Aina nyengine za zaka

8268

 

Zaka ya madeni

Deni

Mali ambayo ni lazima kulipwa na mtu aliyechukua mkopo.

Hukumu ya zaka ya madeni yanayowajibika kulipwa na mtoaji zaka.

Ikiwa mtu ana deni kiwango chake chafika nisabu au kiko chini ya nisabu basi deni hili halimuwajibishi mtu huyu kutoa zaka. Na ikiwa deni halipunguzi nisabu basi atatowa kutoka kwa mali yake kiwango cha deni hilo, na atowe zaka katika mali iliyobaki.

Mfano: Ikiwa mtu ana (Dolari 10000), na deni (anadaiwa) (Dolari 10000), basi haimlazimu kutoa zaka; kwasababu deni hilo limemaliza nisabu, na vile vile ikiwa deni ni (Dolari 9950), basi deni hili linapunguza nisabu hivyo basi hawajibiki kutoa zaka, ama ikiwa deni lake ni (Dolari 4000), basi atapunguza kutoka kwa mali yake kiwango cha deni hilo, na itabakia na (Dolari 6000) ambazo zinawajibika kutolewa zaka

Isipokua achukue mtu deni na asitumie kwa lengo la kibiashara, kama mtu anunue nyumba kwa njia ya kulipa kidogo kidogo (hire purchase)au atumie deni kwa kufanya miradi ambayo inaokadiriwa kwa mamilioni ya pesa, huenda akaamua mmoja wa wafanyi biashara kupanua biashara yake, na kunua kutoka kwa pesa hizo jambo la kuzalisha, je deni hilo lilo zalisha mali itaangusha zakaa?

Kusema hizo ni kupotea mali inaopaswa kutoa zakaa kwa mafukara, pia inamaana kua wafanyi biashara wa leo hawaruhusiwi kutoa zakaana limemelizika kungamao lilofanywa kuweit mwaka wa 1409 hijri sawa na 1989 Miladi kwa yanayofuata:

Hukumu ya zaka ya madeni yanayostahiki mtoaji zaka kutoa.

1. Ikiwa kuna udhuru wa kutolipwa deni, kama vile kufilisika kwa anayedaiwa, au ni mkaidi katika kulipa, halazimiki hapa mwenye kudai kutoa zaka kila mwaka, isipokuwa atatoa zaka mwaka mmoja tu pale atakapolipwa.

2. Ikiwa hakuna udhuru wowote wa kulipwa deni, kama vile awe anayedaiwa si mzito wa kulipa, na ametia nia kulipa, basi hapa yamlazimu mtu kutolea deni hili zaka kila mwaka; kwasababu iko katika hukumu ya vitu alivyonavyo.

Zaka ya shahada na stakbadhi za viashirio vya umiliki au kima cha pesa

Shahada ya kiashirio cha umiliki au kima cha pesa.

Ni shahada au stakbadhi inayowalazimu watoaji shahada kumpatia aliyobeba shahada hio kiasi cha pesa zilizo tajwa wakati akistahiki kupewa, pamoja na kutoa faida ya masikizano iliyo sawa na kima cha kutajwa katika shahada hiyo.

Na hii ni riba iliyowazi kabisa na ni haramu; kwasababu deni hili limeambatanishwa na faida, basi hizi shahada kwa ujumla hazifai; kwa sababu ni deni pamoja na faida waziwazi, basi ni juu ya kila anayehusika na mambo haya kuomba toba kwa Mwenyezi Mungu U.

Hukumu ya zaka ya shahada za viashirio vya umiliki au kima cha pesa, na kiwango cha kutolewa zaka.

Zaka ya shahada ya kiashirio cha umiliki au kima cha pesa inachukuwa hukumu ya zaka ya deni, basi inawajibika kutolewa zaka pale inapofikia nisabu yenyewe, au pale inapochanganywa na anavyomiliki mwenye mali katika pesa zake au bidhaa za biashara, na ikakamilisha mwaka mzima, basi itatolewa robo ushuri. Na ikiwa shahada hizo haziwezi kuvunjwa kubadilishwa pesa ila baada ya muda fulani, basi bado zaka yake ipo pale pale, lakini itatolewa zaka wakati wa kuvunjwa kubadilishwa pesa kwake kwa kila mwaka uliyopita.

