Anaweza Kuswali Na Damu Inayotoka (Nifasi) Baada Ya Kusafishwa Mimba, Ijapokuwa Hakuzaa

SWALI: Assalaamu alaikum warrahmatullahi wabarakatu Swali linamtatiza dada yetu kwa kupewa majibu tofauti,swali lenyewe ni hili: Dada amekuwa mja mzito kwa miezi 3, na mimba hiyo ikawa haina mafanikio yaani ikafika wakati mtoto matumboni hakui tena na ikabidi hiyo mimba itolewe. Baada ya dada yetu kusafishwa ikawa damu inatoka kama kawaida ya mwanamke akisha zaa. Jee anaweza kuswali na hiyo damu ijapokuwa hakuzaa? Jazaakumullahu khairan. wassalaamu alaikum warahmatullahi wabarakatu

JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani kwa swali lako kuhusu kutoa mimba kwa dada yetu na kuwa bado anatokwa na damu. Damu hiyo inayomtoka mwanamke aliyeharibu mimba na kisha kusafishwa ni damu ya nifasi. Kwa hiyo hawezi kuswali wala kufunga mpaka isimame kutoka. Tafadhali bonyeza viungo vifautavyo upate maelezo na manufaa zaidi: Ameharibu Mimba Karibu Na Miezi Mitatu. Je, Damu Inakuwa Ya Aina Gani? Nifaas Au Istihaadhah? Mwenye Kuharibu Mimba Na Hukmu Ya Damu Ya Nifaas Anapoharibu Mimba, Afanye Wudhuu Au Ghuslu? Na Allaah Anajua zaidi




Vitambulisho: