JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani zetu za dhati kwa maswali yako kuhusiana na kusoma Qur-aan kwa Kiarabu, kuvaa buibui na kuhesabu Zakaah. Ama kuhusiana na kusoma Qur-aan kwa Kiarabu ni jambo ambalo ni zito ila unachotakiwa kufanya ni kujiunga na darasa la usomi wa Qur-aan au kujifunza Kiarabu. Inategemea uko wapi? Lakini popote ulipo jaribu kupata na kuulizia kuhusu Islamic centre iliyopo au Msikiti. Na ukienda hapo Insha’Allaah watakusaidia. Ama kuhusu kutovaa buibui ni makosa kwa Allaah Aliyetukuka Ameamrisha uvaaji wake, pale Aliposema: “Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo ni karibu zaidi kuweza kutambulikana wasiudhiwe” (al-Ahzaab [33]: 59). Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) amehimiza hilo katika Hadiyth zake nyingi sana. Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi: Fadhila Za Hijaab Hijaab Hijaab Ya Sheria Inahusu Kufunika Uso Na Miguu? Kuvaa Niqaab Ni Fardhi? Nini Hukmu Ya Mwanamke Kuvaa Suruwali? Ama utoaji wa Zakaah inategemea na pesa, wanyama au mazao. Lakini nadhani lndugu yetu anataka kutoa Zakaah za mali. Zakaah hizo kutolewa ni lazima zitimize masharti mawili ya msingi: Uwe na akiba ya pesa ambayo inaweza kununua dhahabu safi gramu 82. Akiba hii ikae kwa mwaka mzima bila ya kupungua (mwaka wa kalenda ya Kiislamu). Masharti hayo yakitimiwa basi mwenye hizo pesa baada ya mwaka atatoa asilimia 2.5 (2½%) ya akiba yake. Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi: Zakaah Kipi Kiwango Cha Zakaah, Je, Inafaa Kutolewa Kwa Ajili Ya Madrasa? Na Allaah Anajua zaidi.