Ni kujizuia na kujiepusha kufanya jambo fulani.
Ni kujizuia na kujiepusha kufanya jambo fulani.
Ni kufanya ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu U kwa kujizuia kula, kunywa na kufanya tendo la ndoa kuanzia kutokeza kwa alfajiri hadi kutwa kwa Jua.
Asema Mwenyezi Mungu { Enyi mlo Amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andkikwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kucha mungu.(Mfunge) siku maalumu za kuhisabika.na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimiza hisabu katika siku nyingine. Na wale wasio weza watoe fidiya kwa kumlisha masikini na atakaye fanya wema kwa kujitolea, Basi ni bora kwake na Mkifunga ni bora kwenu kama mnajua.} (Al-Baqarah- Aya 183: 185)
Saumu ina fadhila kubwa sana, na thawabu nyingi mno tena maradufu, na kwa hakika Mwenyezi Mungu ameinasibisha saumu kwake yeye kwa ajili ya kuipa utukufu na kuitukuza. Katika Hadithi Al-Qudsy iliyopokewa na swahaba Abu Hurayrah, t Anasema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): “kila tendo la mwanadamu huongezwa malipo ya wema wake mara kumi ya mfano wa jema hilo alilolitenda mpaka hufikia kuongezwa (huku kwa malipo ya wema huo) hadi nyogeza mara sabiini. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Isipokuwa saumu, kwani hiyo saumu ni yangu mimi, na mimi ndiye mwenye kutoa malipo yake; (mja wangu) anaacha matamanio yake na chakula chake kwa ajili yangu. Katika kufunga saumu kuna furaha mbili: furaha (ya kwanza) ni pale anapofungua saumu aliyefunga, na furaha (ya pili) ni wakati (aliyefunga) atakapokutana na Mola wake. Na harufu inayotoka kwenye kinywa cha aliyefunga ni nzuri sana mbele ya Mwenyezi Mungu kushinda harufu ya miski”. [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
1. Ni mja kupata ucha Mungu kwa kuitika amri ya Mola wake amri hii ya kufunga na kujitolea muhanga kuitekeleza sheria ya Mola wake. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlioamini! Mmelazimishwa kufunga (saumu) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu} (Al-Baqarah- Aya 183).
2. Kuipa nafsi mazoezi ya kusubiri, na kujipa nguvu ili kuweza kushinda matamanio.
3. Kujizoezesha mtu kufanya hisani, na kuwa na huruma kwa wanaohitaji masikini na mafukara; kwa sababu mtu anapoonja hisia ya njaa itampelekea mtu huyu kuwa na moyo laini na kuhisi jinsi wanavyohisi ndugu zake wahitaji wasio na chochote cha kula.
4. Kupata raha ya kiwiliwili na afya bora katika kufunga.
Nayo iko sampuli mbili:
1. Saumu aliyoiwajibisha Mwenyezi Mungu U kuanzia mwanzo wake (mwanzo wa hii saumu – chanzo chake) kwa mja wake, nayo ni saumu ya kufunga mwezi wa ramadhani, na saumu hii ni nguzo moja wapo katika nguzo za Uislamu.
2. Saumu ambayo kwamba mja ndiye anayekuwa sababu ya kuwajibishwa yeye mwenyewe kuifunga, kama vile saumu ya nadhiri na saumu ya kafara.
Nayo ni kila saumu ambayo kwamba sheria ya kiislamu imependekeza saumu hiyo kufungwa, kama kufunga siku ya Jumatatu na Alhamisi, na kufunga siku tatu za kila mwezi, na kufunga siku ya A’shura, na kufunga masiku kumi ya mwanzo wa mwezi wa Dhilhijja, na kufunga siku ya A’rafah.
1. Uislamu: Haimlazimu kafiri kufunga.
2. Kubaleghe: Sio lazima kwa mtoto mdogo kufunga, lakini huamrishwa kufunga akiwa anaweza ili kumpa mazoezi ya saumu naye azoee.