Zaka ya malipo ya ziada ya mwisho wa kazi na malipo ya ziada ya uzeeni na mishahara ya uzeeni

Malipo ya ziada ya mwisho wa kazi

Ni kiwango cha pesa kinachokatwa kutoka kwa mfanya kazi, anastahiki mfanyakazi kutoka kwa muajiri wake mwisho wa kuacha kazi kwa mujibu wa kanuni na nidhamu, yanapotimia masharti yaliyowekwa kwa jambo hili.

Malipo ya ziada ya uzeeni

Ni kiwango cha pesa kinachokatwa. Inatolewa na serikali au mashirika maalumu kupewa wafanyikazi au mfanyikazi anayehusika na kanuni za bima ya jamii, ikiwa mtu huyu hakukamilisha masharti yanayohitajika kwake ili kupata mishahara ya uzeeni.

Mshahara wa uzeeni

Ni kiwango cha pesa anachostahiki kupewa mfanyikazi wa serikali au shirika maalumu kwa kila mwezi, baada ya kumaliza miaka yake ya huduma ya kazi kulingana na kanuni na nidhamu, ikiwa ametimiza masharti yanayohitajika.

Hukumu yake.

Hamlazimu mfanyikazi kutoa zaka mda wake wote anaofanya kazi kwa ajili ya malipo haya ya mwisho, kwa kukosekana umiliki uliyokamilika ambao kwamba ndio sharti la mtu kuwajibika kutoa zaka, kwa maana mfanyikazi huyu hawezi kutumia pesa hizo ndani ya kipindi chake cha kufanya kazi, wala hana haki yoyote ya umiliki wa pesa hizo katika kipindi chake cha kazi.

Pesa hizi inapopitishwa sheria ya kuhisabiwa na kupewa mfanyikazi zote kwa pamoja, au kupewa kwa kipindi cha mizunguko fulani (kama kila mwezi hivi) hapa itakuwa ni mwenye kumiliki mali hii kiukamilifu, na atatoa zaka kile atakachopata miongoni mwa hizo pesa (alizopata kwa mara moja) zaka ya mali yakufaidisha.

Zaka za mali zinazo kodishwa

Mali zinazi kodishwa

Kila kilicho andaliwa kwa ajili ya kukodishwa na sio andaliwa kwa ajili ya biashara katika vitu venyewe hasa, kama majengo na magari na viwanda vinavo zalisha

Wamekubaliana wanavyoni kwaba hakuna zaka ya vitu hiyo, na zakae zinatolewa zaka ya faida yake inayopatikana inajumushwa na nisabu na mwaka kwa kile anachomilili katika pesa na mali ya biashara na atatowa robo ya fungu lakumi 2.5% zaka yake ni kama zaka ya pesa

Zaka ya mali ya bima inayotolewa na mfanyikazi.

Mali ya bima

Pesa ambazo mfanyikazi anazitanguliza kwa mwenye kazi kwa mkataba (yaani mfanyikazi hachukuwi pesa hizi- zinakaa kwa mwenye kazi ili mfanyikazi apate huduma fulani pindi anapokumbwa na matatizo).

Haimlazimu mfanyikazi kuitolea zaka; kwasababu haimiliki mali hii, hivyo basi hajapata umiliki uliokamilika, ambao ni sharti ya mtu kuwajibika kutoa zaka.

Zaka ya haki za Hisia

Haki za Hisia

Ni utawala wa mtu juu ya kitu kisichonekana na kushikwa, sawa kiwe kitu kile ni matokeo ya juhudi yake ya kiakili, kama vile haki ya mwandishi katika vitabu vya mambo ya sanyansi na adabu, ama uvumbuzi wa kitu katika viwanda,. Ama matunda ya harakati za biashara alizofanya mwanabiashara ili kuwavutia wafanyikazi, kama katika jina la biashara na nembo za biashara.

Hukumu ya Zaka ya haki za Hisia.

Haki za hisia zimekuwa katika ada ni zenye kima cha mali inayotambulika kisheria, basi inafaa kuitumia haki hii kulingana na mipaka ya kisheria, nacho ni kitu cha kuhifadhi hadhi ya mtu haifai kuiendea kinyume.

Wala haimlazimu mtu kutoa Zaka katika haki ya uandishi na uvumbuzi wa kitu, kwa kule kukosekana masharti ya mtu kuwajibika kutoa Zaka, lakini inapokuwa ni machumo ya pesa itabidi kwa anayepokea machumo haya kuchukua hukumu ya mali ya kufaidisha [ Qadhwaayaa fiqhiyatu muaa’swirah Dr: Swallaah Asswaawy; uk. 60 na za mbele yake.].

Zaka ya malipo ya kibaruwa, mishahara, na faida ya kazi za mtu binafsi

Malipo ya kibaruwa na mishahara

Kile anacholipwa mfanyikazi kulingana na kazi atakayofanya.

Hukumu yake.

Mali haya hayana zaka wakati ya kuyakabidhi bali hukusanya na mali mengine ya mtu yanayo wajibika kutolewa zaka ikiwa yatafikia kiwango na kupitiwa na mwaka basi atayatolea zaka yote na mali ya faida katikati ya mwaka atayatolea zaka mwisho wa mwaka japokuwa mali yote hayatakuwa ya mepitiwa na mwaka madamu yale mali yake mingine ya mefikia kiwngo na kupitiwa na mwaka kwa jumla. Na kiwango cha kutolewa Zaka ni robo ushuri (2.5%).

Zaka ya Mali Haramu

Mali ya Haramu

Kila mali iliyokatazwa na sheria kuichuma, au kuitumia, sawa uharamu wake ni kule kupatikana madhara au uchafu kama maiti na tembo, ama uharamu wake.kwa sababu ya tumo lake ama kuchukuwa mali bila ya ruhusa ya mwenyewe, au kuchukuwa kwa njia isio kubalika kisheria hata kama ataridhika kama vile riba au hongo.

Hukumu ya Zakka ya mali haramu

Mali iliyo haramu yenyewe- kama mali iliyochumwa kutokana na biashara ya tembo/pombe, na nguruwe – haifai kutolewa Zaka, na vile vile mali iliyo haramu kwa kusababishwa na jambo fulani lililotokea kinyume na sheria – kama mali ya kuibwa; kwasababu ya kukosekana umiliki wamali hayo, ambao ni sharti ya kuwajibika kutowa zaka.na endapo anapo imiliki mali hiyo mwenyewe itampasa kutoa zaka mwaka mmoja hata kama amepitiwa na miaka kwa rai iliochaguliwa

Na mwenye kumiliki mali ya haramu na asimregeshe mwenyewe na akatoa kiwango katika mali hiyo, dhambi itabaki vile vile na alilicho kitoa ni sheria amempasa kufanya hivyo, na haizingatiwi alichokitoa kua ni zaka, na dhima yake itabaki vile vile isipokua amregeshe mwenyewe, au atoe sadaka ikiwa ameshindwa kujua mwenyewe

Maelekezo (Jinsi ya kutumia mali haramu)

a) Anayekusanya mali haramu kwa makosa aliyofanya kwenye njia ya kuichuma hafai kuimiliki mali hayo hata ikawa umepita mda mrefu kiasi gani, na inamlazimu kuirudisha kwa mwenyewe, au kwa aliorithi - ikiwa anamjua-, akishindwa kumjua inamlazimu aitumie mali hayo katika mambo ya kheri; ili amalize mali hayo, na akusudie kwamba anamtolea sadaka mwenye mali.

b) Anapolipwa mtu pesa kwa kufanya kazi iliyo haramu basi mwenye kulipwa anafaa kuitumia katika mambo ya kheri, wala asiirudishe kwa aliyempa; kwa vile kumrudishia itakuwa ni kusaidiana katika mambo maovu.

c) Hairudishwi mali haramu kwa mtu aliyechukua kwake ikiwa anajua kwamba anashughulika na mambo yaliyo kinyume na sheria ambayo yamesababisha uharamu wa mali yake, kama vile faida za riba; bali pia utazitumia katika njia za kheri.

d) Ikishindikana kuirudishwa mali haramu yenyewe, inamlazimu mtu huyu kurudisha mali mfano wake; au kima chake kwa mwenyewe ikiwa anamjuwa, ikiwa hamjuwi ataitumia hiyo iliyo mfano wa aliopata, au kima chake katika njia ya kheri, na aikusudie kwamba ni sadaka anamtolea mwenye mali [ Qadhwaayaa fiqhiyatu muaa’swirah Dr: Swallaah Asswaawy; uk. 61 na za mbele yake.]

e) ikishindikana kuregesha mali ya haramu yenyewe itampasa kuregesha mfano wakeau thamani yake kwa mwenyewe akimjua, venginevvyo mfano wake au kima chake katika mambo ya kheri, na akusudie sadaka hio kwa mwenyewe.