si wakazi wa eneo la Msikiti wa Haram. Na mcheni Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kutesa} [2: 196].
Mwenye kufanya mojawapo ya matendo haya atachaguzwa baina ya mambo matatu:
a. Kufunga siku tatu.
b. Kuwalisha masikini sita, kila masikini nusu ya pishi ya chakula kama mchele na mfano wake.
c. Kuchinja mbuzi.
Dalili ni neno la Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Na msinyoe vichwa vyenu mpaka wanyama waliotunukiwa kwa ibada ya Hija wafike mahali pa kuchinjwa. Basi mtu atakayekuwa mgonjwa, au ana vitu vya kumkera kichwani mwake, atatoa fidia ya kufunga, kutoa sadaka au kuchinja} [2: 196].
Na neno la Mtume (saw) kumwambia Ka’b bin ‘Ujrah t na yeye yuko kwenye ihramu: (Je, hao niwadudu wa kichwani mwako?). Akasema: “Ndio”. Mtume (saw) akamwambia: (Nyoa kichwa chako kisha uchinje mbuzi ikiwa ni ibada au funga siku tatu au lisha masikini sita pishi tatu za tende).
Mwenye kufanya katazo miongoni mwa makatazo matano yaliyotajwa kwa kukusudia, au akahitaji kulifanya na akalifanya, kama ilivyotokea kwa Ka’b t, basi atatoa fidia ya kero.
Na mwenye kufanya lolote miongoni mwa haya yaliyokatazwa kwa kusahau, basi hana makosa
Hii fidia yake ni kama ile ya kero iliyotangulia
Nayo ni kuchinja ngamia [ Ngamia]. Akikosa atafunga siku tatu katika Hija na siku saba anaporudi kwa watu wake, na hija yake itakuwa imeharibika, na itamlazimu aikamilishe na ailipe mwaka unaokuja.
Nayo ni mbuzi au kondoo, na Umra yake itakuwa imeharibika. Na itamlazimu ailipe.
Kikiwa kiwindwa kina mfano, Aliyewinda atachaguzwa baina ya kutoa mfano, au kukitia kima (thamani) na kununua kwa kima hicho chakula na kukigawanya kwa mifuto (vibaba): kila masikini mifuto miwili [Almuddani: Nusu ya pishi nikipimo 1020 grm], au afunge kwa kila mifuto miwili siku moja.
Makusudio ya kiwindwa ni kile chenye mfano. Yaani: kuna mnyama mwenye kufanana nacho kiasi fulani, na sio kufanana kikamilifu, kwani kufanana namna hiyo haimkiniki.
Mfano wa hilo: Lau mtu aliwinda mbuni, basi itampasa achinje ngamia mmoja, sababu mbuni anafanana na ngamia, au amtie thamani ngamia na anunue kwa thamani yake chakula kama vile mchele au mahindi, na amlishe kila masikini mifuto miwili ya hiko chakula, au afunge kwa kila mifuto miwili siku moja. Na lau aliwinda pundamilia, basi itamlazimu ng’ombe na namna hiyo.
Na iwapo kiwindwa hakina mfano miongoni mwa wanyama hoa, kama vile nzige na kisigi (ndege mdogo), basi atapewa hiari baina ya kununua chakula kwa thamani ya kile kiwindwa na kuwalisha masikini au afunge kwa kila mifuto miwili siku moja. Na wenye kukitia thamani ni watu wawili waadilifu.
Haifai kufungisha ndoa kwa mwenye kuhiji na mwenye kufanya umra wala hana fidiya mwenye kufanya hivyo
Ni wanyama hoa wanaotunukiwa sehemu takatifu kwa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, au ilio wajibishwa kwa sababu ya Tamattu’au Qiraan au kufungizika
Anayechanganya Hija na Umra kwa njia ya Tamattu› au Qiraan itamlazimu achinje mnyama wa tunuku: naye ni mbuzi au fungu moja la mafungu saba ya ngamia au ng›ombe. Akikosa mnyama atafunga siku kumi: siku tatu ziwe katika Hija na siku saba ziwe baada ya mwenye kuhiji kurudi kwa watu wake. Hili humlazimu Yule ambaye si mkazi wa Makka, iwapo ni miongoni mwa wakazi wa Makka, hatalazimika kuchinja mnyama wa kutunuku wala kufunga, kwa neno la Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Mwenye kujistarehesha kwa Umra mpaka Hija, basi itamlazimu achinje mnyama wa kutunuku aliye sahali kwake, na asipopata atafunga siku tatu katika Hija na saba mtakaporudi. Hizo ni kumi kamili. Hukumu hiyo inamhusu yule ambaye watu wake wa nyumbani si wakazi wa maeneo ya Msikiti wa Haram} [2: 196].
Naye ni mnyama ambaye mwenye kuhiji tu au anayefanya Umra ya kujitolea anamtunuku, au yule ambaye mwenye kufanya Hija ya Qiraan au ya Tamattu› anamtunuku ikiwa ni zaidi ya wajibu, au ni mnyama ambye hutunukiwa Makka na mtu ambaye hako kwenye ihramu kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.
Mnyama anayetunukiwa kwa kujitolea na yule wa Hija ya Tamattu’ au Qiraan, inafaa kwa yule anayemtoa kula kitu katika nyama yake, bali ni sunna kufanya hivyo. Hii ni kuambatana na kitendo cha Mtume (saw) kwa kuwa (Aliamrisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)katika kila mnyama aliyemtoa kuchinjwa, apatiwe sehemu [Imepokewa na Bukhari.]. Basi ikapikwa na akanywa supu yake) [Imepokewa na Tirmidhi].
Ihswaar: Ni kuzuiliwa kutimiza Hija au Umra au yote mawili. Mwenye kuhirimia Hija au Umra, akazuiliwa na adui kuifikia Alkaba, au akatukiwa na jambo likamfanya asiweze kufika kwenye Alkaba, basi atachinja mnyama mahali alipo, kisha atajitoa kwenye vikwazo vya ihramu, kwa neno la Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Basi mkizuilika kuendelea na ibada ya Hija au Umra, chinjeni kilichokuwa sahali} [2: 196].
Na wanyama wa kuchinjwa kwa sababu ya kuzuilika ni mbuzi/kondoo au fungu moja kati ya mafungu saba ya ngamia au ng’ombe.
Tunuku ya Hija ya Tamatta’ au Qiraan au ya kujitolea, huchinjwa ndani ya mipaka ya Haram na hugawiwa masikini wake. Iwapo atachinja nje ya mipaka ya Haram haitomtosheleza.
Na mnyama wa tunuku kwa sababu ya kuzuiliwa atamchinja mahali alipozuilika.
1. Tunuku ya Hijja ya Tamattu’, Qiraan na ya kujitolea
Wakati wake unaanza baada ya Swala ya Idd ya siku ya Idd ya kuchinja mpaka jua la siku ya mwisho ya siku za Tashriiq kuzama, nayo ni siku ya 13.
2. Tunuku ya kuzuilika
Wakati wake ni pale kizuizi kinapotokea
Inafaa kwa mwenye kuhiji kumuwakilisha mtu wa kumchinjia ikiwa Hijja yake ni ya Qiraan au Tamattu› na akiwa aliyewakilishwa ni mwaminifu. Na lililo bora ni kuwa mwenye kuhiji afanye mwenyewe kwa kuwa Mtume( SAW) ndivyo alivyofanya.
Fidia haitoshelezi iwe ni badala ya kudhahi, kwa kuwa fidia ni ya kuchanganya Hija na Umra, ama kudhahi ni sunna ya anayehiji na asiyehiji.