3. Kuwa na akili: Sio wajibu kwa mwendawazimu kufunga.
4. Uwezo wa kufunga: Sio wajibu kufunga kwa mtu ambaye hawezi kufunga (labda amekuwa mzee sana ama afya yake haimruhusu kuhimili saumu).
Kufunga mwezi wa Ramadhani ni nguzo mojawapo kati ya nguzo za Uislam, na ni lazima kufunga mwezi huu. Mwenyezi Mungu amewalazimisha waja wake kufunga.
Anasema Mwenyezi Mungu mtukufu: {Enyi mlioamini! Mmelazimishwa kufunga (Saumu) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu} (Al-Baqarah –Aya 183).
Na amesema Mtume (saw): “Uislamu umejengwa kwa mambo matano” [Imepokewa na Bukhari.] na akataja miongoni mwa mambo hayo: “kufungu saumu ya mwezi wa Ramadhani”.
1. Kufunga na kusimama usiku katika mwezi wa Ramadhani hali ya kuwa mtu ana imani na kutaraji malipo basi husamehewa madhambi yake yote yaliyopita. Amesema Mtume Mtume (saw): “Atakayefunga mwezi wa Ramadhani hali ya kuwa ana imani na kutaraji malipo husamehewa yote yaliyotangulia katika madhambi aliyoyafanya” [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
Na akasema Mtume Mtume (saw): “Atakayesimama (kuswali usiku) katika mwezi wa Ramadhani hali ya kuwa na imani na kuridhia atasamehewa yote yaliyotangulia katika madhambi aliyoyafanya” [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
2. Ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna ‘Lailatu Al-Qadr’ – ‘Usiku wenye hishima kubwa’ ambao kwamba Mwenyezi Mungu. U amesema kuhusu usiku huu: <> (Al-Qadr – Aya 3).
Atakayesimama usiku huu basi atasamehewa madhambi yake yote yaliyotangulia. Amesema Mtume Mtume (saw): “Yoyote atakayesimama usiku wa cheo hali ya kuwa na imani na kuridhia atasamehewa yote yaliyotangulia katika madhambi yake” [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
3. Kufanya U’mrah ndani ya mwezi wa Ramadhani ni sawa na kuhiji pamoja na Mtume Mtume (saw). Amesema Mtume Mtume (saw): “Kufanya U’mrah ndani ya Ramadhani ni sawa na kuhiji pamoja nami” [Imepokewa na Muslim.].
4. Mwezi wa Ramadhani hufunguliwa milango ya peponi, na hufungwa milango ya motoni, na hutiwa minyororo (hufungwa) mashetani, na nafsi huelekea katika kufanya mambo ya kheri. Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtume (saw): “Unapoingia mwezi wa Ramadhani hufunguliwa milango ya mbinguni, na hufungwa milango ya motoni, na hutiwa minyororo mashetani” [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
5. Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa Qur’an, na ndiyo mwezi ulioteremshwa Qur’an, kwa hivyo inafaa kuzidisha kusoma Qur’an ndani ya mwezi huu, Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwezi wa Ramadhani ni mwezi ambao imeteremshwa Qur’an katika mwezi (huo)} [Al-Baqarah – Aya 185]
6. Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa ukarimu na kutoa sana sadaka. Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas t akisema: “Alikuwa Mtume (saw) mkarimu sana kushinda watu wote katika kufanya mambo ya kheri, na alikuwa mkarimu zaidi wakati wa mwezi wa Ramadhani, hakika Jibril alikuwa akikutana na Mtume kila mwaka katika mwezi wa Ramadhani mpaka uishe mwezi, basi ikawa Jibril wakati kama huu anampitishia Mtume (anaregelea kusoma pamoja na Mtume) Qur’an, basi pindi Mtume anapokutana na Jibril alikuwa Mtume mkarimu sana katika mambo ya kheri kushinda upepo mkali uliotumwa” [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
Inathibiti kuingia mwezi wa Ramadhani kwa kuonekana kwa mwezi, utakapoonekana mwezi baada ya kuzama kwa jua siku ya ishirini na tisa katika mwezi wa shabani, basi itakuwa umeshaingia mwezi wa Ramadhani, na ikiwa haukuonekana mwezi baada ya kuzama kwa jua siku ya thelathini ya mwezi wa shabani, au hali ikatanda wingu bila kuonekana mwezi, au kukawa na vumbi kali, au kukawa na moshi (wa umande wa baridi), itakamilishwa mwezi wa shabani siku thelathini; kwa kauli ya Mtume Mtume (saw): “Fungeni kwa kuonekana kwa mwezi na fungueni kwa kuonekana kwa mwezi, na ikiwapitikieni kwamba hamuuoni mwezi basi hisabuni siku thelathini (kukamilika shabani)” [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
Kula ndani ya mwezi wa Ramadhani (yaani nyakati za mchana) ni haramu na ni katika madhambi makubwa, na atakayefungua siku moja tu bila ya udhuru wowote na wala asitubie basi hatokubaliwa saumu ya mwaka mzima hata akifunga, kwa kauli ya Mtume Mtume (saw): “Atakayekula siku moja katika mwezi wa Ramadhani bila ya ruhusa yoyote aliyoiruhusu Mwenyezi Mungu hatokubaliwa mtu huyu saumu ya mwaka mzima” [Imepokewa na Abuu Daud.].
Na dhambi la kula ndani ya mwezi wa Ramadhani ni kubwa sana, kutoka kwa Abi Umaamatu Albaahiliy amesema: “Nilimsikia Mtume Mtume (saw) yuwasema: Pindi mimi nilikuwa nimelala walinijia watu wawili ….., kisha wakaniondokea, nikawa nimefika mahali pa watu ambao wamefungwa sehemu zao za nyuma ya magoti wametanuliwa sehemu za pambizoni mwa midomo yao, sehemu zao za pambizoni mwa midomo inatona damu. Akasema: Nikauliza: Ni kina nani watu hao?. Akasema: Hao ni wale ambao kwamba wanakula kabla ya kukamilika kwa saumu zao) [Imepokewa na Ibnu Hibbaan.]
Asema Ibnul-Qayyim Mungu amrehemu (Na alikuwa mtume (saw) Katika muongozo wake kwnye mwezi mtukufu wa Ramadhani huzidisha sampuli nyingi za Ibada, Alikuwa jibril (AS) Akimsomesha yeye Qur’ani katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Alikuwa anapo kutana na jibril ni mkarimu zaidi kwa mambo ya kheri kushinda upepo uliotumwa, na Alikuwa ni mtowaji zaidi wa kushinda watu na Ramadhani alikuwa zaidi akizidisha kutoa sadaka na kufanya wema na kusoma Qur’ani na kuswali na kumtaja Mwenyezi Mungu na kukaa Itikafu na alikuwa akiukhusisha mwezi wa Ramadhani kwa ibada Asiyo yakhusisha katika miezi mengine mpaka mara nyingine akiunganisha saumu ili akapate masaa mengi ya kufanya Ibada).
Imependekezwa katika nyakati bora kama Mwezi wa Ramadhani haswa katika masiku kuzidisha kusoma Qur’ani kwa ijili yakufaidika kwa Wakati.
Huyu hapa imamul –Bukhari mungu amrehemu alikuwa usiku wa kwanza wa mwezi wa Ramadhani Wakijikusanya kwake marafiki zake akiwaswalisha na akisoma kila rakaa aya ishirini, akifanya hivyo mpaka akimaliza Qur’ani. Na alikuwa wakati wa maladaku akisoma kati ya nusu na thuluthi ya Qur’ani, na akikhitimisha Qur’ani wakati wa kufunguwa saumu kila usiku na Akisema kila unapo maliza msahafu kuna dua isiyo rudishwa
Na imepokewa kuwa imamu shafi alikuwa akikhitisha Qur’ani mara sitini mbali na zile anazo soma katika Swala